ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Hivi msumari ukiugongelea kwenye ubao ukaingia wote, unazidi kuugongelea ili kiwe nini? unataka kuvunja ubao? HIli suala ni la Dowans, kwamba Zitto alipotea/alifanya makosa ya kisiasa au hata mkakati mbona halina ubishi. Lakini kujaribu kuendelea kusema "zitto, hakuna kitu" au "Zitto hivi au vile" ni kukwepa mjadala.
Hamuonekani kukerwa na Dowans, Tanesco, wizara ambavyo ndio wahusika wakuu wa suala hili. Mnasemaje kuhusu Dowans, Ngeleja, Dr. Idris, Mmiliki wa Dowans?
Issue ni chembe ndogo tu katika mjadala huu and if you ask me an irrelevant one!
Ukiona watoto wanachezea bomu huku wakidhani ni mpira ni lazima uhakikishe wanaacha kufanya hivyo mara moja. Zitto katika saga hili tumdiagnose kama ni mpira au bomu, ili tuweze kuhakikisha kuwa wanachochezea ''watoto'' ni kitu salama. Hakuna msumari ulioingia wote, ungekuwepo basi tungesikia confession from Zitto. Je, jukumu la kusema kuwa msumari umeshaingia sio la Zitto mwenyewe?
Hapa ni sawa na mtu mwenye kidonda na malaria concurrently, hupaswu kuchagua kutibia malaria ukaacha kusafisha kidonda - hata kama unakiona kuwa sio major health threat.
Zitto ni mwana JF, anaweza kuja kutoa maelezo yeye mwenyewe. Huna haja ya kumdefend - unless otherwise!