Nimeitikia wito.
Unajua kwamba "Mungu" ni jina tu kwa kumaanisha yule apasae kuabudiwa. Lakini tamko hili limekaa kilugha sana. Kwa waswahili yule apasae kuabudiwa kwa haki,waswahili waliamua kumuita "Mwenyezi Mungu". Tamko kwa waswahili halina wingi bali lina umoja daima. Mungu ni tamko ambalo si stahiki sana kwa kumkusudia Mwenye kupasa kuabudiwa,na matamko yote mawili hayatoshelezi kumuelezea,ila kwa waswahili wanamkusudia yule mwenye kupasa kuabudiwa.
Tamko "Mungu" lina wingi na mimi huwa aipendi kulitumia sababu halikidhi haja.
Ukweli uko hivi "Tunaweza kumuelezea Mola tofauti lakini tukawa tunamkusudia yule yule,lakini hii haimaanishi tuko sawa"
Uliyemnukuu
Truth Teller hoja yake ni dhaifu sana na haipaswi kutolewa mfano au kuegemea kwayo kwani amezuzuka na majina na kuipuuza sifa. Namuuliza uliyemnukuu "Wakristo ambao ni Waswahili huwa wanamuwasilisha kwa jina gani yule apasae kuabudiwa ?"
Mgawanyiko wa Waislamu na Wakristo hauletwi kwa jina bali unaletwa kwa mapokeo yaani mafundisho.
Nakuja kuendelea hapa nilipoishia.