Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,733
- 218,322
Ile Taasisi bora ya akina mama barani Africa, na ambayo inatajwa kushika namba 3 kwa ubora duniani kwa sasa, BAWACHA, Imeishika Nchi kwa kiganja kimoja cha mkono wa kushoto.
Pamoja na kwamba Bawacha ni Taasisi ya wanawake, lakini nguvu kubwa inayotumiwa na Jeshi la Polisi kuwadhibiti bila kufuata PGO, tena bila Mafanikio inazidi kuipaisha Taasisi hiyo
Kwa kifupi ni kwamba hoja za Polisi za kujaribu kuhusisha Jogging za Bawacha na harakati za kisiasa HAZINA MASHIKO, BAWACHA ni Taasisi ya kisiasa, chochote watakachokifanya hauwezi kukitenganisha na siasa, kiongozi wa kisiasa hawezi kubadilika kwa mavazi, hata akiingia Kanisani au Msikitini atabaki kuwa mwanasiasa tu, hata akihudhuria msiba bado TAITO yake ya uanasiasa haitapotea, udiwani wake, ubunge au uenyekiti wake hautaondoka kwa vile yuko kwenye mazishi.
Kwahiyo kuwazuia BAWACHA kufanya mazoezi kwa vile ni viongozi wa kisiasa, au labda kutaka wanasiasa hao wafanye mazoezi yao au Jogging zao huku vyeo vyao wameviacha nyumbani ni KITUKO kisichowezekana, Polisi ni lazima iseme ni namna gani kiongozi anaweza kujitokeza kama raia huku akiacha cheo chake nyumbani, na ni wakati gani ambao anapaswa kutembea na cheo chake, kwa mfano, ni wakati gani Waziri labda Jenister Mhagama anakuwa Waziri ni wakati upi anakuwa Raia? bila shaka si rahisi.
Bali Polisi wanapaswa kulinda amani na usalama tu, wakianza kupiga ramli na kuzuia wengine kukimbia barabarani kwa Visingizio vya kichovu watajidhalilisha tu, uonevu duni kama huu hautasaidia Polisi katika lolote na wala HAUTAFANIKIWA, zaidi utatengeneza Uhasama wa Kudumu.