NEMC kufanya msako wa wanaopiga kelele nyakati za usiku kwa kiwango kilichozidi Desibeli 40

Haiwezekani yani mlio wa mvua uwe kimya kuliko friji ya Samsung kuna walakini😅😅😅 katika hili bandiko lako wakati mvua ikinyesha hata TV haiskiki vizuri bila kuongeza sauti yake!
Inategemeana na hayo matone ya mvua yanafikia katika surface gani. Kama ni bati za kawaida na ndani No Gypsum Ceiling Board mirindimo na mitetemo ya sauti haikwepeke na Sound production yake itakuwa ni beat after beat.
Lakini mvua hiyo hiyo ikifall kwenye surface ya kigae sound production yake itakuwa ndogo ukilinganisha na kwenye bati.
The same na kwenye friji uenda fridge compressor yako ina matatizo au unaipa fridge mzigo mkubwa ukilinganisha na uwezo wa compressor yake hapo unakuwa umeioverload.
 
Barabara ina bar
Ukianzia dagaa dagaa,kona pub,sportslounge,Ibungu,TTG,Perfect etc

Ngoja tuone kama kweli. Kabla hawajafika huko kuna sehemu zipo karibu na ofisi zao wangefuatilia kwanza. i.e Lile gorofa pale victoria au TIPs kule karibu na Migombani
 
Kuna mambo mengi muhimu na ya maana kuhusu mazingira yanayotakiwa kutekelezwa nchini.

Mfano wameshindwa kuzuia ujenzi holela wanakuja na maswala ya kelele.

Kwa jinsi nyumba zilivyojengwa hovyo mitaani hata ukikohoa tu tayari ni kelele na kero kwa mwingine.

Hii operation haifiki popote kutokana na complexity ya mazingira pia ukichangia gharama za uendeshaji na upuuzaji wa wananchi na watekelezaji wenyewe.

Ni hasara na kupoteza muda.
Ni vizuri kujua kwamba nilikuwa sahihi.
Ni kupoteza muda tu na mikwala isiyo na msingi.
 
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linaanza msako wa kukamata na kuwafikisha mahakamani wanaopiga kelele za kiwango cha juu usiku kinachozidi desibeli 40 .

Msako huo unafanywa nchi nzima katika maeneo tofauti ikiwamo nyumba za ibada,kumbi za starehe, klabu, baa, mitaani na maeneo mengine hatua iliyofikiwa kutokana na kukithiri kwa kelele kunakoleta athari kwa afya ya binadamu na viumbe wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema kero za kelele zimeongezeka nchini katika maeneo tofauti na zinaathiri afya ya wanadamu na kusababisha malalamiko .

"Kero ya kelele na mitetemo isiyokubalika imekuwa ikiongezeka licha ya wapiga kelele hao kufahamu viwango vya kelele zinazokubalika, sasa (kesho) nchi nzima tunaanza msako,anayepiga kelele kwa kiwango cha zaidi ya desibeli 40 usiku tutamkamata na kumfikisha mahakamani,"alisema Dk Gwamaka

Alisema vipo viwango vya kelele vina yoruhusiwa na wamiliki au viongozi wa nyumba hizo wanazifahamu kwa sababu ni moja ya vibali wanavyopaswa kuwa navyo kabla ya kuanzisha ama nyumba ya ibada,kumbi ya starehe,baa na nyingine.

Alitaja viwango vya kelele au mitetemo inayokubalika mchana ni desibel hadi 60 na kuanzia saa nne usiku hadi asubuhi ni desibel 40 na si zaidi ya hapo.

Alisema athari za kelele kwa binadamu ni pamoja na kupoteza usikivu, kuleta msongo wa mawazo kutokana na kukosa usingizi,kupunguza umakini katika kusoma kwa wanafunzi na hata watumishi na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wenye maradhi ya moyo.

Aidha alisema kwa viumbe hai vipo vinavyotoweka kwa sababu mazingira ya kelele yamezidi na hata kusababisha athari kwa wajawazito na kwa watoto wachanga kuzaliwa viziwi kutokana na athari ya mitetemo aliyopata kwa mama wakati wa ujauzito.

Dk Gwamaka alisema kwa mwaka huu, wameshapokea malalamiko 300 kutoka kwa wananchi juu ya kero za kelele kwenye nyumba hizo na kwamba hatua sasa zinakwenda kuchukuliwa kuhakikisha sheria za mazingira zinalindwa na wananchi wanalala.

Alitaja faini na adhabu ya kupiga kelele na mitetemo kwa kiwango cha juu zaidi ya kinachokubalika kuwa ni faini kuanzia Sh milioni mbili hadi milioni 10 na kifungo cha hadi miezi sita. Aliwataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kupiga simu ya bure kutoa kero eneo lenye kelele kwa namba 0800110115 au 0800110117 na 0800110116.
Waanze na misikiti na makanisa.....watu wamelala usiku wa manane, saa kumi kasorobo mtu unaamshwa eti uende kuswali msikitini kwa sababu swala ni muhimu kuliko usingizi. Seriously, what kind of bullshit is this? Kila mwanadamu inabidi alale ili apate nguvu ya kufanya kazi zake na kulitumikia taifa. Au mke wa mtu anaacha familia yake nyumbani kwenda kupiga kelele kanisani usiku mzima, mwisho wa siku anazaa mtoto anayefanana na mchungaji wake.
 
Mwaka jana nilienda Arusha aisee nilipofikia sikuwa nalala hayo makelele ya makanisa.Ni usiku kucha,siku 7 za juma
 
Back
Top Bottom