Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Umesema vema. Neno la kiingereza 'dear' lina 'utata' (i.e. lina maana zaidi ya moja!). Kwenye kiingereza neno 'dear' linaweza kutumika kama kivumishi (adjective), interjection, jina(noun) au adverb (kielezo).
Kama alivyodadavua Creative Thinker hapo juu, neno 'dear':
Likitumika kama kivumishi (adjective), linaweza kuwa na maana zifuatazo:
Pia linatumika kama kielezo (adverb) kumaanisha sana au kiasi kikubwa (mfano: The effort would cost them dear).
- mbaya (i.e. severe, sore mfano: .. in our dear peril)
- enye thamani (highly valued Mfano dear friend) kwenye barua za kiofisi nadhani linabeba maana hii.
- enye kupendwa (affectionate, fond)
- aghali (expensive mfano: mangoes are very dear just now)
Linatumika kama jina (noun), linaweza kuwa na maana ya: Mwenye kupendwa/mpenzi (a loved one sweetheart!) au Mtu anaependeka (a lovable person).
Pia, neno dear linatumika kuonesha kukerwa, kushangazwa nk (interjections or exclamations) mfano: Oh, dear! Does it hurt?, Dear me! Thats a surprise!
Mkuu hapa tuko pamoja. Ambaye hatataka kuelewa kutokana na maelezo yako, shauri yake!!!!
Tiba