News Alert: Yono apewa siku 10 aombe radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

News Alert: Yono apewa siku 10 aombe radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 30, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yule Mbunge aliyesema Pumba Bungeni ambaye alitaka watu walioambukizwa virusi wawekwe alama amepewa siku kumi akutane na waathirika na pia awaombe radhi. Yeye mwenyewe hata hivyo analaumu vyombo vya habari kuwa hakusema anachodaiwa kusema ingawa alionekana akisema alichosema kwenye Luninga akiwa Bungeni. Hadi hivi sasa sijui kama atakubali kuomba radhi au la..
   
 2. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hivi hakuomba radhi? Yaani kauchuna mpaka ashurutishwe kuomba radhi? Alitakiwa kuomba radhi haraka sana mara baada ya kutoa kauli yake ya kipumbavu! Vilevile anapaswa kuwajibishwa na bunge, au kuwajibishwa na bunge ni pale unapogusa mikataba ya madini "a la Buzwagi" tu?
   
 3. k

  kingwendu Member

  #3
  Nov 30, 2007
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni mpambano wa kifikra.....

  Mkuu mwanakijiji naafiki yale maneno yako, huu ni mpambano wa kifikra ,na kwa hili ni baina ya fikra zenye nguvu na fikra dhaifu (goigoi). Kwa hakika fikra zenye nguvu zitashinda!!!

  Lazima tuwakatilie watawala wetu pale wanapokwenda nje ya mstari. Kama nilivyokazia ktk nukta zilizopita huyu Mh. aombe radhi ama sivyo awajibike/awajibishwe na wapiga kura wake muda utakapotimu nna uhakika wanajimbo wake hawakumtuma akaseme hayo aliyoyasema, the words said were totally our of order & beggars belief.....,'Come out and appologise sincerely' na kama watz tulivyo wastaarabu tutakusamehe kwa maneno yako yaliyopotoka. Omba msamaha yakhe.''Kiburi si uungwana'

  Salaam all.
   
 4. K

  Kasana JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 413
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  aombe radhi kwa lipi? kwa kuongea anachokifikiria kuwa ni sawa?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hapana, kwa unyanyapaa! lengo lake ni kuwanyanyapaa waathirika. Ni haki ya mtu kuwa na mawazo yoyote yale lakini unapoyatoa mawazo yale hadharani jamii inayohaki ya kuyakosoa, kuyaunga mkono au kuyapinga moja kwa moja. Wazo la kutia watu alama kwa vile ni wagonjwa ni wazo la hatari. Kwanini iwe kwa wagonjwa wa Ukimwi tu? Kwanini tusiwaweke wagonjwa wa STDs nyingine pia alama?

  Tukimaliza hapo kwanini tusiamue kuwaweka alama nyusoni watu wote ambao wamekutwa na uhalifu wa aina fulani? Tukimaliza hapo kwanini tusianze kuangalia kuwa makundi fulani ya watu yanawekwa alama ili tuwajue?
   
 6. A

  Atanaye Senior Member

  #6
  Dec 1, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  With all due respect

  KASANA!

  Una maana unyanyapaa ni sawa?

  Si ajabu wewe umejaa vidudu vya malaria-kama watanzania wengi tu-magonjwa ya tropic, na kwa vile ulishasema humu nchi zingine zinaogopa kupata madudu haya, basi watanzania wenye vidudu hivyo vya malaria wawekewe alama? Is this the future you are advocating for? Creation of Unyanyapaa?

  Unajua lazima uwe na mawazo finyu kufikiria huo ndio mwelekeo mzuri tu,mbali kutamka! Mfano; Mwanao wa kuzaa akizaliwa mbumbumbu utampeleka shule na bango linalosema mie mbumbumbu?

  Nafikiri wewe na huyo Mbunge muwekewe alama kama wenye mawazo finyu tuone kama utakubaliana nayo!

  As i said before huyo ni MDUDU GANI? -maana yake hatambuliki hata kwenye jamii ya MADUDU.
  Na akimaliza kuomba radhi,huyu MDUDU GANI? ashinikizwe kutoka bungeni!
   
 7. mashoo

  mashoo Member

  #7
  Dec 1, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  La muhimu kabisa itakuwa ni kuwaweka label wanaotembea nje ya ndoa zao, tuone nani atabaki! Binadamu ni rahisi kuwanyooshea wenzao vidole utafikiri wao ni wakamilifu. Cha kushangaza kabisa hao wanaotoa wazo kama hilo hata hawajapima au mwenendo wao pia ni wa mashaka kama sio kutisha. Tukumbuke "kutoa boriti katika macho yetu kabla hatujatoa kibanzi kwenye macho ya wenzetu"
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2007
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  ndugu mwandishi nimesikitika sana kuona mheshimiwa kama huyu labda tatizo lake kijana ni kushika pesa umri mdogo,.ndio maana analeta dharau hata kwa wenye ukimwi,,yeye mwenyewe namshauri akapime maana yule bibi pale TRA aliekuwa anamla uroda hali yake ni mvutano,,
  PILI:Bwana yono sioni ajabu kuwaambia wenye ukimwi wawekewe alama,,kama wewe una uwezo wa kuondoa ndugu zako,,majuzi tu kamlaza mwanae huko kilimanjaro sababu ya uchawi,,mwezi aujapita kamlaza mdogo wake,,we ndugu yangu kibaya zaidi waakati unapokea msiba wa mwanao pale airport unachungulia then unacheka ,,kaka yetu hata kama UTAJIRI bado,,jitahdi ulindee ndugu zko hata ukija kufa na UKIMWI na wewe NDUGU au watoto waweze kukulindia mali zako,,ukome na semi zako bunge si la kujipatia sifa ndugu yangu,,na ukitamka pale usifikkirivideo inaishia YONO ACT MART,watu wananukuu ndio maana pale bunge kuna vitu vya kurekodi kushindana na wanaosema pumba kama wewe,,tunaomba jitahdi upate utajiri wa baraka achana na xxxxxxxx
  ahsanten
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2007
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  muulize ndugu yako T.LYIMO ameishia wapi na vile vibanda vya maziwa hayo mambo machafu achana nayo,,mimi nafnya jirani na kampuni yao nimesikitishwa sana kuona usemi wako,,,,waulize wafnyabiashara wa mabasi ya mbeya/iringa wako wapi????right off.
  lipi bora uumwe ukimwi na kuishi na amani au uwe na hela na kulalia mito badaala ya magodoro..mkeo anajua masharti uliopewa katika utajiri wako,,,,,njua masharti hayakubali kumjulisha mkeochochote ila jitahdi kwa hili usije baki history ndugu yangu
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2007
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hana haja ya kuomba radhi,tena mimi naunga mkono kabisa ,hilo ni wazo lake binafsi na sababu zipo wazi wala huna haja ya kufikiria kwa nini,hata wanyama aina ya ng'ombe mbuzi nao huwekwa alama ili kuwajua na kuweza kuwabagua kirahisi wanapoingia katika mkanganyiko.
  Na hawa waathirika ikiwa watapatiwa alama flani basi watafahamika na mwisho watazoeleka na wao kuzoea hali hiyo,mboni kuna wengine wanajijulisha na wana andaa makongamano makubwa makubwa na wengine huvaa na beji kabisa ili kuwajulisha na kuwatahadharisha wengine,sasa hawa ikiwa watakubali kwa ridhaa yao wataipatia jina Tanzania katika kilingo cha Kimataifa na naamini kabisa nchi nyengine zinaweza kuiga mfano wa wagonjwa wa kwetu au mpaka waseme wazungu kama mikataba ni mibaya.
   
 11. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2007
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aanze kuweka wenzake humo bungeni maana wamo waathirika na yeye sidhani kama hana!
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,217
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Nimesoma maelezo ya Yono Kevella, anasema alinukuliwa vibaya! Hivi huu upotofu wa baadhi ya viongozi wetu, wanaoropoka bila kufikiri na baadaye kukanusha na kusema vyombo vya habari viliwanukuu vibaya utaisha lini?
  Yaani nashindwa kuwaelewa kabisa! Mnisaidie
   
 13. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2007
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mwiba sijui kama kweli unaamini unachosema! Hivi unajua unyanyapaa ni kitu gani? Naomba urudi katika historia usome unyanyapaa wa kikabila huko Ujerumani chini ya Hitler ilivyopelekea holocaust ya wayahudi, waroma, walemavu wa viungo na walemavu ya akili!
  Hakuna nchi itakayoiga mfano wetu tutaonekana ni washamba! Haiwezekani! Kwani tuwatenge wagonjwa! Hata kama baadhi yao wanatenda maovu, tukumbuke ya kuwa Mungu huhakikisha mvua inatunyeshea wote, waovu na wema! We have no right to judge any1!
  Yono's proposal is disgusting, unacceptable in the 21st century and he should apologize immediately!
   
 14. M

  Mtu JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Inawezekana ana mtindio wa Ubongo....mimi nashauri kabla ya kushurutishwa kuomba radhi apimwe akili
   
 15. C

  Choveki JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ......LOL!!
   
 16. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  mwiba anayo haja ya kuomba radhi kwa unyanyapaa aliyoonyesha kama binadamu. Hivi kweli unaweza toa mfano wa ng;ombe na binadamu???? haiingii akilini, sisi ni binadamu tuna haki ya kuishi huru, na tuna haki ya kupendwa hata tukiumwa.
  Tuwabague ili iweje?
  Kama suala ni kuwatahadharisha wengine mara ngapi tunapigiwa kelele misikitini na kanisani. Tuwe waaminifu kwenye ndoa zetu, kwa wapenzi wetu. Hilo halitoshi? Hivi tumekosa utashi kiasi gani sisi wanadamu?
  Kila mtu mwenye akili timamu anajua Ukimwi unaenezwa kwa njia gani sasa kwa nini asijilinde binafsi?
  Mtu akitaka kuutangazia umma kuwa ana ukimwi well and good let him do that but asifisiwe ajitangaze.
  Hivi unafahamu malaria inaua kuliko ukimwi? kwa nini wasisieme basi tuwabadikie wenye malaria maana tukikaa nao au kulala nao na bahati mbaya tukang'atwa na mbu mmoja basi tushaukwaa ugonjwa sugu afrika malaria?
  Embu kwanza kabla ya kuunga mkono hoja zinazohusu undani wa watu tujikague wenyewe. Nani msafi? Nani hafanyi ngono na mtu asiye mkewe/mumewe. nani hafanyi ngono kabla ya ndoa? Na wangapi hupima ukimwi kabla ya kuanza mahusiano?
  tusipende kuona wengine wana matatizo wakati in reality we ourselves ndio vyanzo vya matatizo.

  Yono omba radhi baba.
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Dec 3, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hivi hajaomba tu bado?

  hii sio nzuri ukichemka kuwa mkweli uombe radhi yaishr.

  kwenye maisha kuchemka kumo
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2007
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Bado hamjanishawishi hata nione umuhimu wa kuomba radhi,kwani ilani zinazotolewa na viongozi wetu zimeshajaa kila kona na sisi tunaojisifu kuwa ni binadamu tunawadharau viongozi hao na kuwaona hawana la kusema,halafu Ukimmwi sio homa ya malaria hili ni gonjwa lililo na indicator ya uuwaji halina simile,kubwa ambalo lingenifanya nione umuhimu wa walioathirika na ugonjwa kuwekewa alama ni namna unavyoonea na unavyoenezwa kuna watu wakishajiju kuwa wameukwaa basi hufanya juu chini nao kupata wafuasi au kupata na kupanga njama za kuwaambukiza wengine kwa ufupi wanageuka na kuwa maadui wenye kuambukiza kwa makusudi,lazima na hili mulipime ili kuiona haja ya watu hawa kuekewa alama mbona wagonjwa wa UKOMA wanatengwa tena nakumbuka siku zile nipo shule walipita madakitari na manesi kutupima ukoma nafikiri ilikuwa kampeni ya Tanzania nzima,wakikuchoma choma kila sehemu halafu wanakuuliza kama unahisi lakini ukimwi ni vyengine kabisa huu unaua na kuangamiza jamii nzima,mnafanya mchezo nyinyi na namna gonjwa hili llinavyoteketeza kuna vijiji vimeshaambukizwa kuna familia kuna makundi na yote haya kama wagonjwa wa ukimwi wangeliwekewa alama flani flani basi yasingelitokea zaidi ya apendavyo Bwana Mungu.
   
Loading...