NETFLIX Ni zaidi ya Shule ya Maarifa ya zaida. ikitumika Vizuri

Rweyemam105

Member
Sep 8, 2012
27
51
Hallo, kwa wale wenye access ya NETFLIX. Nimegundua jambo moja zuri sana kupitia NETFLIX online Video Library kubwa sana Duniani kwa sasa. Ambayo unaweza kui access kwa Tshs 27,000/= tu kwa mwezi au kila mwezi kwa hiyo gharama tajwa hapo juu.

Mwanzoni wakati najiunga/nanunua subscription, ilikuwa kwa minajili ya kuweza kuangalia Movies mbali mbali. Nikawa nafuatilia Movies mpya na za zamani. Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda, siku moja nikaona Tweet moja iki promote Hot documentaries on NETFLIX(Must watch).

Nikaanza kufuatilia moja baada ya nyingine, wastani wa documentaries 12 walizozielezea. Nilivyozimaliza zote, nikawa addicted na documentaries. Nilichogundua, documentaries and docuseries ni zaidi ya Movies, ni maarifa ya nmna ya kipekee mtu anaweza kuyapata kwa gharama nafuu sana, kwani zinakuwa zinaelezea chanzo na uhalisia wa jambo mwanzo mwisho, Aloooo!

Hadi sasa hivi naweza sema, nimeshaangalia docuseries na documentaries zaidi ya 200 on netflix. Nimejifunza mambo mengi sana ambayo naamini, ni maarifa ambayo nisingeweza kuyapata popote pale duniani bila ya kuwa na jitihada binafsi za kutaka kujua Mambo. Na hata ukisema uyatafute hayo maarifa, itakagurimu pesa mingi sana, pasingekuwa na msaada wa hii Online Video Library NETFLIX.

Moja ya documentaries kati ya chache zilizonivutia na kunihamasisha hadi mimi kuwa addicted ni hizi hapa, ukipata muda na wewe unaweza kuziangalia. Ila zipo nyingi kedekede. Kila moja unayokutana nayo, inamzidi mwenzie.

1. OUR PLANET 1 & 2.
2. MH370 Ndege ya Malaysia iliyopotea angani.
3. How to get Rich.
4. I am a killer
5. Icarus

Hizo ni kwa uchache tu.
Ila Netflix ni mwisho wa habari, huenda wasiwe na Movies nyingi current/mpya zinazotoka ila ni online Video Library iliyosheheni na kujitosheleza kila nyanja.

Itumieni NETFLIX vizuri katika kukuza maarifa.
images.jpg
images.jpg
images.jpg
 
Ligi ya bongo wana rekodi zake nataka nirudie kuangalia magoli ya Mayele ligi iliyopita.
 
Back
Top Bottom