Ngawira za waarabu kwa Polisi shida kuu kwa abiria

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Katika hii nchi, ukistaajabu ya Vijisenti utaona ya majisenti.
Tulikuwa tukisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza na Basi la Mohamed Trans. Abiria wote walikatiwa Tiketi kule wanakoishia na basi likaondoka Tabora Saa 9.14 Mchana badala ya saa 9 Mchana iliyokuwa Imetangazwa.

Kufika Nzega mtu anayeitwa BM aliamuru gari liende kituo cha Mafuta na hapa abiria wote wanaonedelea safari wakateremshwa na kubwagwa kwenye kituo hicho bila huduma wakiambiwa wasubiri gari linalotoka Dar na wataingia humo na kuendelea na safari.

Abiria walikerwa na hali ila na kupiga simu kwa RPC Tabora ambaye aliagiza OCD naye akaagiza OCS wa Nzega mjini ambaye alifika kwa abiria wale na kuwaletea pole kutoka kwa RPC. Akamkaripia huyo anayeitwa BM, ambaye kimsingi katika hali ya dhihaka alijifanya kumng'akia Kondokta huku akishika kidevu, ilikuwa dharau kwa OCS ambaye nina hakika kuna kitu ambacho kilimfanya alobwanike, ni hiki huenda ni rushwa, yupo kwenye pay roll.

Akaagiza kwa nini hawa mmewatupa hapa, ni bora muwapeleke ofisini kwenu, Bwana Mkubwa BM alilipuuza hili wala hakujali akaendelea kushika kidevu, alikuwa nia wale waarabu wa haki ya Muungu. Maana Tabora kuwa mwarabu inaelekea kuwa sifa, na utakuta mtu akiapia, haki ya Mungu Mi Mwarabu.

Baada ya saa moja likaja basi hilo la kutoka Dar likiwa halina nafasi na abiria wote kama zaidi 15 wakalazimika kusimama, walihadaiwa kuwa ingieni ndani kuna seat, wakaingia na hapakuwa na seat, na wakati abiria wanataka kumuona OCS watoe malalamiko OCS huyoo alianza kuchanja mbuga akiongozana na BM na gari likaondoshwa katika mkakati wa kuwanyika abiria nafasi zaidi ya kulalamika.

Mle ndani kukawa na zogo kidogo, mtumishi mmoja wa basi lile akasema hapa kinachafanyika hata mwenye basi anajua, na njia itakuwa safi hadi tunafika Shinyanga. Kufika Tinde kwenye mzani kama saa mbili usiku hivi, basi lilikaa mbali kidogo na vijana wakaenda kusafisuha njia. Baadaye basi likapita bila kupima.

Hapa cha kushangaza ni kuwa Polisi badala ya kusaidia abiria nao wakafanya wanafanya usanii, wa funika kombe mwanaharamu apite, na hapa hakuna kingine ni zaidi ya rushwa rushwa. Kuna siku niliwahi kumuona mtumishi mmoja wa Kampuni ya mabasi akiagiza kumuwekea RPC mmoja shilingi laki tatu kwenye akaunti yake. Sijui kaka IGP Mwema anayajua haya na sijui kama anajua kuwa askari wake wamenunuliwa wamewekwa mfukoni na wamiliki wa mabasi.

Ni shida kweli kweli, lakini hawa ndiyo wafadhili wa shughuli za kile chama chetu................
 
Hapa mkuu hata huyu IGP anajua kwani naye kuna kawio lake anajua kila kitu kwani hawajui malalamiko ya wananchi kila siku ni hayo hayo.
Nyie hapo mlikosea mngechukua sheria mkononi kumshushia kipigo huyo BM pamoja na konda wake.Angalia barabara ya MBY- IR kule madereva ni full heshima akileta za kuleta kiminyo alafu anashushwa POLICE au kwa trafic watu wanasonga mbele.
Huko huwezi ukaona upuuzi kama huu.Mteja mfalme bwana umelipia nauli alafu unasimama toka Nzega mpaka Mwanza dah!
Lakini Mohamed ana ofisi yake hapo Shinyanga mngemwamulu dereva mwende mkaonana nae.
 
Hiyo sio rushwa ndugu bali huitwa chauchau,hata kule ulaya inakuwa wao hawatoi hiyo chau chau laikini upo mtindo ukifika kituo fulani unashuka na kupanda kipando kingine ,na hiyo chau chau sio wametoa kwa ajili ya hao wenye basi bali kwa ajili ya abiria ambao wamesimama kama ungelitaka sheria basi hao abiria nao wangeliteremshwa.Tayari abiria waliosimama walikuwa na wasiwasi wa kuteremshwa ,lakini konda na dereva wake wakazungumza kiuwanaume na kumalizana na wanausalama bila ya usumbufu wa abiria.sasa hao abiria kama wangelikuwa hawaridhiki si wangelishuka tu,lakini bila ya shaka walikuwa na haraka na kwa hali yeyote hata juu ya mizigo wangelikaa,wao haja yao wafike wanakokwenda.
nafikiri kuna kamtindo cha kufanya mabasi yawe yanapokezana abiria kutoka kituo fulani hadi kituo kingine ila abiria inaonyesha hawajakielewa ,wanahitaji elimu tu maana ni mambo yanafanyika huko ulimwenguni.
 
Siamaini Mohamed trans!wameanza kufanya hivi!walikuwa wakiaminika kwa level seat!sasa nao wamakuwa hivi!
hawa waarabu wa mwamashele wao ndo wao!money talks bwana!sisi kina kayumba tutakoma!
 
Fedha fedheha hao polisi kwenye mikwanja wanakuwa laini kama boflo na hayo maharabu yameshajua hilo....Kweli wakati mwingine watu hawatakiwi kuwa wapole sana inabidi tu kurahisisha mambo kwa kuwapa kipondo...mbona polisi wengine wako tayari hata kutoa roho za watu ili wakamate mikwanja kwani HAMJUI???
 
kw kw kw kw Kijana unachekesha mno yaani haujajua tofauti ya watu ni fedha! pole,
hapa mtu mwenye mshiko ndio mwenye sound bwana we vipi? acha warabu wapete nyinyi si hamjui kutumia malizenu acha watufundishe tutulie tuli kama tunanyolewa,na wewe tia maji ukiona mwenzako ananyolewa itakukuta au itakukuta mara ya pili na 3,4,5,6,7,8,9 ...................10000 :)
 
kw kw kw kw Kijana unachekesha mno yaani haujajua tofauti ya watu ni fedha! pole,
hapa mtu mwenye mshiko ndio mwenye sound bwana we vipi? acha warabu wapete nyinyi si hamjui kutumia malizenu acha watufundishe tutulie tuli kama tunanyolewa,na wewe tia maji ukiona mwenzako ananyolewa itakukuta au itakukuta mara ya pili na 3,4,5,6,7,8,9 ...................10000 :)
Bado nipo na msimamo wa kuwa hawa hawakutoa rushwa hata kidogo ni ileile chauchau ili kuhakikisha haachwi abiria ,maana kama ni rushwa sababu ya kutoa rushwa sijaiona ?
Naona juzi kulikuwepo na habari ya mjeshi mmoja na abiria wengine kushushwa kwenye basi na debe kuachiwa kuendelea na safari,kimantiki utaona mwenye kosa si dereva konda na debe lao bali ni abiria ambae amekosa kiti na kwa hiari yake ameomba achukuliwe hivyo hivyo liwalo na liwe atasimama mpaka afike anakokwenda na mwana usalama yule aliwashusha wenye makosa ambao ni wale waliokosa kiti, yaani kama Basi likisimamishwa na wana usalama kwa upekuzi yeye yupo tayari kushushwa.
Nahisi ili kulekebisha ni bora ashitakiwe abiria aliesimama au aliekosa kiti ,yaani hapo patakuwa patamu sana ,konda atamuambia abiria kwamba kiti hakuna je upo tayari kwa safari ambayo gharama yake itaongezeka ikiwa tutapambana na wana usalama barabarani ,mteja unasemaje ? Na kwa mtindo huo mabasi yatakuwa salama kabisa na hakutakuwepo na malalamiko kati ya wanausalama na wenye mabasi kwani wenye mabasi kazi yao ni kufanya biashala ya kusafirisha abiria popote walipo na kuwafikisha popote waendapo alimradi ruti inalingana.
 
Back
Top Bottom