Newcastle United na safari ya kuwa Timu Tajiri zaidi Duniani

Mnyuke Jr

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
4,471
6,371
Newcastle United iliingia katika mfumo wa private company limited by shares mnamo Tar. 6 September 1895, timu hii Ilijiendesha kwa mfumo huu hadi karne 20 ikiwa inatawaliwa kwa umiliki na Mckeag, Westwood na Seymoor family hadi kufikia Mwezi wa 4 1997.

Katika kipindi hicho alitokea tajiri mwingine aitwaye John Hall na akanunua 72.9% ya hisa za timu kwa kiasi cha Euro milioni 3, huku asilimia ya hisa zilizobakia zikauzwa kwa mfanyabiashara wa karibu wa Bwana John Hall aitwaye Freddy Sherpherd na John Hall kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi katika timu hiyo ila ktk mwaka huo huo Bw.Hall alijiuzulu katika nafasi hiyo ya uenyekiti na ikachukuliwa na Bw. Shepherd, huku katika Bodi ya timu hiyo familia ya Bw. Hall ilikuwa inawakilishwa na mtoto wake mkubwa ambaye anaitwa Douglas

Mwaka 1998,kampuni ya habari ya NTL ilinunua hisa 6.3% za klabu ya hiyo kwa kiasi cha Euro milioni 10 na baadae kuwa na mawazo ya kutaka kununua hisa zote za klabu ili kuwa na umiliki wa klabu ya Newcastle kwa asilimia zote ila baadae tume ya ushindani iliingilia kati swala hilo na kuweka vizingiti kwa kampuni za vyombo vya habari kumiliki klabu za mpira na kufanya ndoto zao kufifia

Mwaka 2007,alitokea mfanyabiashara ambaye anajulikana kwa jina la Mike Ashley na kuzinunua 41% za hisa za klabu hiyo ambazo kwa kipindi hicho zilikuwa kwa kiasi kikubwa na Hall family, huku kukiwa na kipengele cha kununua zaidi hisa zilizobakia ili awe na full control katika klabu hiyo ya Newcastle kupitia kwa kampuni yake ya St. James holdings, na kufikia Tar. 29.6.2007 Bw. Mike Ashley alikuwa tayari amenunua 93.19% ya hisa za klabu hiyo na kufikia pia Tar. 11.7.2007 alikuwa anatengeza force kubwa kwa shareholders waliobaki na asilimia hizo chache ili wamuuzie na awe na full control ya timu hiyo

Baada ya kufanikisha zoezi la kununua hizo zote za klabu hiyo Bw. Mike Ashley ilipofika mwaka 2008 alianza mchakato wa kutafuta mnunuzi wa klabu hiyo baada ya timu hiyo kuyumba katika matokeo ya uwanjani na jaribio la kwanza la kuuza timu hiyo lilianza baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Timu Bw. Kevin Keegan mnamo Tar. 14.9.2008 na mashabiki wa Timu hiyo kufanya maandamano kushinikiza mmiliki huyo kuuza timu hiyo kwa kushindwa kuleta matokeo mazuri kwa timu hiyo na Bw. Mike Ashley alijitokeza mbele ya mashabiki hao na kusema "I have listened to you"." You want me out" "and this what am trying to do" Ila Tar 28.12.2008 aliondoa sokoni klabu hiyo kwa kukosa mnunuzi wa timu hiyo.

Mnamo Tar 31.5.2009, iliripotiwa kwamba Bw. Mike Ashley ameingiza tena sokoni klabu hiyo ya Newcastle na hadi kufikia mwezi wa 6 mwaka 2009 mmiliki wa timu hiyo alitangaza klabu hiyo inauzwa kwa bei ya Euro milioni 100.Ila kufikia mwisho wa mwaka huo aliweza kuitoa tena sokoni klabu hiyo kutokana na kukosa tena mnunuzi wa timu hiyo. Na kufikia tena Tar. 16.10.2017 Bw. Mike Ashley alitangaza tena kuiuza klabu hiyo na mnunuzi tayari kapatikana na Anategemea deal kumaliza mwishoni mwa mwezi December.

Kufikia mwezi wa 4 mwaka 2020 vyombo mbalimbali vya habari duniani viliripoti ya kuwa kampuni ya Public investment fund chini ya mwana mfalme Bin Salman, PCP Capital partners na The Ruben Brothers zote za kutoka Saudi Arabia walitangaza wapo katika nyakati za mwisho wakiandaa offer yao kwa ajili ya kuinunua timu ya Newcastle United, bila kutegemea wanaharakati wa haki za kibinadamu nchini Uingereza walijitokeza na kupinga Saidi Arabia kuinunua timu hiyo kwasasa zifuatazo:-

Moja, ikiwa ni Ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu ambao ulikuwa unaendelea katika nchi hiyo ya Saudi Arabia chini Mwana mfalme Bin Salman.

Na pili, ni Urushwaji wa matangazo ya mpira hasa Ligi kuu ya Uingereza bila kuwa kibali hicho kutoka skysports ambao ndio wenye haki hiyo ya kurusha matangazo hayo kupitia kampuni ya BeIN Sports ambayo ina operate kutoka nchini Saidi Arabia na mmiliki wake akiwa ni Rubein sports&Media company.

Hiyo ilipelekea Mwana mfalme wa Saudi Arabia Bin Salman kutangaza kujitoa katika mchakato huo wa kuinunua klabu hiyo ya Newcastle United na ndoto za Bw. Mike Ashley kupata mnunuzi zikawa zinafifia taratibu ila kufikia mwezi September 2020 klabu ya Newcastle ilitoa officail statement yao ambayo ilikuwa ikitoa lawama kwa chama cha soka Uingereza kwa kitendo chao cha kuzuia Saudi Arabia kuinunua timu hiyo na baadae chama cha soka na chenyewe kikapinga vikali malalamiko ya Newcastle dhidi yao

Mazungumzo baina ya chama cha soka nchini Uingereza na timu ya Newcastle kupitia kwa mmiliki wake Bw. Mike Ashley na upande wa Public investment fund chini ya Mwana mfalme Bin Salman na hatimaye, Tar 7.10.2021 The public investment fund, PCP Capital partners na RB sports and media company wametangaza na kuthibitisha rasmi wameweza kumaliza mchakato wa kuweza kuinunua timu ya Newcastle United kwa dau la Euro Milioni 300

Na pia chama cha soka nchini Uingereza kuthibitisha uhalali huo wa kampuni hizo kutoka Saudia chini Mwana mfalme Bin Salman kuwa wamekuwa wamiliki wa Newcastle United

Na sasa ni rasmi Newcastle United ndio imekuwa timu Tajiri na ghali zaidi duniani.

Nitawaletea list ya timu tajiri Zaidi duniani na thamani zao.

I stand to be corrected
Yours Insigne
 
🚨| Can’t wait until Newcastle sign a big player and in their first interview they say “I’ve watched Newcastle ever since I was a child and always wanted to play for them.” 😂😂😂

Let’s Go Newcastle United 😀😀
 
Big players after signing for Newcastle:

I grew up watching Newcastle, they have a huge history. Allan Shearer made me fall in love in with this club, he's a true legend. I hope I can achieve what he did at Newcastle. It's a dream come true. I can't wait to represent this badge
 
Hawa Newcastle wana moto

20211008020404_1.jpg
20211008020244.jpg
Screenshot_20211008-022154.jpg
20211008015718_1.jpg
20211008015718_2.jpg
20211008015718_4.jpg
20211008015718_3.jpg
20211008015718_0.jpg
Screenshot_20211008-022116.jpg
20211008015548.jpg
 
Exactly...huku wananchi wanalia njaa
Nchi ina invest kuwanunua kina mbape
Mkuu si unajua hizo ni nchi za kifalme, wananchi hawawezi kutoka na kupinga chochote na ndio maana wana kashfa ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliowazingua ktk harakati za kuinunua hii timu kipindi cha Nyuma
 
Wana asset za usd 500 bn....kwa nini hawamo kwenye list ya matajiri duniANI?
Hawa waarabu ni kufuru na huyu jamaa Mike Ashley ameula nadhani ataingia kwenye list ya mabilionea....kumbe psg,Mancity hawana hela kivile wamepitwa mbali sana.
Pesa ya umma hiyo mkuu
 
Na united yangu wainunue jamani
Mkuu hawa kampuni ya Public Investment fund, nafikiri mwaka 2015 walihitaji kuinunua timu ya Manchester united na Glazers family wakasema tunaiuza timu kwa Pound Bilion 2,Bin Salman akasema atawapa Pound Bilion 3.5

Ila ndo hivyo Glazers family wakazingua coz faida wanayopata pale ni kubwa mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom