Neno shikamoo kwa kizungu!!

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,287
Nijuavyo mimi ni neno la kumpa heshma mtu aliyekuzidi umri.Sasa maswali yangu ni
1.Ni kuanzia tofauti ya miaka mingapi ndo unaweza kumpa mtu neno hili.
2.Na pia kwa kizungu tutasemaje?
 
  1. Hata mdogo wako waweza kumamkia
  2. Kizingu ya shikamoo ni SHE KOOL MORE.
Ha Ha Haaaaaa !!!!! Weekend Blues. Its just fun.
 
Waweza jumpa mtu yeyote shkamoo japo ktk jamii zetu zaidi ni kwa wakubwa. Pia sidhani kama neno shkamoo lina maana kwa kingireza
 
mmm shika-mo touch inside
mara-haba few times

nzuri zaidi kwa jinsia tofauti, salamu hunoga.
 
Shikamoo ni neno lilotokana na kiarabu enzi za utumwa, na maana yake ni kuwa niko chini ya miguu yako. Hapa ilikuwa ni bwana na mtwana.
 
Waweza jumpa mtu yeyote shkamoo japo ktk jamii zetu zaidi ni kwa wakubwa. Pia sidhani kama neno shkamoo lina maana kwa kingireza

Hata yule aliyekufanya usiku wa jana ukakosa amani, ukamshushia Sredi, pia wapaswa kumpa Shkamoo. Nakutakia mwisho wa juma mwema.
 
shikamoo manake nakushiga miguu, ni namna ya kumpa heshima bwana wako anaekutuma. Sijui ni lugha gani lkn ilianza enzi hizo za utumwa na ubwana na wenyewe walikua wanainama kweli kuwashika miguu halafu bwana huitikia marhaba huku anampigapiga kichwani. Sasa weka kwenye kizungu hayo maneno mawili shika moo, teh teh teh, have a great day
 
Shikamoo ni neno lilotokana na kiarabu enzi za utumwa, na maana yake ni kuwa niko chini ya miguu yako. Hapa ilikuwa ni bwana na mtwana.
Ni kweli kabisa TaiJike, na naomba niongezee. Kwa sababu ya historia hiyo ya 'shikamoo' hakuna tafsiri yake ya kiingereza.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom