NEMC kufanya msako wa wanaopiga kelele nyakati za usiku kwa kiwango kilichozidi Desibeli 40

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linaanza msako wa kukamata na kuwafikisha mahakamani wanaopiga kelele za kiwango cha juu usiku kinachozidi desibeli 40 .

Msako huo unafanywa nchi nzima katika maeneo tofauti ikiwamo nyumba za ibada,kumbi za starehe, klabu, baa, mitaani na maeneo mengine hatua iliyofikiwa kutokana na kukithiri kwa kelele kunakoleta athari kwa afya ya binadamu na viumbe wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema kero za kelele zimeongezeka nchini katika maeneo tofauti na zinaathiri afya ya wanadamu na kusababisha malalamiko .

"Kero ya kelele na mitetemo isiyokubalika imekuwa ikiongezeka licha ya wapiga kelele hao kufahamu viwango vya kelele zinazokubalika, sasa (kesho) nchi nzima tunaanza msako,anayepiga kelele kwa kiwango cha zaidi ya desibeli 40 usiku tutamkamata na kumfikisha mahakamani,"alisema Dk Gwamaka

Alisema vipo viwango vya kelele vina yoruhusiwa na wamiliki au viongozi wa nyumba hizo wanazifahamu kwa sababu ni moja ya vibali wanavyopaswa kuwa navyo kabla ya kuanzisha ama nyumba ya ibada,kumbi ya starehe,baa na nyingine.

Alitaja viwango vya kelele au mitetemo inayokubalika mchana ni desibel hadi 60 na kuanzia saa nne usiku hadi asubuhi ni desibel 40 na si zaidi ya hapo.

Alisema athari za kelele kwa binadamu ni pamoja na kupoteza usikivu, kuleta msongo wa mawazo kutokana na kukosa usingizi,kupunguza umakini katika kusoma kwa wanafunzi na hata watumishi na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wenye maradhi ya moyo.

Aidha alisema kwa viumbe hai vipo vinavyotoweka kwa sababu mazingira ya kelele yamezidi na hata kusababisha athari kwa wajawazito na kwa watoto wachanga kuzaliwa viziwi kutokana na athari ya mitetemo aliyopata kwa mama wakati wa ujauzito.

Dk Gwamaka alisema kwa mwaka huu, wameshapokea malalamiko 300 kutoka kwa wananchi juu ya kero za kelele kwenye nyumba hizo na kwamba hatua sasa zinakwenda kuchukuliwa kuhakikisha sheria za mazingira zinalindwa na wananchi wanalala.

Alitaja faini na adhabu ya kupiga kelele na mitetemo kwa kiwango cha juu zaidi ya kinachokubalika kuwa ni faini kuanzia Sh milioni mbili hadi milioni 10 na kifungo cha hadi miezi sita. Aliwataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kupiga simu ya bure kutoa kero eneo lenye kelele kwa namba 0800110115 au 0800110117 na 0800110116.
 
Vinakubalika kwa makubaliano na nani?

Je wananchi wameshirikishwa katika kufikia viwango hivyo?

Je kuna ulazima gani kuwalazimishacwatu kusikia kelele wasizohusika nazo?

Kwanini isiwe amri kwa wote wanaotaka kelele hizo kufunga sound proof kama requirement kabla ya kuruhusiwa kufanya shughuli zao?
Miji yetu imepanuka sana, je huyo Mkurugenzi hajaona umuhimu wakuweka namba ya simu ya wazi ya kufikishia malalamiko yao kwa kuzingatia kwamba watendaji wake hawawezi kufika kila kona kukabiliana na tatzo hilo?

Kama jambo hili likisimamiwa vizuri linaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato ya serikali kuanzia vinakouzwa hivyo vyombo mpaka kwa watumiaji wa mwisho
 
Waje wajeeee.
Nchi yetu ufanyakazi kazi ni kukurupuka na wa msimu ndiyo maana hali haibadiliki. Kama ni mji wataacha watu wajenge holela wee mpaka ikifikia kiwango cha juu ndiyo wanakurupuka kuja na tamko au onyo.

Na utekelezaji wa tamko unakuwa wa kukurupuka, uliojaa rushwa na wa msimu. Yaani kila sekta ni hivyo hivyo. Si wamachinga, si uegeshaji wa magari, si uendeshaji wa magari na bodaboda, you mention...

Hili tamko ni upotolo kama upotolo mwingine wowote. NEMC wajaribu kufanya kazi malengo, wazuie matatizo kabla hajajitokeza na siyo kusubiri matatizo yakishakuwa sugu ndiyo wanajaribu kuyashughulikia.

Matokeo yake yanakuwa ni chaos, rushwa, usumbufu na kila aina ya ushenzi. Kwa sababu uzembe ni wao na walijipa likizo na kuacha mambo yajindee holeli kwa miaka mingi, basi watafute njia nzuri ya kushughulikia tatizo bila kuleta bughula. Waanze na elimu, watoe muda wa masahihisho na mwisho wachukue hatua kama kuna ambao hawajarekebisha.
 
Hiyo desibeli ndio nini ? mngetumia muda kutuelemisha kuliko kuanza kuasakana tu
images (51).jpeg
 
safi sana NEMC kwa kazi nzuri, sijawahi kuona kazi nzuri kama hii tangu nimeanza kuisikia NEMC masikion, Kumbe inawezekana!!!
sasa hakikisheni pia VICHAKA/MAPORI yanaondolewa sehemu za mijini, mfano DSM kuna vichaka vingi sana maeneo ya pembezoni, mkishirikiana na wizara ya ardhi hakika mtatokomeza mapori ktk Jiji la DSM haswa maeneo ya pembezoni kuna vichaka/mapori mengi ambayo yanachangia kuficha wahalifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waweke namba ya wazi ya kuwafikishia malalamiko 24/7
 
Kuna mambo mengi muhimu na ya maana kuhusu mazingira yanayotakiwa kutekelezwa nchini.

Mfano wameshindwa kuzuia ujenzi holela wanakuja na maswala ya kelele.

Kwa jinsi nyumba zilivyojengwa hovyo mitaani hata ukikohoa tu tayari ni kelele na kero kwa mwingine.

Hii operation haifiki popote kutokana na complexity ya mazingira pia ukichangia gharama za uendeshaji na upuuzaji wa wananchi na watekelezaji wenyewe.

Ni hasara na kupoteza muda.
 
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linaanza msako wa kukamata na kuwafikisha mahakamani wanaopiga kelele za kiwango cha juu usiku kinachozidi desibeli 40 .

Msako huo unafanywa nchi nzima katika maeneo tofauti ikiwamo nyumba za ibada,kumbi za starehe, klabu, baa, mitaani na maeneo mengine hatua iliyofikiwa kutokana na kukithiri kwa kelele kunakoleta athari kwa afya ya binadamu na viumbe wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema kero za kelele zimeongezeka nchini katika maeneo tofauti na zinaathiri afya ya wanadamu na kusababisha malalamiko .

"Kero ya kelele na mitetemo isiyokubalika imekuwa ikiongezeka licha ya wapiga kelele hao kufahamu viwango vya kelele zinazokubalika, sasa (kesho) nchi nzima tunaanza msako,anayepiga kelele kwa kiwango cha zaidi ya desibeli 40 usiku tutamkamata na kumfikisha mahakamani,"alisema Dk Gwamaka

Alisema vipo viwango vya kelele vina yoruhusiwa na wamiliki au viongozi wa nyumba hizo wanazifahamu kwa sababu ni moja ya vibali wanavyopaswa kuwa navyo kabla ya kuanzisha ama nyumba ya ibada,kumbi ya starehe,baa na nyingine.

Alitaja viwango vya kelele au mitetemo inayokubalika mchana ni desibel hadi 60 na kuanzia saa nne usiku hadi asubuhi ni desibel 40 na si zaidi ya hapo.

Alisema athari za kelele kwa binadamu ni pamoja na kupoteza usikivu, kuleta msongo wa mawazo kutokana na kukosa usingizi,kupunguza umakini katika kusoma kwa wanafunzi na hata watumishi na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wenye maradhi ya moyo.

Aidha alisema kwa viumbe hai vipo vinavyotoweka kwa sababu mazingira ya kelele yamezidi na hata kusababisha athari kwa wajawazito na kwa watoto wachanga kuzaliwa viziwi kutokana na athari ya mitetemo aliyopata kwa mama wakati wa ujauzito.

Dk Gwamaka alisema kwa mwaka huu, wameshapokea malalamiko 300 kutoka kwa wananchi juu ya kero za kelele kwenye nyumba hizo na kwamba hatua sasa zinakwenda kuchukuliwa kuhakikisha sheria za mazingira zinalindwa na wananchi wanalala.

Alitaja faini na adhabu ya kupiga kelele na mitetemo kwa kiwango cha juu zaidi ya kinachokubalika kuwa ni faini kuanzia Sh milioni mbili hadi milioni 10 na kifungo cha hadi miezi sita. Aliwataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kupiga simu ya bure kutoa kero eneo lenye kelele kwa namba 0800110115 au 0800110117 na 0800110116.
Kuna makanisa ya walokole aisee wao ni makelele full blast mpaka majirani hatulali. Wake hapa mbezi Jogoo karibu na kanisa la Gamanywa (WAPO radio) ni makelele muda wote na Kuna vijana wwnalala hapo kanisani ni shida tupu.

Yani unaweza kushangaa saa kumi na mbili asubuhi wanawasha makelele ni kwaya na magitaa makelele balaa, this is getting out of control.

NEMC wasisshie kwenye bar tu wake kwa hizi kelele za makanisa, viwanda holela vya mtaani kama vya kutengeneza matofali kwa mashine za umeme Zina kelele sana.
 
Back
Top Bottom