NETFLIX wanafeli wapi?

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Wiki hii nilipata nafasi ya kuangalia movie pamoja na series mpya kutoka NETFLIX ORIGINALS. Hizi zote wameziandaa wenyewe;

EXTRACTION (Movie)
Hii imejipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na kuwa full packed na fights za kutosha, kwa wapenzi wa action movie hii lazima uikubali. Ila walipofeli na wanapozidi kufeli NETFLIX ni jinsi wanavyomaliza movie zao, huwa wanaacha maswali mengi kwa watazamaji; hii movie imezua maswali mengi sana, Je, Tyler alifariki baada ya kupigwa risasi ya shingo na kujitupa ndani ya maji? Je, yule anayeonekana mwisho kwa mbali wakati Ovi anaogelea ndio Tyler mwenyewe na aliwezaje kupona katika hali ile?

Kiukweli maswali ni mengi kuliko majibu, wengu tumebaki kujijibu wenyewe maana muda mwingi kazi za sanaa zinakuja na mafumbo na unapaswa kuyavumbua mwenyewe.

EXTRACURRICULAR (SERIES)
Hii ni kutoka Korea chini ya NETFLIX, story nzuri sana, waigizaji wamejitahidi na wengi wao ni wageni kabisa katika filamu huko Korea. Hii inahusu dogo anayepambana kupata pesa za shule pamoja na matumizi mengine, huku ndoto yake ni kusoma hadi chuo, ku-graduate na kufanya kazi ila dili anazopiga sasa ni haramu (Sex Trafficking) anajiita Uncle huku akifanya kazi na watu ambao hawamjui, yani yeye ni kupiga tu simu na kujificha nyuma ya keyboard.

Mwanamke mmoja tu ndio aliyefanya akapoteza kiasi kikubwa cha pesa alicho-save kwa muda wote pamoja na kusababisha dili zake kumfamya kuwa mmuaji na ndoto zake kuzima.

NETFLIX wametisha ila kama kawaida yao pia humu wametuacha watazamaji na maswali mengi, Je, Jisoo Oh na Baeggyul walitoroka na kuwakimbia polisi? Je, Jisoo Oh atafariki baada ya kuchomwa na mkasi tumboni? Au tusubiri season 2? Japokuwa series haihitaji season 2.

Series nyingi kutoka NETFLIX zitaanza kukosa ubora kutokana na hili wanalofanya mwishoni, huwa wanalazimisha kuanzisha story ilimradi watoe season nyingine zaidi. Hili nililiona pia katika series ya VAGABOND waliongeza kastori ilimradi tu waje na Season 2, MONEY HEIST nadhani ilipaswa kuishia season 4 ila kwakuwa ni NETFLIX itaendelea hadi ikose mvuto, nilicheki pia THE PLATFORM (Movie) ila mwisho pia uliniacha na maswali mengi kuliko majibu au labda ndio aina yao ya kufikisha ujumbe kwa hadhira na kutuachia homework.

NETFLIX soko lao haliwezi kufa kirahisi au kuzidiwa kirahisi na AMAZON PRIME VIDEO, USA ORIGINALS, HBO, APPLE TV au kampuni nyingine yoyote ila tu Movie na Series zao nyingi zitaanza kukosa mvuto.
 
Huo ndio utamu wa movie.
Mbona hana 24 Jack Bauer alikuwa anapotea kwenye mazingira ya kutatanisha ili tu waje na season nyingine.

Angalia na Blindspot pia ilipoishia ambapo wote wanaonekana kufa except Jane ila wanakuja na season finale

Prison Break pia walifanya hivyo kwa Michael

Tuliza munkari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah! Kweli ndio utamu wa movie mkuu ila kama hizi series wengi huwa subira inatushinda, kusubiri mpaka waanze uandaaji tena ndio swala gumu, bora waue game season 1 tu.
 
Vipi kuhusu Kingdom, series ya Netflix ya kikorea hii. Nayo ni nzuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaiangalia ila naona inapata sifa nyingi, nimeona pia wametoa season mpya. Ila kwa wapenzi wa K-Drama kuangalia hizi za NETFLIX huwa inawapa tabu maana wengi wamezoea zile kutoka SBS au JTBC ambazo nyingi huwa zinaishia season 1 tu ila hizi za NETFLIX inabidi ujipange kuona kama season 3 hivi kutoka series 1.
 
kiukweli mimi nilikuwa sio mpenzi wa series lkn nilivo kuja kuchek game of throne,imeniharibu mno kuona kuwa hakuna movie yenye adventure na fantasy na drama ambazo ni almost real life situation kama game of throne...nimejaribu kuchek the last king lkn bado haija nigusa actors wake wengi unaona kabisa hawa wanaigiza.ila kwa upande mwingine netflix hii extractio binafs ni movie ambayo ukiangalia utaona kabisa hii movieni real mtu anapambana kweli kujiokoa maisha yake na maslai yake.naomba tu kwalio nielewa wa mention movei zingine kama hizo ili nipate kuzijua na kufarahia zaid uandishi wa uwelidi wa hali ya juu ambao unakufanya kishindwa kujua nn kinaendelea ndani ya sekunde moja ijayo na huo ndo uhandishi bora zaid kwa upande wangu mm
 
Kuna series moja kali sana ila imeshaisha inaitwa homeland, hii ni ya mambo ya kijasusi. Imeisha mwaka huu ipo season mpka 8. Haita kushosha
 
Kuna series moja kali sana ila imeshaisha inaitwa homeland, hii ni ya mambo ya kijasusi. Imeisha mwaka huu ipo season mpka 8. Haita kushosha
nshawai isikia iyo ngoja niichek google hapa kwanza
 
  • Thanks
Reactions: k29
Extraction ni action packed..mitutu, ngumi na visu hamna kupumzika :)

Nimezicheki na Spenser Confidential (movie), Ozark, Luther, The Crown & The Stranger. Money Heist sijaendelea na season mpya.
 
Kama the bodyguard jina kubwa likn hamna kitu nilitegemea kuona action za maana na msako wa hatari kama jina la movie.lakin mwisho wa siku huyo mlinzi ndo anafanya kazi ya kumtia ududu boss wake anae mlinda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom