New revelation, Dowans in huge debt


Ukiona watoto wanachezea bomu huku wakidhani ni mpira ni lazima uhakikishe wanaacha kufanya hivyo mara moja. Zitto katika saga hili tumdiagnose kama ni mpira au bomu, ili tuweze kuhakikisha kuwa wanachochezea ''watoto'' ni kitu salama. Hakuna msumari ulioingia wote, ungekuwepo basi tungesikia confession from Zitto. Je, jukumu la kusema kuwa msumari umeshaingia sio la Zitto mwenyewe?
Hapa ni sawa na mtu mwenye kidonda na malaria concurrently, hupaswu kuchagua kutibia malaria ukaacha kusafisha kidonda - hata kama unakiona kuwa sio major health threat.
Zitto ni mwana JF, anaweza kuja kutoa maelezo yeye mwenyewe. Huna haja ya kumdefend - unless otherwise!
 
Jamni kuhusu ZITTO acheni tu kijana napenda sifa sana na ndizo zinazomponza, nawahakikishia kuwa hajapewa senti hata moja ila aliitwa na wakuu fulani wakamsifu sana kuwa yeye ni mbunge makini mwenye akili sana na anajua kujenga hoja na wakamwambia urais unamngoja 2015. Baada ya kumsifia hivyo ndo akaambiwa asaidie kulainisha mambo ya Dowans, Vile ananpenda misifa akashindwa kuchomoa.

Hivi ZITTO tarehe 21 February 2009 pale bar ya G8 Summit kinondoni ulikuwa unachonga deal gani? plse uwe mkweli....
 

Susuviri, Dar Es Salaam hapa, ni wapi niliitetea Dowans, hebu kandamiza hapa.
 
Susuviri, Dar Es Salaam hapa, ni wapi niliitetea Dowans, hebu kandamiza hapa.

Ni misimamo yako na wengine wenye mawazo kama yako. Shuhudia haya uliyosema huko nyuma.

Yes, kwa upuuzi wa watu kuchanganya siasa na biashara. Dr. Idriss kutaka kununuwa hii mitambo alikuwa sahihi kabisa.

Na alichofanya, ni kama kuwaambia haya. nyinyi si mnajuwa zaidi na lidode!


Kazi kwako, naipenda JF... kazi kweli kweli, upo ?
 
Ni misimamo yako na wengine wenye mawazo kama yako. Shuhudia haya uliyosema huko nyuma.





Kazo kwako... kazi kweli kweli, upo ?

Ama kweli kuna watu na viatu, sijaona hata sehemu moja niliyoitetea Dowans katika hayo! Duhh, hamuelewi maana ya kutetea au vipi?

Msimamo wangu umeuelewa haswa? au nikuombe urudie tena kusoma?

Katika yote niliyoandika kama utakuwa mwangalifu na makini, nimetetea wa Tanzania watakao patwa na adha ya kukosa umeme wakingoja mitambo mipya wakati mitambo ipo Ubungo, haisaidii kitu.

Hakuna nilipotetea Dowans.

Msikurupuke.
 


Documents seen by THISDAY show that during 2007, Dowans was awarded several loans worth a total of $55m from Barclays Bank alone


Hii benki ya Baclays Bank managing director wake ni Rished Bade ambaye anatoka Arusha na wana undugu na Idrisa Rashid managing director wa Tanesco.Huyu Rashid Bade walikuwa wote benki kuu ya Tanzania wakati Idrisa Rashid akiwa gavana wa Benki kuu.Hivyo kama mikopo ilichukuliwa Baclays twaweza unganisha dots.Pia ile mipesa ya EPA na Richmond iliyopitia CRDB kwa managing director Kimei haikuwa bahati mbaya.Kimei alikuwa ni mkurugenzi benki kuu wakati Idrisa Rashid alipokuwa gavana wa benki kuu.Kwa hiyo Idrisa Rashid,Rished Bade na Kimei wanafahamiana sana tu na kwa karibu wakiwa benki kuu na baada ya kutoka benki kuu inaelekea wameendeleza mtandao fulani wa kuliza nchi.

Kiufupi twaweza kusema unapoongelea ufisadi na connection na benki kuu Rished bade,Idrisa na Kimei wako connected Kiuhalifu unaohusu ndani na nje ya benki kuu kupitia EPA,Richmond,Dowans.Maana mapesa yaliibwa benki kuu yakaenda CRDB mengine yakaibwa kupitia Richmond yakaenda CRDB na mengine yakakopwa Baclays sijui yalienda wapi kama mmiliki anakana kuwa hakukopa labda yalifanyiwa money laundering kupitia benki fulani yakayeyukia kule kunakofanana na wanakoficha pesa akina chenge na wengineo.
 

Subiri kidogo tu - utajua "ghost faces behind Richmond/Dowans" Halafu utajua kwa nini mitambo ya Dowans ni lazima inunuliwe - labda wazalendo wa kweli waseme NO, no, nooooo !! Utakosaje kutetea Richmond/Dowans kama unatetea nguvu zinazosukuma Richmond/Dowans !!
Stand now and be counted - uko upande gani ?

Kwa ukumbusho tu - ripoti ya Mwakyembe ilificha nini kwa kulinda heshima ya serikali - Lowasa, Karamagi au Msabaha ? Mbona hawa walitoswa ? Dar es Salaam, jaribu kupima mawazo yako - Ama hujui kinachoendelea au unajua vizuri sasa, sasa kipi kinakusukuma ?

Haya ndio yalisemwa na Mwakyembe baada ya hao jamaa kujiuzulu :-


Ni watu gani hawa anawaongelea Mwakyembe ?
 

Huyu Rished Bade sidhani kama anauraia wa TZ maana wazazi wake ni wasomali. Kama hajawahi kuomba alipofikisha miaka 18, he might be working illegaly in TZ.
 
Dar es salaam,
Duh mkuu wangu ama kweli wewe mtoto wa mjini.. mitambo ipo Ubungo sio..

wanabodi,
hawa Tanesco wanacheza shere tu!..hata wakishikilia mitambo haiwezi kuwasaidia kitu kwani mitambo hiyo imewekwa kama dhamana ya mkopo waliochukua Dowans.. period.
Hata ktk nyumba za kupangisha benki ikija chukua nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipia Mortgage mpangaji hawezi kukatalia nyumba au kukataa kuondoka kwa madai kwamba anamdai mwenye nyumba hivyo anashike nyumba...Utatolewa mkuku tena vibaya sana..Tanesco ni mpangaji tu.
Hii yote zuga kinachofuatia ni ununuzi wa mitambo hiyo kulipa deni la Dowans na sio kabisa tunanunua mitambo hiyo kwa sababu ya uhaba..
 

Arusha Connection still....ongoing.......I love this!!
 



Hakyanani, tungetapeliwa vibaya na mwisho wa siku mitambo ambayo tungenuu ka mabilioni kutoka Dowans ingeng'olewa na hayo Mabenki na giza lingerudi palepale au tungelipa na deni la Dowans Tshs. 90 bn bei ya kukunua kutoka Dowans + Tshs 90 bn deni la mabenki= 1080 bn!.

ZITO JIEPUSHE KUINGILIA SIASA ZA CCM MAANA WENGIWAO NI MAFISADI, WATAKUZAMISHA! TUNAJUA UNA UCHUNGU NA NCHI YETU LAKINI UGOMVI WAO WAACHIE WENYEWE, NDUGU WAKIGOMBANA SHIKA JEMBE UKALIME, 2010 WATAPATANA UPYA THEN UTABAKI NA AIBU!
 
Two wrongs don't make a right! Haya ndio matokea ya kufutwa kwa maadili ya Uongozi yaliowekwa chini ya Azimio la Arusha. We need these rules back and in full swing! Yes Mwakyembe did well to lead efforts to uncover the Richmond with his team and we all salute that, but how on earth can he justify his position as a Vice Chairperson in the committee and Head of Probe team dealing with his very own area of interest, and making and influencing laws that are directly relating to his area of such a close interest? I don't care what they can say with existing rules - whether Mwakyembe did put this kwenye daftari of interest bungeni as law requires, this simply proves before our very eyes that kama Wananchi tumelala usingizi mzito, mzito mno kwani this should have never been allowed to exist in a first place, period! Huwezi wewe kuwa a judge, jury, victim, advocate kila kitu wewe mmoja! No way.

This does not mean Lowassa was right or is right! Not at all, wote ni wachafu wa maadili and don't tell me katika watu 40milioni wa Tanzania hakuna watu wasafi!!! This is very frustrating and we seriously need to change these debates into actions now. Tunaibiwa day light! We get presidents opening companies while in State House - then we say KATIBA haituruhusu kuuliza na kupeleka mahakamani, we get people getting appointments kiukoo wakati katiba iko wazi hii sio nchi ya Kifalme wala Kiukoo, we get Richmonds and Dowans, We get KIGODA and we still debating endlessly and spending countless hours online and on print and nothing is changing as fast as it should be!

We all need to get organized kama Watanzania, sio kama watu wa chama chochote, kama Watanzania na kudai nchi ikombolewe kutoka kwa huu ujangili uliozidi kikomo. I don't have to be modest in my statements kwani hawa watu they have not modesty all they have is power and will to get rid of anyone coming to them in the open but we need to plant this seed of true revolutionary minds as much as possible so that even if you or I are not here, people can take the fight to the people for peoples good. Tuache kutukanana online endlessly.

Mwakyembe amechemsha BIG time. Lowasa BIG time, Our President is not using his political capital to clean the mess. You tell me who is there to fight for your corner??? Niambie kama sio wewe peke yako na mie peke yangu?? Now Slaa anapendekeza noble idea, wapunguziwe posho ili miradi majimboni ifanyiwe kazi, wait and see kama atapata any support! Haiwezekani kmwe kwani pale asilimia kubwa sana ni Ujangili wa Nchi ndio unaendelea! Huwezi nunua mashangingi yote yale wakati watu wenyewe wenye pesa wana shida left right centre! You tell me, leo hii mkiwa na kikundi chenu, mchange kuanzisha association ili mtoe huduma ya shule - hamna waalimu lakini mnaweza fundisha wenyewe kwa kuanza. Kama wajumbe mtaamua kulipana mishahara minono wakati mnajua pesa hakuna?? No way, mtajitolea ikibidi kama kweli what you want ni association yenu ifanye kazi. Lakini mkiwa na nia za kichonyo, wapo watakaosema lazima tulipwe na watajichotea ndio hawa wabunge wetu. Their association is how they manage affairs za nchi kwa jina la Uzalendo halafu wafanyayo hakuna Uzalendo wowote ule, na ndio hao hao wanasema wanaoishi nje ya nchi si Wazalendo?? Akili hiyo??
 
Last edited:

Daahh....Mkuu Taasisi tumekusikia........na tunakuelewa.......hili jambo tumeshalijadili kwa kirefu...inaonekana kila mtu ana uelewa wake kuhus conflict of interest........
 
Nawashuru sana watu hawa, waliosimama kidete, tusinunue ile mitambo ya Dowans, Mr. Samwel Sitta, Dr Halison Mwakyembe hao ndio walijitoa mhanga kwenye radio na TV kupinga hili swala, tunajua mambo mengi yalitokea hapo. Sasa naamini hata zile ajari za akina Mwakyembe kule Iringa zilikuwa za kupanga. Na waheshimiwa kama Kilasi na Sherukindo wamepotezwa na mafisadi
 
Kuna mtu wa TRA hapa atuwekee hadharani kiasi cha kodi ambacho Richmond/Dowans wanadaiwa? plus interest charges and penalties for late payment. Kama hayupo basi hakuna ubaya tukiitafuta hii namba kutoka kule TRA sidhani kama na yenyewe ni siri kubwa.
 
Habari za kuaminika ambazo sikuweza kuzihakiki zaidi kutoka ndani ya TRA zinadai kuwa dowans inadaiwa kodi zaidi ya billion 25 ambazo zilikadiliwa na kukubaliwa na kampuni hiyo!, yeyote mwenye habari zaidi tumwagie humu jamvini
 
Habari za kuaminika ambazo sikuweza kuzihakiki zaidi kutoka ndani ya TRA zinadai kuwa dowans inadaiwa kodi zaidi ya billion 25 ambazo zilikadiliwa na kukubaliwa na kampuni hiyo!, yeyote mwenye habari zaidi tumwagie humu jamvini

Hio wala sio siri mkuu, kuna wakati TRA walitia kufuri kwenye mitambo ya DOWANS lakini kuna mnene aliingilia kati...
 
Yaani kuna kiumbe mwenye uwezo wa kuzuia mapato/kodi ya nchi kwa kiasi cha sh.25 bilioni !!
Haki ya nani, huyo hukumu yake ni kunyongwa tuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…