Neno la Leo - Kirusi cha ‘kupumbazwa’

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
Raha ya kupumbazwa mara nyingi unakuwa hujui kuwa wewe ni muathirika wa kirusi hicho.

Yaani usipokuwa makini unaweza ukawa na jitihada kubwa ya kunyosha kidole kwa wale ambao kweli ni wazi wamepumbazwa na kitu fulani bila kutarajia hata kidogo kwamba, kama kirusi hicho cha “kupumbazwa” kingegeuka ugonjwa wa kuua haraka basi wewe hapo ulipo ni maiti.

Kuna aina nyingi ya virusi hivi katika jamii yetu, kwa leo naomba nigusie kirusi hiki ambacho kimejikita katika Ulimwengu wa Siasa.

Wengine huita Waathirika hao makundi mbalimbali kama vile Mazuzu, Msukule, Minions, Nyumbu, Lumumba, Buku7, n.k

Kumekuwepo na changamoto kubwa ya jamii hasa linapokuja suala la Kimaendeleo au uhamasishaji wa mabadiliko haswa linalorandana na Kisiasa.

Wengi katika jamii hushindwa kuwa na uwezo wa kutumia akili na ubongo wao kwa uhuru katika kuelewa jambo vema. Kunazuka kundi kubwa la mashabiki wasioweza kutetea na kusimamia hoja zao na wala hata kujipatia nafasi ya kutumia akili kupembua hoja, mawazo ama maoni.

Hii imezaa makundi matatu
  1. Kundi la watu ambao hujenga hoja (kwa vigezo, agenda na misingi yao wenyewe) wenye wafuasi wengi ambao wanawafuata kama upepo.
  2. Kundi la watu ambao lolote lile linalotoka kundi ambalo hakubaliani nalo analijengea hoja pinzani. Ambalo wafuasi wake hufuata pia bila upepo.
  3. Kundi la wafuasi, ambao wameweka imani yao katika kundi fulani (la kwanza na la pili). Hili ndilo kundi limeathirika vibaya sana na Kirusi hiki kupumbazwa na hivyo kuwa ‘bendera fuata upepo’. Wanatia huruma, hawajitambui wala hawaelewi kile wanachoshabikia. Hawa wanaitwa Wapumbazwa.
ANGALIZO: Si mbaya kuwa mfuasi wa kundi lolote, ila ni vema kutia akili yako pia kuelewa kwanini upepo wa Kisulisuli unakupeleka huko.

Kuweza kufanikisha hilo, ni lazima kutambua tunachosimamia, kutambua tunachosimamia ndicho hujenga ramani inayojengeka kwenye kufikia malengo, iwe ya maendeleo au Mapinduzi.

Ni vema kujitathmini nafasi zetu katika kuleta maendeleo na mabadiliko.

Ningependa kupata maoni zaidi juu ya tatizo hilo ambalo limegeuka kuwa kirusi.

Neno La Leo.
 
Baharia tatizo "mfumo", na "mfumo" ndio mlezi mama wa hicho kirusi.

Na kwa kasi ya 'dunia ya leo' MONEY IS NOT ONLY POWER BT ALSO POWERFUL, ukibisha tumia sampuli zangu hizi chache Prof. Kabudi, Dr. Mwakyembe, Prof. Lipumba e.t.c.

Dunia ya leo hasa kwa sisi wa bara hili sio ile tena ya kusoma na kupambanua hoja za kina Alistore, Newton, Chinua, Patrice, Rostow e.t.c dunia yetu ya leo ni ya kuuliza una "shi ngapi?"
 
huwezi pingana na itikadi, sera za chama chako, ukiwa mwana CCM, lazima ufuate maamuzi ya chama, kama hukubaliani nayo ondoka tafuta chama kingine, au anzisha chama chako, hao unaowaita bendera fuata upepo unawadhalilisha tu, hata wewe ungekuwa hivyo hivyo kama wao, mbona jamii forum mnapenda sana topic za kupinga serikali sijaona ukikemea hilo
 
Baharia tatizo "mfumo", na "mfumo" ndio mlezi mama wa hicho kirusi.

Na kwa kasi ya 'dunia ya leo' MONEY IS NOT ONLY POWER BT ALSO POWERFUL, ukibisha tumia sampuli zangu hizi chache Prof. Kabudi, Dr. Mwakyembe, Prof. Lipumba e.t.c.

Dunia ya leo hasa kwa sisi wa bara hili sio ile tena ya kusoma na kupambanua hoja za kina AlistorE, Newton, Chinua, Patrice, Rostow e.t.c dunia yetu ya leo ni ya kuuliza una "shi ngapi?"
Kwenye Sampuli umemsahau Dr Bashiru
 
huwezi pingana na itikadi, sera za chama chako, ukiwa mwana ccm, lazima ufuate maamuzi ya chama, kama hukubaliani nayo ondoka tafuta chama kingine, au anzisha chama chako, hao unaowaita bendera fuata upepo unawadhalilisha tu, hata wewe ungekuwa hivyo hivyo kama wao, mbona jamii forum mnapenda sana topic za kupinga serikali sijaona ukikemea hilo

Inawezekana hujamwelewa Asha D,
jaribu kumsoma tena kwa utulivu.

:Jamii forum ni kina nani?
:Nawewe upo katika jamii ipi?
Katika makundi matatu alieleza mleta mada, wewe upo kundi gani?
Mwisho tazama vizuri, fikiri sana na uliza ujue.
 
Nimesoma sehemu kwenye kitabu cha Meyers (They thought they were free) They Thought They Were Free: The Germans, 1933-45 by Milton Mayer, an excerpt, 2017 edition

Humo ameelezea visa vya Wajerumani waloishi zama za Hitler. Unaweza usielewe mtu alochaguliwa aliwezaje kuvuka vizingiti vya katiba na sheria zao na wao wapo.
Na kuna Mwanaharakati mmoja alisema watu hufikiri nchi za Africa zenye watawala wanaocheza na katiba kujiongezea muda kila leo wananchi wake huwa ni wajinga.
La hasha! Wanapumbazwa.

Mwanzoni mnaweza kujadili baadaye hamtaweza kabisa. Sababu kubwa ni kuwa hakuna mwenye kuhisi mwisho.
Zimbabwe wale walokuwa wakimpelemba Mugabe ndio walomuondoa. Hii maana yake walikuwa wakimsifu basi tu lakini wahakuamini anachokiamini. Wako wengi sasa tunafanya hivyo hapa leo.

Haya tunayoyashuhudia si ya kawaida. Hata katika maendeleo hayana mwisho mzuri.
 
Kwa kweli kirusi cha kupumbazwa kimekuwa tatizo kubwa sana katika Tanzania yetu ya leo. Vijana wengi tumejikuta tunakosa uelekeo na msimamo na hatimaye tunaangukia kundi la tatu ambalo tunakuwa bendela fuata upepo. Kimsingi, watu wengi tunajikita na kinachotrend zaidi kuliko kuchunguza na kuangalia mambo katika ukweli na uchambuzi wa jamii yetu. Mmmh! Mwenyezi Mungu atuepushe na hiki kirusi cha kupumbazwa maana la sivyo future yetu inaenda kuteketea Mkuu.
 
Katika hayo makundi ya watu, uliyoyaweka kiukweli yapo zaidi kwenye ishu yeyote inayojumuisha fundamentalism ambayo ni zao la schoolism. Katika hii dunia isiyotaka falsafa, watu hulazimishwa kufuata moja kati ya upande na kuupinga upande mwingine. being with or being against.

Sio kosa sana, japo kiuhalisia linafanya kweli watu kuwa na hicho kirusi cha kupumbazwa na uhafidhina wanaouleta katika wanayoyaona.
I follow what Nietzsche said about Ubernsmesch. Kitu Kezilahabi amekiita Nagona!
 
Unapokuwa muathirika wa virusi tajwa hususani kwenye masuala ya kisiasa, wakati mwingine unaweza kujikuta unaona yale yanayoendelea ni sawa tu hata kama sio hali halisi. Unajijenga kuangalia upande mmoja pekee na ni vigumu sana kuona au kukubali mazuri yanayofanywa na wengine ambao hawana mtazamo sawa na wa kwako.

Kuna muda unaweza kushuhudia chama chako kinafanya mambo kinyume na utaratibu lakini utafanyaje? Unaona ni saw tu kwasababu wao ndio wanaofanya.

Nchi yoyote ile haiwezi kwenda namna hii. Kila chama kina nafasi yake na kinapaswa kuheshimiwa. Tuna kila haki za kuwa wafuasi wa kile tunachoona kinaendana na ideology zetu lakini hii isiwe sababu ya kuwaonea wengine. Na wao wana haki hii vile vile.

Nafasi yetu katika kuleta maendeleo ni kubwa sana ikiwa itatumika accordingly.
 
denoo49,
Mkuu umeona mbali sana, shilingi ndo inafanya maamuzi, mimi nilijifunza jambo kubwa pale Mh. Lowasa alipohamia upinzani na akaonyesha ana nguvu kubwa ya kuchukua nchi, angalia kundi kubwa lililomfuata kwa kusema mabaya ya chama chao kilichowafanya wawe maarufu.

Baada ya uchaguzi na matokeo yake, wengi wamerudi nyumbani na wengine hawajulikani walipo. Naungana na wewe pesa ina nguvu, Tupambane tumwabudu Mungu na tutafute pesa
mengine yatajileta yenyewe.
 
hakuna apendae kupumbazwa bt wengi mifumo yakiutawala ndo huwalazim kupumbazika, coz wakosoaji wote wenye hoja zenye mantiki ajili yakuwatoa tongotongo wapumbazwa huwekewa na mamlaka vizingiti vyakuonekana waovu, jambo hili hupelekea wapumbazwa kuendelea kuona wapo sahih
 
Well, kwanza ni aibu sana kwamba hiki kirusi hakijatuathiri tu sisi wakina ‘no-school-at-all’ bali hadi wale wenye ‘title’ za juu kabisa katika uwanja wa kitaaluma, tena hawa wana hiki kirusi, plus bakteria mwingine wa usaliti. Wana ‘misimamo’ inayohamishika kirahisi, hususani ‘twist’ ikihusisha ujira kiduchu tu toka dolani – wanalegea na kugeuzwa kundi moja kati ya mawili ya mwanzo. Hawa ni wanazuoni waliobebewa vichwa vyao wanaofanya hii hali kuendelea kuwepo.

Cha muhimu hapa ni kujifunza tu kuwa mahaba na mikumbo ime-replace utashi, jambo ambalo litaendelea kuwa na athari nzito sana. #RestoreUtashi
 
huwezi pingana na itikadi, sera za chama chako, ukiwa mwana CCM, lazima ufuate maamuzi ya chama, kama hukubaliani nayo ondoka tafuta chama kingine, au anzisha chama chako, hao unaowaita bendera fuata upepo unawadhalilisha tu, hata wewe ungekuwa hivyo hivyo kama wao, mbona jamii forum mnapenda sana topic za kupinga serikali sijaona ukikemea hilo

MOja wapo ni huyu.
topic inahusu pande zote, ila wewe tayari ushaiweka kisiasa na umeattack JF.
duh!
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom