Mwenendo mbovu wa Man. Utd na Newcastle kwenye Klabu bingwa Ulaya kuikosesha EPL nafasi moja ya zaidi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Timu 4 zitaongezeka kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2024/25, ambapo timu 2 kati ya hizo zitatoka kwenye ligi mbili zilizofanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu huu

Ilitarajiwa moja ya nafasi itachukuliwa na Klabu ya Ligi ya England (#EPL) kwani Ligi hiyo imekuwa ikifanya vizuri Ulaya na kumaliza katika nafasi mbili za juu kwa misimu 6 kati ya 7 iliyopita

Msimu huu, Man. Utd na Newcastle zipo nafasi za mwisho kwenye Makundi na huenda zikatoka, hatua inayopelekea EPL kuwa nyuma ya Ligi za Ujerumani, Italia na Uhispania kuwania nafasi hizo

Ubora wa Ligi kwenye michuano ya UEFA hupimwa kwa pointi zinazotolewa kwa timu ya Ligi husika inaposhinda au kupata sare katika hatua ya makundi, kufuzu kwa hatua ya mtoano na kwa kila hatua inayoingia

12.jpg

 
Back
Top Bottom