Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,253
MEYA wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe amewataka wamiliki wa Makanisa na Misikiti mjini hapa,kufuata sheria za utunzani wa Mazingira na kuacha kuzalisha kelele chafuzi zinazobughudhi na kuleta athari kwa wananchi.
Iranghe ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini kuhusu utunzaji wa mazingira,yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC na kutaka mafunzo hayo yawe endelevu ili kupunguza athari zinazotokana na mitetemo ya mziki.
Meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini,Lewis Nzali alisema wamelazimika kutoa semina hiyo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya uwepo wa kelele chafuzi zinazosababishwa na makanisa,viwanda,misikiti na kumbi za starehe.
Baadhi ya viongozi wa dini,mch.Estomih Mwanga wa kanisa la Last Glorious ,lililopo Ungalimited na Julieth Masawe wa kanisa la Pentekoste Ebenezer walisema semina hiyo itawasaidia sana katika kusimamia mazingira kwani wengi wao walikuwa wakiendesha mahuburinkwa sauti kubwa kwa sababu hawakuwa wanajua kuwa ni kosa kisheria.
"Ki ukweli tulikuwa hatujui kama tunavunja sheria kwa kupiga kelele zinazochafua mazingira ila tulikuwa tunajua ni kwamba tunaendesha ibada kihalali"alisema mch.Julieth.
Naye mch Mwanga alisema semina hiyo ni fursa ya kupata elimu itakayosaidia kuwarejesha kwenye msingi na kuepusha kupiga kelele chafuzi kwenye makanisa yao.