NEMC wasikamate tu mifuko ya plastiki; waangalie miundombinu ya mifereji Dar, wasingoje mafuriko ndio wamtafute mchawi

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wada!

Naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha hawa ndugu zetu wa NEMC hususa kipindi hiki cha kiangazi, kuangalia na kukagua miundombinu ya mifereji yetu ya jiji la Dar es Salaam.

Naona NEMC wamekuwa kama wanazima moto vile kwenye baadhi ya mambo ambayo ni wajibu wao hususa miundombinu ya mifereji baadhi ilijengwa kwa pesa nyingi za serikali imekuwa ikiharibiwa na baadhi ya watu wanaofanya ujenzi kando ya mifereji pasipo kuangalia athari za kimazingira.

Baadhi ya mifereji iliyojengwa hivi karibuni imeanza kujaa na kutema sasa sijui masika itakuwaje. Nashauri NEMC wajenge taratibu za kuzunguka kipindi km hiki kuangalia na kukagua miundombinu ya mifereji sio kungoja mpk masika,waache kujikita tu kwny kukamata mifuko ya plastic.
 
Swala la usafi likikomaliwa Dar itapendeza.

Kwanza waondoe machinga afu waondoe wote wanaofanya kazi kwenye miundombinu ya serikali.
 
Back
Top Bottom