Kumcha Mungu kunaongeza siku za mtu za kuishi

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
KUMCHA MUNGU KUNAONGEZA SIKU ZA MTU ZA KUISHI.

Hakuna shaka kuwa tulizaliwa. Na ni kweli kuwa tunaishi. Na tuna uhakika kuwa kuna siku tutakufa.

Maisha ya mwanadamu Yana kikomo, lakini kumcha Mungu kunaweza kuongeza siku za mtu za kuishi.

Neno la Mungu linasema,
"Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu, bali miaka yao wasio haki itapunguzwa."
MITHALI 10: 27

✨Ukiwa mtu mwenye kutenda mema, unaweza kumkumbusha Mungu juu ya mema uliyotenda na kuomba kuongezewa siku za kuishi.

Unaweza Kupinga lakini, tukisoma biblia, kuhusu habari za Hezekia, tutakubaliana katika hili.

Neno linasema,
"Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,

akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema,

Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.

Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu."
ISAYA 38:1-6

Hapa tunaona Hezekia aliongezewa miaka 15 ya kuishi pamoja na kuuokoa mji wake na kuulinda.

✨Mungu anaweza kusikia hata maombi ya watu uliowatendea mema na ukaongezewa siku za kuendelea kuishi.

Mfano:
Tabitha au Dorcasi ambaye wajane walimlilia Mungu arejeshe uhai wake kwakuwa aliwatendea mema nyakati za uhai wake.
Soma=
MATENDO 9:36-41

✨Mungu anaweza kuzuia usipoteze maisha hata pale maadui zako watakapotaka kukatisha uhai wako.

Mfano:
Mtume Paulo alipigwa mawe na kuburutwa hadi nje ya mji hadi watu walijua kuwa amekwisha kufa lakini baadae anasimama na kwenda zake.
Soma=
MATENDO 14:19-20

✨Mungu atakuweka hai kusudi uzidi kuitenda kazi yake.
Neno linasema
"Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana."
ZABURI 48:17

✨Ukiwa mtenda mema, hata wakati wa kufariki kwako utakapowadia utaufurahia kwasababu utakuwa umetimiza kusudi lako la kuja duniani.

Neno linasema
"Kwa maana mimi sasa namiminywa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda.
Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake."
2TIMOTHEO 4:6-8

✨Ndugu zangu katika Bwana, tuzidi kutenda yaliyo mema na kuomba Mwenyezi Mungu atujalie mwisho ulio mwema.

Neno linasema
"Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.'
MWANZO 25:8

✨Nafasi hii ya kufa katika uzee mwema, haikuwa kwa Ibrahimu peke yake bali kwa kila mwenye kuishi maisha yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Muhimu hapa sio kufa katika uzee, bali inategemea na kusudi la Mungu juu ya maisha yako hapa duniani. Na ijapofika kikomo basi turejee mbinguni tukiwa wema machoni pa Mungu.

Na hili ndilo neno la Bwana katika siku ya leo.

#No_learning_No_earning
So we have to Learn

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

To Join Our Group
"Extreme Knowledge Organization"
Tuma neno "NIUNGE" kwenda Namba 0713736006
IMG_20231013_192454_459.jpg

👇👇
 
Babu yangu alikua haamini mambo ya Mungu ila Ali ishi miaka 116 na alikufa bila kuumwa chochote.

Hizo ni swaga tu za kuendelea kunasa waoga wa kufa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom