Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,337
- 17,566
Namaanisha mifumo ya kinyonyaji (systematic racism).Mara kadhaa umezungumzia neno KUONDOA ALAMA YA WEUPE. Sijui una maanisha nini?
Hizo pesa zinazobaki mbona hazi saidii 80% wa SA wanaoishi kwenye shanty towns, zinaenda wapi?Kama ukiwa mfuatiliaji wa siasa za kimataifa vizuri ungegundua kwamba hata Wakulima na Wenye migodi Afrika ya kusini walitaka kutoka kwa kutoa hela yao katika mabenki katika miaka ya karibuni baada ya kuona wakulima wa Zimbabwe wanaporwa mashamba. Serikali ya Afrika ya kusini iliwaambia wawekezaji weupe haitapora mashamba wala migodi yao. Lakini hawakuamini, bado wakataka kutoka Afrika ya kusini na kuhama na mtaji wao. Lakini walishindwa kuhamisha mtaji wao kutokana na sheria kali ya REPATRIATION OF CASH ya Afrika ya kusini na hiyo ndiyo sababu iliyofanya wabaki kwa lazima.
Katika sheria hiyo ambayo inamtaka mwekezaji au yeyote mwenye biashara atoe nje ya nchi asilimia 15 tu ya kiasi anachoingiza kwa mwaka na hivyo kufanya asilimia 85 ya mapato ya mtu huyo kubaki ndani. Hiyo inamaanisha kwamba hata kama unataka kuhamia nchi nyingine lakini huwezi kuhama na mapato yako ambayo umeyachumia Afrika ya kusini.
Bado tunarudi pale pale, hiyo 85% imewasaidia nini watu wanaoishi kwenye townships?Hicho unachokisikia kuwa Johannesburg ilijengwa kwa dhahabu ya migodi ya Kimberley ni kweli. Lakini unachotakiwa kujua pia ni ukweli kwamba kasoro ya utawala wa serikali ya Afrika ya kusini ilikuwa ni ubaguzi wa rangi,..lakini katika maeneo mengine kama kusimamia sheria na uchumi wao walikuwa vizuri sana.
Watu waliowekeza katika migodi, baada ya kuuzwa kwa dhahabu na madini mengine, ukiacha masuala ya serikali kuwa na mrahaba na kuchukua kodi yake, lakini mmiliki wa mgodi alitakiwa kurudisha nyumbani Afrika ya kusini asilimia 85 ya mapato yake kwa mujibu wa sheria.
Wataalam wa kiuchumi wanasema ni bora hata serikali isichukue kodi toka kwa investors lakini ihakikishe kuwa asilimia 85 ya mapato yao yanabaki au kurudi nyumbani ndipo utaona faida ya uwekezaji.
Ukiacha Afrika ya kusini, nchi nyingine kusini mwa jangwa la Sahara ambayo iko makini katika kuhakikisha sheria ya kurudisha mapato ya uwekezaji nyumbani inasimamiwa vizuri ni Botswana.
Utasemaje wasingeweza, mbona Tanzania yenye eneo zaidi ya mara mbili za Zimbabwe inazalisha na kusaza kwa kutumia wakulima wadogo wadogo? Mugabe alifanyiwa fitna tuu na waingereza na nchi za Afrika hazikufanya jitihada zozote (kama ilivyokuwa Libya) kumsaidia. Hayo mashamba yalinyang'anywa kwa nguvu kutoka kwa wenyeji, hivyo ilikuwa sawa kurudishwa kwa wenyewe.Mugabe alikosea sana lazima ujue hilo. Alikuwa sahihi katika nia yake kugawa ardhi kwa wakulima wazawa weusi kwa sababu ilikuwa ni ardhi ndiyo hasa waliyoipigania wakati wa kudai uhuru.
Lakini alikuwa na nafasi ya kugawa ardhi kwa wakulima weusi bila kusababisha kuporomoka kwa uchumi.
Kwanza nusu tu ya ardhi ambayo wakulima weupe walikuwa wakiilima na ambayo tayari walikubali kuitoa, wakulima weusi wasingeweza kuilima yote. Hata kiasi cha robo ya ardhi hiyo wasingweza kuilima, jambo hilo lilijulikana,.kwa hiyo Mugabe alishauriwa na watendaji wake kwa vile uchumi wa Zimbabwe ulitegemea pia wakulima wakubwa ambao wengi wao ni weupe,basi waendelee kuilima nusu ya ardhi na nusu ya ardhi wapewe wakulima weusi. Lakini Mugabe akakataa kwa kusikiliza makada wa chama chake ambao kumbe walikuwa na agenda ya kutaka mashamba yale.
Jambo la pili Mugabe akashindwa tena kuwazuia wakulima waliotaka kutoka na kutoa mapato yao yote. Alisema kama wanataka wanataka watoe cash yao waondoke, jambo liliporomosha uchumi wa Zimbabwe ghafla.a.
Utachukuliaje mfano wa china kwa maendeleo, nchi iliyokuwa inatengeneza baruti miaka elfu na elfu iliyopita na yenye ustaarabu uliotukuka kama kuwa na maandishi yake. Nchi iliyokuwa na tekinolojia ya kuchimba mifereji kuwezesha meli kupanda milimani (The Grand Canal) na yenye falsafa kebe kebe kama za Sun Tzu wakati huo wazungu walikuwa wanaishi mapangoni? Wewe unaiangalia China ya kina Mao, Jintao na Xi, mimi naongelea ile ya kian Qin Shi Huang.Kuna uzuri mmoja Mugabe kabla hajafa alikiri kukosea katika namna walivyogawa mashamba kwa kuwapa watu ambao waliyaua.
Tatizo letu sisi Waafrika kwa kila tunapokwama tunasingizia watu wengine.
Utasikia nchi zetu zimekuwa maskini kwa sababu ya ukoloni. Wasichokijua kuwa hata nchi nyingi zilitawaliwa lakini sasa hivi zimeshapiga hatua kubwa.
China imepata uhuru wake mwaka 1949 tu toka kwa Japan, na huku kupigwa vita na nchi za magharibi lakini leo ndiyo nchi namba 2 kiuchumi duniani.
Ni muda kwa nchi za Afrika kuwajibika kwa uongozi mbovu wanaoundekeza, na siyo kusingizia watu wengine