Kwa kawaida msanii anayetokea sehemu ambazo ladha zake haziko kimataifa hua inambidi abadilishe mtindo wa kuimba/ kurap na hata beat hubadilishwa ili kumpa nafasi yule mwenye ladha ya kimataifa atambe.
Mfano AY alivyoimba na Lil Romeo ilibidi asirap kabisa ili kumpa nafasi Romeo, 2 Face alivyoimba na T pain ikabidi beat iwe ya reggae ili T pain apate pa kuhemea. Drake alijikaza kwenye Ojuelegba ya Wizkid lakini kama unajua rap utajua tu pale hakua Drake wa siku zote.
Kwa vyovyote Diamond ilibidi awe na beat ambayo Neyo angekaa na yeye angekaa, matokeo yake imewekwa beat ambayo haiwezi kukubalika Afrika wala huko Marekani na hata mashairi hayako poa, hii beat ni ya klabu tena uwe umelewa, wimbo hauko poa kwa kifupi katika nyanja zote (labda video ikitoka).