Mgoyangi
Senior Member
- Feb 6, 2008
- 184
- 9
Katika hii nchi, ukistaajabu ya Vijisenti utaona ya majisenti.
Tulikuwa tukisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza na Basi la Mohamed Trans. Abiria wote walikatiwa Tiketi kule wanakoishia na basi likaondoka Tabora Saa 9.14 Mchana badala ya saa 9 Mchana iliyokuwa Imetangazwa.
Kufika Nzega mtu anayeitwa BM aliamuru gari liende kituo cha Mafuta na hapa abiria wote wanaonedelea safari wakateremshwa na kubwagwa kwenye kituo hicho bila huduma wakiambiwa wasubiri gari linalotoka Dar na wataingia humo na kuendelea na safari.
Abiria walikerwa na hali ila na kupiga simu kwa RPC Tabora ambaye aliagiza OCD naye akaagiza OCS wa Nzega mjini ambaye alifika kwa abiria wale na kuwaletea pole kutoka kwa RPC. Akamkaripia huyo anayeitwa BM, ambaye kimsingi katika hali ya dhihaka alijifanya kumng'akia Kondokta huku akishika kidevu, ilikuwa dharau kwa OCS ambaye nina hakika kuna kitu ambacho kilimfanya alobwanike, ni hiki huenda ni rushwa, yupo kwenye pay roll.
Akaagiza kwa nini hawa mmewatupa hapa, ni bora muwapeleke ofisini kwenu, Bwana Mkubwa BM alilipuuza hili wala hakujali akaendelea kushika kidevu, alikuwa nia wale waarabu wa haki ya Muungu. Maana Tabora kuwa mwarabu inaelekea kuwa sifa, na utakuta mtu akiapia, haki ya Mungu Mi Mwarabu.
Baada ya saa moja likaja basi hilo la kutoka Dar likiwa halina nafasi na abiria wote kama zaidi 15 wakalazimika kusimama, walihadaiwa kuwa ingieni ndani kuna seat, wakaingia na hapakuwa na seat, na wakati abiria wanataka kumuona OCS watoe malalamiko OCS huyoo alianza kuchanja mbuga akiongozana na BM na gari likaondoshwa katika mkakati wa kuwanyika abiria nafasi zaidi ya kulalamika.
Mle ndani kukawa na zogo kidogo, mtumishi mmoja wa basi lile akasema hapa kinachafanyika hata mwenye basi anajua, na njia itakuwa safi hadi tunafika Shinyanga. Kufika Tinde kwenye mzani kama saa mbili usiku hivi, basi lilikaa mbali kidogo na vijana wakaenda kusafisuha njia. Baadaye basi likapita bila kupima.
Hapa cha kushangaza ni kuwa Polisi badala ya kusaidia abiria nao wakafanya wanafanya usanii, wa funika kombe mwanaharamu apite, na hapa hakuna kingine ni zaidi ya rushwa rushwa. Kuna siku niliwahi kumuona mtumishi mmoja wa Kampuni ya mabasi akiagiza kumuwekea RPC mmoja shilingi laki tatu kwenye akaunti yake. Sijui kaka IGP Mwema anayajua haya na sijui kama anajua kuwa askari wake wamenunuliwa wamewekwa mfukoni na wamiliki wa mabasi.
Ni shida kweli kweli, lakini hawa ndiyo wafadhili wa shughuli za kile chama chetu................