Ngoja niropoke

Ngoja niropoke

Haya someni hizo hapo juu mpate kujua kwa hakika kwanini haya yanatokea sasa.. Adam hakuwahi kukosa changamoto toka jinsia pinzani.. Toka Lilith mpaka Eva!
Baada ya kushindwana na Lilith, Mungu akamletea Eva lakini naye bado akazingua vilevile.. Hapa tunapata tafsiri gani?
Mchukulie Lilith ndio hawa wanawake wasomi wa kileo... Mostly they are beyond control! Na mchukulie Eva kama mwanamke asiyesoma wa kileo unamshape mwenyewe utakavyo.. Wengine wanafit kwenye model shaping yako. Wengine akishajua ABC wanakuwa kama Lilith
Hivyo basi Mwenyezi Mungu hakuona sababu ya kumtafutia babu yetu Adam dizaini ya tatu akajua nayo itazingua tuu ndio maana mwishowe akaja na suluhu ya kusema ISHINI NAO KWA AKILI
Kwamba mwanaume uwe mpole kama HUA (njiwa) lakini uwe mwerevu kama Nyoka (ibilisi) Hiyo ndio akili ya kuweza kuishi na Sweet heart wako na mkafika mbali sana! Ukishindwa kuishi basi tambua huna akili!

Kuchapiwa hakukuanza leo Je unajua mtoto wa kwanza wa Adam hakuwa wake!? Huyu ndio matokeo ya Eva kukutana na Nyoka pale Eden na kula tunda la mti wa kati.....lakini hii ikawa siri ya Eden.. Dah

Ya mwisho ni hapa!
Mungu akambariki Mfalme Suleiman kwa HEKIMA na UTAJIRI halafu akamuongezea bakshish ya LIBIDO Jamaa akaoa WAKE halali wa ndoa 700 na bado wakawa hawamtoshi akaongeza na MASURIA (vimada) 300.. Salute kubwa sana kwa huyu mwamba!
Ila bado dhambi ya usaliti haikumuacha salama akamla mke wa mjakazi wake! Unafunzwa nini hapa!? Mwanaume HATOSHEKI...Na mwanamke ku cheat ni asili
msinipige mawe.. sio maneno yangu ni Maandiko
Siropoki tena!
 
Hao unaowatongoza na kuwapa jeuri kuwa achana na huyo jamaa nitakutunza mbona hujawataja?

Na hao walokole mnaowalaghai nao umewasahau.

Mind you kuwa hao wanawake wengi wanaotaka talaka licha ya usomi wao ni watoto wenu nyie wenye vihela, mnawapa jeuri, inakuwaje kwenye sendoff umpe binti yako nyumba mbili, kiwanja, mtaji wa biashara ? Hapo unampa kichwa na kibri

Mashangazi wa kitchen party nao utasikia.. sufuria huwezi injika kwa mafiga moja au mbili, .. sawa aunt eeh ?

Wapo pia wenye wivu wetu, nikihakikisha umechepuka, sina msalia Mtume, mi nafungasha.

Ukiongeza na ki elimu na jeuri yenu wanaume ndo hayo ya kutaka talaka.
 
Takwimu zinaonesha Wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA), kwa mwaka unapokea maombi ya talaka yasiyopungua 500+ Tanzania nzima.

Kilichonishangaza ni kwamba asilimia 78% ya Ndoa zinazovunjika ni wanawake ndio wanaoomba talaka na kupeleka maombi hayo.

Kilichonishangaza na Kunimaliza zaidi ni kwamba asilimia 89% ya wanawake wanaoomba talaka ni WANAWAKE WASOMI (Intellectual Women)

Swali; Wanawake wasomi wana SHIDA GANI, kwanini kwao talaka ziwe nyingi, kwanini wengi wanasumbuka na mahusiano na kwanini wengi ni single mothers?

Honestly kuna kitu hakiko sawa kwa hawa Intellectual women, kwa takwimu hizi tunaweza kusema elimu zimewaharibu badala ya kuwatengeneza wawe wake bora.

Ndio, haiwezekani asilimia 89% ya maombi ya talaka yakaliwe na wao pekeao, ina maana elimu zao zinawaambia kwamba solution pekee ni talaka, nawaza sana yani

Ngoja niropoke; wanawake wengi wasomi wana kakiburi ka maarifa kanaitwa "INTELLECTUAL ARROGANCE"

Haka kakiburi kanawaambia hivi "wewe ni msomi, una akili, unajiweza na mwanaume hatakiwi kukusumbua kwa lolote lile"

Haka kakiburi kamewafanya wengi washindwe kuwa wanyenyekevu kwa sababu wanajiona ni classy and high, inafika hatua wanaanza kuvimba.

Wengi walifanikiwa sana kielimu kiasi cha kupata fedha, vyeo na status katika jamii vichwa vikaelemewa sifa na kujiona wanajua na kuweza kila kitu.

Pengine ofisini kwao yeye ndo Managing Director na ana watu wengi wakiume wako chini yake kikazi, anataka na mumewe awe chini yake pia.

Elimu yake, cheo na fedha vinamwambia "Unastahili kunyenyekewa na sio kunyenyekea na unaweza kila kitu" wengi hapa ndipo wanapofeli sasa na kuleta mabalaa.

Pengine walipokuwa wanasoma waliambiwa maneno kama "Soma sana, tafuta fedha zako ili mwanaume asikusumbue kwa lolote lile" (hii ndo shida kubwa)

Kwahiyo wengi kuanzia hapo wakawa wanatembea na competetive mentality (fikra za kishindani) na muda wote wapo kinyume na jinsia ya kiume.

Kinachotokea, wakiolewa wanafanya mambo kama washindani (competetors) kwa wanaume wao na sio wapambanaji wenza (teammates)

Kitu kingine kinachowaharibu ni hizi FEMINISTS MOVEMENTS (harakazi zinazodaiwa kumpa nguvu mwanamke na kumkomboa kifikra)

Ukizifuatilia vizuri hizi harakati zinawafanya wanawake wahisi kwamba hata wao wanaweza kuwa kama wanaume since they can pay bills na ada za watoto.

Sikatai, ni kweli kabisa kuna majukumu mwanamke anaweza kuyaperform kama mwanaume lakini haitatokea hata siku moja akawa kichwa cha familia.

Elimu walizopata wengi wao zimewasababishia kakitu kanaitwa "Control Freak Disorder" (unajua ni kanini haka, soma hapa chini)

Ni kale ka akili ka kumtaka mwanamke amcontrol mwanaume na kumfanya mwanaume aenende vile mwanamke anataka (amuweke chini)

Na hii inatokana na ukweli kwamba wengi wameweza kuongoza kakundi ka watu, wengi wameweza kufanya vitu vikubwa katika academic fields zao.

Kitendo cha kufanikiwa kuongoza kakundi ka watu kinawafanya hata kwenye ndoa nafasi ya kuongoza ambayo ni ya mwanaume aitake mwanamke, yaani yeye ndo awe kichwa.

Msuguano unaanzia hapo, mwanaume yeyote yule anataka yeye ndo awe top, ikitokea mwanamke akataka kumshusha mwanaume ili mwanamke awe top balaa linaanza.

Fuatilia, wanawake ninaowazungumzia hapa wengi wana kakiburi, wanajiona, na wanaamini kwamba hakuna kitu wanahitaji kutoka kwa wanaume na wanaweza kila kitu pekeao.

Wanaume wengi wanatafuta fedha ili wahudumie familia zao na kuwatimizia mahitaji, ila kwa wanawake mambo yako kinyume kabisa!

Wengi wanasoma na wanatafuta fedha ili waweze kuthibitisha kwamba wanaweza kufanya kama wanaume, wanaweza kuishi bila wanaume na hawawezi kusumbuliwa kwa lolote.

Ndio maana, kukiibuka kaugomvi kadogo wengi solution inakuwa ni kuachana ili kuthibitisha kwamba "NINAWEZA KUISHI MWENYEWE NA KAMA NI MTOTO/WATOTO NITALEA COZ NINA FEDHA"

Dear ladies, black brother wenu nawakubali kinoma na nafurahi kuwaona vile mnastrugle kupambania ndoto zenu (hongereni kwa hilo)

Lakini, jitahidi kadri uwezavyo fedha zako, elimu yako na cheo ulichonacho/utakachopata visikutie Kiburi mbele ya mumeo uliyenae/utakaekuwa nae.

Ni kweli umefanikiwa kielimu, pengine una mshahara mkubwa, au biashara zako zinaenda safi, una cheo/position fulani somewhere lakini WEWE BADO NI MWANAMKE.

Wakati wowote uwapo mke, mpe nafasi mwanaume awe mume, awe baba, awe kuongozi, awe dereva wa familia huku wewe ukiwa kwake msaidizi.

Hata kama ofisini kwenu una wanaume wengi unaowaongoza na wananyenyekea mbele yako usitake na mumeo akunyenyekee..

Mpe yeye nafasi ya kuwa king, mtii, msikilize na panapohitajika ushauri mpe ushauri kwa upole huku ukionesha kwamba unamuheshimu na kuamini..

Kwanini wanawake wa sahivi wamesoma lakini hawadumu kwenye ndoa kama mama na bibi zetu walioishia darasa la nne/la saba.

Kadri mwanamke anavyoanda juu kielimu, kuna namna anapoteza WIFE TRAITS umakini unahitajika sana ndo mana wengi wanabaki single/single mothers.

Fuatilia wanawake woote unaowajua Tanzania ambao wana vyeo vikubwa, wamefanikiwa kibiashara au wapo top kwenye eneo lolote lile.

Wengi utagundua kwamba hawajawahi kuolewa, waliolewa wakaachika, walizalishwa na wakabaki hapo.

Elimu sio mbaya, fedha sio mbaya..lakini inakuwa mbaya pale inapoanza kumfanya Quuen atake kuwa king, haiwezekani!

[Nimemaliza kuropoka

Credit: WhatsApp forwarded msg
Author: Unknown
Kula miwa popote hapo nalipia kwa pesa ya tozo.
 
"Ni kweli umefanikiwa kielimu, pengine una mshahara mkubwa, au biashara zako zinaenda safi, una cheo/position fulani somewhere lakini WEWE BADO NI MWANAMKE".

Nakazia hapo.
 
Mwanamke msomi hayuko tayari kutumikishwa kwa mujibu wa Mila za mfumo dume zinazokumbatiwa na Wanaume wa Kiafrika..

Huu ndio ukweli mchungu ikizingatiwa kwamba wao sio tegemezi kama wale wasioenda shule so wanaume ndio wa kubadili Mtizamo..
Kutumikishwa ni kupi?
Kumpikia mme na kumtengea chakula?
Kumpokea akitoka kazini?
 
Back
Top Bottom