Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,889
Nina deni na wana JF! Si deni Lingine bali deni la Shukrani.... Shukrani ya mshikamano mkubwa mlioninyesha katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yangu mzazi.
Si kwa kikubwa wala kidogo kwa vipimo vya viwango vya kibinadamu, bali kwa ule moyo mlioninyesha kwa pm, posts za Faraja na kutia moyo na hata kufariji kwenye makala ile ya ndugu yangu Ambiere kivyele na hata wale walionitumia chochote.
Kwa umoja wenu na kwa pamoja nasema asanteni sana,Mama amevua mwili uharibikao na kuvaa mwili uishio milele, Amevua mwili wa asili na kuvaa mwili wa kiroho, amefaulu mtihani wake na sasa hana maumivu tena.
Maisha ya mwanadamu ni miaka 70 akiwa na nguvu ni miaka 80 na kuishi ni faida lakini kufa ni Kristo na Kristo ni ushindi..Mama ameshinda vita hii na amepumzika kwa amani.
Asante tena na tena na tena sina neno bora zaidi la kuonyesha unyenyekevu mkubwa kwenye hili
Jr...!