Neno la Shukrani

Neno la Shukrani

View attachment 496726

Nina deni na wana JF! Si deni Lingine bali deni la Shukrani.... Shukrani ya mshikamano mkubwa mlioninyesha katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yangu mzazi.

Si kwa kikubwa wala kidogo kwa vipimo vya viwango vya kibinadamu, bali kwa ule moyo mlioninyesha kwa pm, posts za Faraja na kutia moyo na hata kufariji kwenye makala ile ya ndugu yangu Ambiere kivyele na hata wale walionitumia chochote.

Kwa umoja wenu na kwa pamoja nasema asanteni sana,Mama amevua mwili uharibikao na kuvaa mwili uishio milele, Amevua mwili wa asili na kuvaa mwili wa kiroho, amefaulu mtihani wake na sasa hana maumivu tena.

Maisha ya mwanadamu ni miaka 70 akiwa na nguvu ni miaka 80 na kuishi ni faida lakini kufa ni Kristo na Kristo ni ushindi..Mama ameshinda vita hii na amepumzika kwa amani.

Asante tena na tena na tena sina neno bora zaidi la kuonyesha unyenyekevu mkubwa kwenye hili

Jr...!
apumzike kwa amani.mama yetu mpendwa
 
Pole sana, na Mungu awajalie moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Pole mkuu, pole rafiki, pole sana hivi ndio nasoma hii taarifa, muombee Sana mama
 
Afu msiba umekuja kipindi hiki cha sikukuu, pole sana bro... R.I.P mama yetu
 
Pole sana Mtani. Ila nafarijika sana ninapokuona una imani ya kutosha kbsa. Maisha ni kristo na kufa ni faida. Mungu akutangulie kk
 
Pole sna mshana Mungu azidi kukutia nguvu kwenye hiki kipindi kigumu cha kumpoteza mama
 
Dah bibi yetu hope mmemaliza vema ndugu yako nilibanwa kdg ila mama alikuja pole sana kaka alikua mwali pia bibi yangu dah
 
View attachment 496726

Nina deni na wana JF! Si deni Lingine bali deni la Shukrani.... Shukrani ya mshikamano mkubwa mlioninyesha katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yangu mzazi.

Si kwa kikubwa wala kidogo kwa vipimo vya viwango vya kibinadamu, bali kwa ule moyo mlioninyesha kwa pm, posts za Faraja na kutia moyo na hata kufariji kwenye makala ile ya ndugu yangu Ambiere kivyele na hata wale walionitumia chochote.

Kwa umoja wenu na kwa pamoja nasema asanteni sana,Mama amevua mwili uharibikao na kuvaa mwili uishio milele, Amevua mwili wa asili na kuvaa mwili wa kiroho, amefaulu mtihani wake na sasa hana maumivu tena.

Maisha ya mwanadamu ni miaka 70 akiwa na nguvu ni miaka 80 na kuishi ni faida lakini kufa ni Kristo na Kristo ni ushindi..Mama ameshinda vita hii na amepumzika kwa amani.

Asante tena na tena na tena sina neno bora zaidi la kuonyesha unyenyekevu mkubwa kwenye hili

Jr...!
Ooh pole kwa kuondokewa na mpendwa wako, Mola amrehemu, akupe faraja kipindi hili ulichonacho, hakika sisi kwake ni marejeo.
 
Back
Top Bottom