Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,351
- 10,232
Wiki hii nilipata nafasi ya kuangalia movie pamoja na series mpya kutoka NETFLIX ORIGINALS. Hizi zote wameziandaa wenyewe;
EXTRACTION (Movie)
Hii imejipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na kuwa full packed na fights za kutosha, kwa wapenzi wa action movie hii lazima uikubali. Ila walipofeli na wanapozidi kufeli NETFLIX ni jinsi wanavyomaliza movie zao, huwa wanaacha maswali mengi kwa watazamaji; hii movie imezua maswali mengi sana, Je, Tyler alifariki baada ya kupigwa risasi ya shingo na kujitupa ndani ya maji? Je, yule anayeonekana mwisho kwa mbali wakati Ovi anaogelea ndio Tyler mwenyewe na aliwezaje kupona katika hali ile?
Kiukweli maswali ni mengi kuliko majibu, wengu tumebaki kujijibu wenyewe maana muda mwingi kazi za sanaa zinakuja na mafumbo na unapaswa kuyavumbua mwenyewe.
EXTRACURRICULAR (SERIES)
Hii ni kutoka Korea chini ya NETFLIX, story nzuri sana, waigizaji wamejitahidi na wengi wao ni wageni kabisa katika filamu huko Korea. Hii inahusu dogo anayepambana kupata pesa za shule pamoja na matumizi mengine, huku ndoto yake ni kusoma hadi chuo, ku-graduate na kufanya kazi ila dili anazopiga sasa ni haramu (Sex Trafficking) anajiita Uncle huku akifanya kazi na watu ambao hawamjui, yani yeye ni kupiga tu simu na kujificha nyuma ya keyboard.
Mwanamke mmoja tu ndio aliyefanya akapoteza kiasi kikubwa cha pesa alicho-save kwa muda wote pamoja na kusababisha dili zake kumfamya kuwa mmuaji na ndoto zake kuzima.
NETFLIX wametisha ila kama kawaida yao pia humu wametuacha watazamaji na maswali mengi, Je, Jisoo Oh na Baeggyul walitoroka na kuwakimbia polisi? Je, Jisoo Oh atafariki baada ya kuchomwa na mkasi tumboni? Au tusubiri season 2? Japokuwa series haihitaji season 2.
Series nyingi kutoka NETFLIX zitaanza kukosa ubora kutokana na hili wanalofanya mwishoni, huwa wanalazimisha kuanzisha story ilimradi watoe season nyingine zaidi. Hili nililiona pia katika series ya VAGABOND waliongeza kastori ilimradi tu waje na Season 2, MONEY HEIST nadhani ilipaswa kuishia season 4 ila kwakuwa ni NETFLIX itaendelea hadi ikose mvuto, nilicheki pia THE PLATFORM (Movie) ila mwisho pia uliniacha na maswali mengi kuliko majibu au labda ndio aina yao ya kufikisha ujumbe kwa hadhira na kutuachia homework.
NETFLIX soko lao haliwezi kufa kirahisi au kuzidiwa kirahisi na AMAZON PRIME VIDEO, USA ORIGINALS, HBO, APPLE TV au kampuni nyingine yoyote ila tu Movie na Series zao nyingi zitaanza kukosa mvuto.