Ngorongoro ilishachukuliwa kitambo...

Naomba nisizungumzie mnunuzi kwakuwa hilo neno halipo kwenye mada yangu hii bali unaweza kunisaidia kuyajibu haya

*Ni nani alifadhili mchakato wa Environment Impact Survey ya Wamasai kuharibu mbuga ya Ngorongoro?

*Ni nani alifadhili utafutaji na ununuaji wa eneo la Handeni Tanga ili Wamasai wa Ngorongoro wahamishiwe huko?

*Ni nani alifadhili ujenzi wa nyumba na miundombinu ya Handeni?

*Ni nani alifadhili fidia malipo na bakshish ya waliokubali kuhama?

Serikali huwa na bajeti yake ya mwaka na kila pesa hupitia bungeni je hili lilifanyika? Kama LA je ni nani yuko nyuma ya haya yote?[emoji848]
 
Ndiyo sasa mfahamu mna serekali makini na inayojali inaona tatizo na inajitahdi kulitatua kwa faida ya wanyama wetu na vizazi vijavyo...
kiongozi mwingine anakufukuza anakubomolea na hana habari na wewe tena! #MASAI_MUST_MOVEOUT_PEACEFUL
 
Upareni WAP tena mbona tunatishana
 
Ukiwa mtu mzima afu unaanzi nyuzi za kipumbuvu inakera.
 
Kuna siku ambayo wananchi tutaamua kufanya yetu na hiyo ndio siku ambayo kila aliyewahi fanya maasi dhidi ya wananchi atakatwa kichwa la sivyo akimbie hii nchi. Mmetushika vichwa tumewaacha naona wanataka kutushika na nyeti.
Hawa watanzania ninao wajua ?
 
Na wakimaliza hapo wanahamia bagamoyo , twende taratibu , si ndo uongozi mliokuwa mnaulilia , baada ya hapo wanahamia Mlima mlima kilimanjaro...mpak barabara atapewa mwekezaji , ni swala la mda tuu
 
Toa hoja amechemka kitu gani siyo unalalamika bila hoja ya kueleweka. Jibu maswali yake hapo juu kuhusu fedha ilipitia bunge gani kuhamisha wamasai!!
Akiweza kukujibu walau moja najitoa JF
 
Na wakimaliza hapo wanahamia bagamoyo , twende taratibu , si ndo uongozi mliokuwa mnaulilia , baada ya hapo wanahamia Mlima mlima kilimanjaro...mpak barabara atapewa mwekezaji , ni swala la mda tuu
Wote ni wale wale kwani ya Chato huyajui ama unataka kuyapotezea?
 
Nimetokwa machozi mimi
 
Hivi yule mtetezi wao bungeni alirestishwa in peace alipoanza kutetea wamasai ee?
 
Naona umekwepa kujibu maswali yangu na kuchomekea kitu kingine, Rejea kwenye hoja husika tafadhali ili kuonesha weledi na ukomavu
Yapo mambo kwa akili ndogo tu ya kiuanadamu unaona kabisa hili silo, unaona kabisa watu wanachota mchanga kwenye kingo za daraja unangoja utafiti kwanza ufanyike badala ya kuwaondoa haraka"
 
Je, unaweza kuleta uthibitisho dhidi ya hizo tuhumu kuwa Ngorongoro ilishachukuliwa au umeota usingizini ukaja kuandika hapa?
 
Huu ni mchanganyiko sirahisi kujua nani ni nani na upi ni upi, sasa kilichobaki [emoji125] CHANGANYA MALUNDI PEPEA KIVYAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…