Mungu aliye hai yupi? Yeye alitokea wapi, kwani kuna wengine waliokufa?
Ni dini gani inakupeleka kwa huyu Mungu aliye hai wakati yeye mwenyewe hakuna dini aliyoshusha kutoka ili tuiabudu.
Ni hukumu gani atatupa sisi tuliokengeuka na kukataa kanisa na misikiti. Wanasema tutachomwa moto milele, kuna moto gani unaweza kuchoma roho?
Unasema hii dini mpya asili yake ni shetani inatupeleka mbali na Mungu, kwani hujui kuwa siku nyingi tuko mbali na mungu shetani ndiye mtawala wa hii dunia? Jehova na kina Alah washaiacha siku nyingi hii dunia wako huko kwenye solar system ingine na shughuli zao.
Kwanini huyu Mungu aliyetuumba atupe akili ndogo kiasi kwamba tushindwe kujua chanzo chake yeye au mwanzo wake maana kwa akili alizotupa tunajua hakuna kiti kisicho na mwanzo wala mwisho, je mwisho wake yeye ukifika sisi viumbe alivyotuumba tutakuwaje ?