Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Namkubali sana Neymar Jr kwenye kuchezea mpira, sijapata kushuhudia mchezaji mpira anayejua kuchezea mpira atakavyo kama huyu kijana. Kuna watu wanasema Ronaldinho alikuwa fundi wa mpira, ila kwangu huyu kijana alikuwa hatari zaidi yake.
Tukirudi kwenye mada, Neymar Jr alikuwa na upigaji penati ambao unachukuliwa kama wa udanganyifu ambapo alikuwa akitishia kama anapiga, kipa akienda upande fulani basi Neymar humalizia kwa kupiga upande mwingine tofauti na kipa aliporukia.
FIFA iliona siyo sawa hivyo ikaamua kubadilisha sheria ya upigaji wa penati ambayo inatumika mpaka sasa.