Ngoja niropoke

Haya someni hizo hapo juu mpate kujua kwa hakika kwanini haya yanatokea sasa.. Adam hakuwahi kukosa changamoto toka jinsia pinzani.. Toka Lilith mpaka Eva!
Baada ya kushindwana na Lilith, Mungu akamletea Eva lakini naye bado akazingua vilevile.. Hapa tunapata tafsiri gani?
Mchukulie Lilith ndio hawa wanawake wasomi wa kileo... Mostly they are beyond control! Na mchukulie Eva kama mwanamke asiyesoma wa kileo unamshape mwenyewe utakavyo.. Wengine wanafit kwenye model shaping yako. Wengine akishajua ABC wanakuwa kama Lilith

Hivyo basi Mwenyezi Mungu hakuona sababu ya kumtafutia babu yetu Adam dizaini ya tatu akajua nayo itazingua tuu ndio maana mwishowe akaja na suluhu ya kusema ISHINI NAO KWA AKILI
Kwamba mwanaume uwe mpole kama HUA (njiwa) lakini uwe mwerevu kama Nyoka (ibilisi
) Hiyo ndio akili ya kuweza kuishi na Sweet heart wako na mkafika mbali sana! Ukishindwa kuishi basi tambua huna akili!


Kuchapiwa hakukuanza leo
Je unajua mtoto wa kwanza wa Adam hakuwa wake!? Huyu ndio matokeo ya Eva kukutana na Nyoka pale Eden na kula tunda la mti wa kati.....lakini hii ikawa siri ya Eden.. Dah


Ya mwisho ni hapa!
Mungu akambariki Mfalme Suleiman kwa HEKIMA na UTAJIRI halafu akamuongezea bakshish ya LIBIDO
Jamaa akaoa WAKE halali wa ndoa 700 na bado wakawa hawamtoshi akaongeza na MASURIA (vimada) 300.. Salute kubwa sana kwa huyu mwamba!
Ila bado dhambi ya usaliti haikumuacha salama akamla mke wa mjakazi wake! Unafunzwa nini hapa!? Mwanaume HATOSHEKI...Na mwanamke ku cheat ni asili
msinipige mawe..
sio maneno yangu ni Maandiko
Siropoki tena!
 
Kuzaa kwa tabu kwa mwanamke na mwanaume kula tabu so tambua akiwa na uwezo kuliko wewe utakula tuu kwa tabu
 
Hao unaowatongoza na kuwapa jeuri kuwa achana na huyo jamaa nitakutunza mbona hujawataja?

Na hao walokole mnaowalaghai nao umewasahau.

Mind you kuwa hao wanawake wengi wanaotaka talaka licha ya usomi wao ni watoto wenu nyie wenye vihela, mnawapa jeuri, inakuwaje kwenye sendoff umpe binti yako nyumba mbili, kiwanja, mtaji wa biashara ? Hapo unampa kichwa na kibri

Mashangazi wa kitchen party nao utasikia.. sufuria huwezi injika kwa mafiga moja au mbili, .. sawa aunt eeh ?

Wapo pia wenye wivu wetu, nikihakikisha umechepuka, sina msalia Mtume, mi nafungasha.

Ukiongeza na ki elimu na jeuri yenu wanaume ndo hayo ya kutaka talaka.
 
Kula miwa popote hapo nalipia kwa pesa ya tozo.
 
"Ni kweli umefanikiwa kielimu, pengine una mshahara mkubwa, au biashara zako zinaenda safi, una cheo/position fulani somewhere lakini WEWE BADO NI MWANAMKE".

Nakazia hapo.
 
Mwanamke msomi hayuko tayari kutumikishwa kwa mujibu wa Mila za mfumo dume zinazokumbatiwa na Wanaume wa Kiafrika..

Huu ndio ukweli mchungu ikizingatiwa kwamba wao sio tegemezi kama wale wasioenda shule so wanaume ndio wa kubadili Mtizamo..
Kutumikishwa ni kupi?
Kumpikia mme na kumtengea chakula?
Kumpokea akitoka kazini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…