Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Is a real jesuit, as reported in the news
Kulikuwa na mada nyingi vyombo vya habari kwamba ni kipindi kizuri kwa Kanisa Katoliki kupata Papa kutoka bara la Amerika Kusini au Afrika kwa vile idadi kubwa ya waumini siku hizi ni kutoka mabara hayo. Naona Mungu ameelekeza mkono wake huko na kumchomoa Cardinal Jorge Mario Bergoglio Kuwa Pope. Hawa wazungu walitaka kuharibu kanisa na ni wepesi mno kukata tamaa mambo yanapokuwa magumu. Anahitaji mtu mstahimilivu, mvumilivu, mwenye msimamo na asiyeyumba, maana pope ni uhai wa kanisa.
Shaka lilikuwa wajumbe katika mkutano huo wa kumchagua papa ambao ni makardinali wengi ni wa kutoka Ulaya na USA, lakini tujuavyo hii ni kazi na nguvu ya Mungu, ni roho wa Bwana anayeongoza na kumweka mtumishi anayeona atasimamia mahali pake patakatifu.