Asha D Abinallah
Senior Member
- Apr 5, 2015
- 140
- 904
Raha ya kupumbazwa mara nyingi unakuwa hujui kuwa wewe ni muathirika wa kirusi hicho.
Yaani usipokuwa makini unaweza ukawa na jitihada kubwa ya kunyosha kidole kwa wale ambao kweli ni wazi wamepumbazwa na kitu fulani bila kutarajia hata kidogo kwamba, kama kirusi hicho cha “kupumbazwa” kingegeuka ugonjwa wa kuua haraka basi wewe hapo ulipo ni maiti.
Kuna aina nyingi ya virusi hivi katika jamii yetu, kwa leo naomba nigusie kirusi hiki ambacho kimejikita katika Ulimwengu wa Siasa.
Wengine huita Waathirika hao makundi mbalimbali kama vile Mazuzu, Msukule, Minions, Nyumbu, Lumumba, Buku7, n.k
Kumekuwepo na changamoto kubwa ya jamii hasa linapokuja suala la Kimaendeleo au uhamasishaji wa mabadiliko haswa linalorandana na Kisiasa.
Wengi katika jamii hushindwa kuwa na uwezo wa kutumia akili na ubongo wao kwa uhuru katika kuelewa jambo vema. Kunazuka kundi kubwa la mashabiki wasioweza kutetea na kusimamia hoja zao na wala hata kujipatia nafasi ya kutumia akili kupembua hoja, mawazo ama maoni.
Hii imezaa makundi matatu
Kuweza kufanikisha hilo, ni lazima kutambua tunachosimamia, kutambua tunachosimamia ndicho hujenga ramani inayojengeka kwenye kufikia malengo, iwe ya maendeleo au Mapinduzi.
Ni vema kujitathmini nafasi zetu katika kuleta maendeleo na mabadiliko.
Ningependa kupata maoni zaidi juu ya tatizo hilo ambalo limegeuka kuwa kirusi.
Neno La Leo.

- Kundi la watu ambao hujenga hoja (kwa vigezo, agenda na misingi yao wenyewe) wenye wafuasi wengi ambao wanawafuata kama upepo.
- Kundi la watu ambao lolote lile linalotoka kundi ambalo hakubaliani nalo analijengea hoja pinzani. Ambalo wafuasi wake hufuata pia bila upepo.
- Kundi la wafuasi, ambao wameweka imani yao katika kundi fulani (la kwanza na la pili). Hili ndilo kundi limeathirika vibaya sana na Kirusi hiki kupumbazwa na hivyo kuwa ‘bendera fuata upepo’. Wanatia huruma, hawajitambui wala hawaelewi kile wanachoshabikia. Hawa wanaitwa Wapumbazwa.