Ngoja anipigie simu ananiona ----...!

Ngoja anipigie simu ananiona ----...!

lara1 hujui kuwa akitaka jua kama umesafiri atajua tu kwa kukuomba passport?
Watu hata kudanganya hamjui

Hawezi kwani mi majinga nimpe passport yangu? Mpaka katoa hio hela haikuwa kazi nyepesi nimempa referal ya Dr. Muhimbili, chezea nguvu ya muhuri na kuaminika kwa Dr. Ye ataniangalia ugonjwa umepungua?
 
Mimi ukiniweka blacklist natumia namba nyingine kukupigia simu. Pia kwani ukienda kutibiwa ndio mawasiliano yanakatika au sijakuelewa vizuri hapo lara?
Simu gharama tunatumia EMAIL, na face book kuwasiliana. Sasa akiona line ya voda inapatikana si ataona uhuni huu sasa?
 
Nina demu mmoja wa Kichaga huwa tunaburudishana kwa kupeana vyetu,ni mzuri kwelikweli kiasi hata cha kunifanya kwa nini amekuwa Mchaga kwa kuwa ana shepu balaa... sasa juzi kati akanipigia simu akiniambia eti anakwenda Moshi kwa bahati ambaya sikuwa na fedha za nauli nikamwambia asubiri.
Baada ya siku tatu akanipigia akisema kuwa ameshapata nauli na yuko Moshi... daaa! akaniambia sasa jukumu langu ni kumpa nauli ya kurudi, nikaona ni sawa, kwenye mitandao ya kijamii akaanza kuweka picha akiwa kijijini, nikaamini kuwa yuko old Moshi.
Ijumaa akanipigia simu kama nimepata nauli ya kumtumia, nikamwambia Jumapili nitamtumia nauli ili arudi tuendelee na mambo yetu, eeeeh Jumamosi asubuhi nakatiza sehemu nikamuona anashuka ndani ya bajaji, baahati mbaya eneo hilo kuna mtu anafahamu uhusiano wetu. Akaingia ndani kwa mtu anayejua mambo yetu, miye nikapata fursa ya kujibanza sehemu ili nimuone vizuri.
Dakika chache tu akatoka ndani mbio huku akiangaza huku na kule, nahisi aliambiwa uwepo wangu maeneo yale na mtu anayejua uhusiano wetu ambaye kuna muda aliniona na kusalimiana. Mpaka leo sijapata simu yake... siju alijua kama nimemuona au... nasubiri sana simu yake....mademu wengine bwanaaa... najitahidi kummhudumia lakini halidhiki anaendeleza mila za kizamaniiiiiiii....Ananiona miye falaaa...

Kaka imepita mda gan tangu umbambe uyo dem
 
na nyie mnayatafutaga acha yawakute, unamuhudumia mtu ambae wala si mkeo wala ndunguyo kisa nini? umekuwa mzazi wake au kaka yake?

mrsleo kwa mwelekeo wa post yako nahisi upo kwenye ndoa. Je kabla hujaingia kwenye ndoa, hukugharamiwa na aliyekuwa mchumba hata siku moja?
 
wanaume mabwege hawaishi!wakiingia anga zako we kamua tu
Tena we Chizenga ningekupata bila hata stress! Sio WANAUME MABWEGE, SEMA WANAWAKE SMART TUNAJILIA KIULAINI.
THE BIGGER THE LIE THE EASIER IT IS BELIEVED! Ningemdanganya naenda TMJ angesema twende nikupeleke. ILA NJE HATA MTU AKIENDA JIONI HII AMWAMBIE LARA1 ANAKUCHOTA KINGI ATAMUONA HANA HURUMA KWA MGONJWA MIE, HOW CAN HE THINK THAT LOW OF A SICK PERSON..???
 
hahahahaah!!!!! jamani, mpaka mpewe sababu ndio mcheue mayuro. we mrushie nauli mwenzio arudi. loh
 
Bila technic hela mnayoa nyie? Mwenyewe kuna mtu nimemwambia anipe hela mwezi wa 5 naenda nje kutibiwa, kanipa hela ya passport, visa, bado matumizi, mwezi wa 5 namuweka black list atajua nipo nje, siku zikitimia namtoa afu ndo inakuwa nimerudi, MJINI MIPANGO!


Shikamoo kubwa la maadui!
 
Hongera sana mkuu kwa kupata changamoto ambazo zitakukomaza akili. Ktk mahusiano. Tatizo nawewe unamuwazia sana. Akikwambia anasepa wewe kausha then fanya yako. Lol l l l .
 
Bila technic hela mnayoa nyie? Mwenyewe kuna mtu nimemwambia anipe hela mwezi wa 5 naenda nje kutibiwa, kanipa hela ya passport, visa, bado matumizi, mwezi wa 5 namuweka black list atajua nipo nje, siku zikitimia namtoa afu ndo inakuwa nimerudi, MJINI MIPANGO!

mwishowe akuone mjini kwenye mishe mishe kama huyo binti kwenye mada utajielezaje
 
sasa kwa nini mpaka leo ujanitumia nilirudi jmosi bwana ... mbona hivyo tena sikutaki tena mwanaume unaombwa hela mda wote hutumi ndo nini.... alafu nataka laki mbili naomba nitumie

hahahaha hapo baada ya kukuona ndo kashapata sababu hatumi tena lol
 
mrsleo kwa mwelekeo wa post yako nahisi upo kwenye ndoa. Je kabla hujaingia kwenye ndoa, hukugharamiwa na aliyekuwa mchumba hata siku moja?

Aisee me hela ya mme wangu naifaidi sasahv lakn enzi za kudate niliishia kupelekwa outing na kununuliwa vizawad basi, lakn pia haikuwa inanisumbua manake me si muombaji hela kwa mwanaume cjawah, sijazoea na siwez kwanza na mpaka niombe ujue nimebanwa hasa na sitakwambia naomba ntakwambia nikopeshe, alikuaga ananishangaa
 
Hahahaaa... siku izi wasichana wana kila mbinu za kudanganya ili wapate pesa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom