Diamond kwa kwel umenisikitisha sana..alipokuja Neyo na ikasemekana kwamba mtatoa ngoma pamoja nilijua sasa kijana anaanza kuchomoza na kupasua anga kwa kasi..nikawa na hamu sana ya kuisikia ngoma yenyewe itakavyokua nzuri na kali...
Nilipoanza kusikia kua nyimbo imeshakua released kwakwel nilikimbilia kudownload kwa haraka ili nisikie ngoma kali ambayo nilikua natarajia itateka akil yangu kwa mapenzi niliyonayo kwa muziki.
Nimeanza kusikiliza ...daaah...sikuamini...nkajua labda nimekosea kuchagua track kwenye simu yangu...nikaangalia vizuri..ndo yenyewe bwana..nimesikiliza hadi mwisho nikaishia kusikitika tu nkawa najiuliza diamond ndio ameanza kufanya vitu gani sasa...wadau wapenda mziki na mnaojua mziki na kusikiliza mziki..sio washabiki hivi huu wimbo mmeuelewa kweli? ndivyo ilivyokua inatarajiwa kweli??
Ukweli baada ya kusikiliza nyimbo hio haikukaa zaidi ya dakika 15 katika simu yangu nkawa nshaiondoa. Nkabaki na zile zile ambazo diamond alizifanya kwa umakini mfano "Kidogo" na "salome".
Bora hata "my heart" aliyoimba na casper nyovest unaweza kuisikiliza au hata hii mpya alioimba na mavoko. Diamond ajitafakari upya. Unawanyima haki wapenz wako kusikiliza mziki mzuri.
View attachment 438237