Neno la Leo Januari 10, 2024: Maombi Yenye Nguvu

NGOSWE2

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
635
547
Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.
Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu.*Naye akanena, Enenda tena mara saba.

Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie...(1Wafal 18:42b-45).

SOMO KUU: MAOMBI YENYE NGUVU.

Pointi ya Kwanza: Sababu za kuombea.

Biblia inatoa sababu za wazi kabisa Kwa nini watu wa Mungu wanapaswa kuomba:

(1). Ya kwanza na ya muhimu zaidi, waumini wameagizwa na Mungu kuomba. Agizo la kuomba linotoka kwenye midomo ya mtunga Zaburi (Zab 105:4; 1 Nyak 16:11), manabii (Isa 55:6; Amo 5:4,6), mitume (Efe 6:17-18; Kol 4:2; 1Thes 5:17), na Bwana Yesu mwenyewe ( Math 26:41; Lk 18:1; Yoh 16:24). Mungu anapenda sana ushirika wetu; Kwa njia ya maombi tunadumisha uhusiano wetu pamoja naye.

Mpendwa wangu katika Bwana,

Neno la Mungu linatuagiza na kusema :*"mtakeni Bwana na nguvu zake"*inamaansha tunaalikwa sio tu kuutafuta uwepo wa Mungu bali pia uwezo na nguvu za neema yake Kwa sababu zifuatazo:

(a). Sisi sote tunahitaji nguvu za Ki-Mungu ili kudumu katika wokovu, kuishi maisha yanayomoendeza Mungu, na kushuhudia katika uwezo wa Roho Mtakatifu (Mdo 1:8; 2:4)

(b). Ni lazima Kila siku tumwangalie Mungu na neema yake, la sivyo tutashikwa na udhaifu wa kiroho na kushindwa, hivyo basi, ni lazima tuchochee wenyewe siku zote kumtafuta Kwa bidii Kwa moyo wote ( Math 7:7-8) na tutarajie ishara za uwepo wake na nguvu katika maisha yetu ( 2Nya 26:5; Kumbu 4:29).

N.B: KUMBUKA MWAKA HUU 2024 NI MWAKA WA KUZAMA KWENYE KILINDI CHA MAOMBI ILI UTOBOE

Nakutakia Siku njema, nakuombea neema ya maombi iwe juu yako Mwaka huu wa 2024.
 
Ndugu mpendwa, leo tunaendelea na somo letu lenye kichwa:

Maombi Yenye Nguvu.

Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.
Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu.*Naye akanena, Enenda tena mara saba.
Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie...(1Wafal 18:42b-45).

SOMO KUU: MAOMBI YENYE NGUVU.

Pointi ya Kwanza: Sababu za kuomba.

Biblia inatoa sababu za wazi kabisa Kwa nini watu wa Mungu wanapaswa kuomba:
(2).Maombi ndicho kiungo muhimu katika kupokea Baraka na Nguvu za Mungu, na kutimilizwa Kwa ahadi zake. Vifungo vingi katika Biblia vinaelezea kanuni hii. Kwa mfano, Yesu, aliahidi kwamba wafuasi wake watapokea Roho Mtakatifu iwapo watadumu katika kuomba, kutafuta na kubisha kwenye mlango wa Baba yao aliye mbinguni ( Lk 11:5-13). Hivyo baada ya kupaa kwake, wafuasi wake walikuwa wakidumu Kwa moyo mmoja katika kusali ghorofani(Mdo 1:14) mpka Roho Mtakatifu alipomimiminwa kwa Nguvu juu yao katika siku ile ya Pentekoste ( Mdo 1:8; 2:1-4).

Mpendwa wangu katika Bwana.

Mara Kwa mara Mtume Paulo aliomba Maombi yafanyike Kwa ajili yake, akifahamu ya kuwa kazi yake isingefanikiwa mpaka pale ambapo Wakristo watakuwa wanamuombea ( Rum 15:30-32; 2Kor 1:11; Efe 6:18-20; Kol 4:3-4).
Yakobo anaelezea wazi wazi kwamba muumini anaweza kupokea uponyaji wa mwili wake kutokana na kuomba Kwa Imani(Yako 5:14-15)

N.B: KUMBUKA MWAKA HUU 2024 NI MWAKA WA KUZAMA KWENYE KILINDI CHA MAOMBI ILI UTOBOE

Nakutakia Siku njema, nakuombea neema ya maombi iwe juu yako Mwaka huu wa 2024.
 
Back
Top Bottom