Nelson Mandela ni msaliti wa harakati za Uhuru wa Afrika Kusini na Afrika kiujumla?

Mkuu uchumi wa Africa umebaki unathibitiwa na mzungu
Mweusi ameendelea kuwa mkimbizi ndani ya nchi yake
Kwa kuwa aliamua kuwa soft kuhusu ubaguzi wa kaburu angepigania hata uchumi wa walio wengi
Kwa sasa bado Africa hatuna namna ya kujinasua. Athari za ukoloni zitaendelea kuvitafuna vizazi vyetu vijavyo.

Na huu ukoloni mamboleo ndo kabisa unazidi kuzididimiza nchi za Africa.

Wakati mwingine huwa nafikiri hatima ya Africa ilipangwa toka mwanzo.

Alichokifanya Mandela kwa nchi yake ya Africa Kusini ni hatima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1484014
Kwa takribani miaka 27 Nelson Mandela (Tata/Madiba) amekuwa gerezani Hadi mwaka 1990 alipoachiwa.

Hadi kufikia mwaka 1990 nchi zote za kiafrika zilikuwa zimepata Uhuru kutoka kwa wakoloni. Ikumbukwe Afrika Kusini ilipata Uhuru wake mnamo 1931, mwaka 1994 haukuwa mwaka wa kupata Uhuru kwa Afrika Kusini bali ilikuwa end of Apartheid.

Mchango wa Nelson Mandela kwenye harakati za kusaidia bara la Afrika kujikomboa Ni mdogo Sana. Ni tofauti sana na ule Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius .K. Nyerere aliyeifanya Tanzania kambi kuu ya wapigania uhuru Kama Robert Mugabe (Zimbabwe), Sam Nujoma (Namibia), Mozambique (Samora Machel, Eduardo Mondlane),Afrika Kusini yenyewe n.k
Katika Historia ya ukombozi wa Afrika mchango wa Nelson Mandela ni mdogo Sana.

1: Kipi kilichompelekea mpaka kupata tuzo ya amani ya Nobel?
2: Kipi kilicho pelekea kuonekana kiongozi mashuhuri na Bora kwa Afrika nzima?
3: Umaarufu wake umepikwa na wabepari?
4: kwa Nini sio J.K Nyerere na Ni Nelson Mandela?
5: Nyuma ya heshima ya kimataifa aliyopewa Nelson Mandela ni Nini?
6: Ni kweli Nelson Mandela aliingia makubaliano ya Uhuru kwa wa-afrika?
7: Toka mwisho wa Apartheid ni kipi kimebadilika kwa wa-afrika Kusini? Ardhi umerudi kwa wa-afrika Kusini? Serikali ya Afrika Kusini inayo kauli asilimia Mia juu ya ardhi yake?

Ni maswali ya kujiuliza sana na Ni maswali ya kupatia ufumbuzi.
Na hi ni tokana na mchango mdogo Sana wa Nelson Mandela hususa kwenye harakati za Afrika.

Mnamo mwaka 2009 umoja wa mataifa ulisimika tarehe 18 ya mwezi wa 7 kuwa sikukuu ya kimaitaifa ikiitwa Mandela day na ndio siku ya kuzaliwa kwa Mandela, kwa lengo la kumhenzi Mandela.
How Nelson Mandela betrayed us, says ex-wife Winnie
ww upo kamanda👊Yafanye hayo Aliyoshindwa Mandela bro! Yeye uwezo wake umeishia hapo!
 
Hata Mimi huwa najiuliza na kushangaa hili
Historia ya mapambano ya kudai haki na usawa katika Afrika ya kusini ni ndefu na yenye kona nyingi. Ikumbukwe kuwa Afrika ya kusini ilishapata uhuru wake mapema mwaka 1910. Kwa hiyo mapambano yenyewe yalikuwa ni ya kudai haki na usawa katika jamii kwa vile mfumo wa sheria,uchumi na biashara uliwapendelea wazungu. Mathalan, mtu mweusi hakutakiwa kisheria kuchukua mkopo mkubwa katika bank. Na kutokana na hilo, fursa kubwa za kibiashara kama tenda za ujenzi wa majengo na miundombinu hawakutakiwa kufanya. Hali hiyo iliwafanya Weupe katika Afrika kusini kuzidi kuwa matajiri kwa kupendelewa fursa nyingi za kiuchumi.
NELSON MANDELA alijiunga na chama cha ANC wakati tayari hicho chama lilishaanza mapambano miaka mingi nyuma kabla hata Mandela hajazaliwa. Msingi mkuu wa ANC ulikuwa ni kudai haki hizo ili jamii ya Afrika ya kusini iishi katika usawa. ANC walisema hawakuwa na agenda ya ubaguzi; lengo lilikuwa ni kupigania haki kwa watu wote bila kujali rangi zao. Kutokana na agenda hiyo hata watu wasio weusi kama jamii ya wahindi ambao nao walikuwa wakibaguliwa nao wakajiunga na harakati za kudai haki kwa WAZI. Lakini kuna kitu ambacho hakisemwi sana ambacho kwa watu ambao hawajazama sana katika mwenendo wa historia ya Afrika ya kusini wanaweza kushangaa endapo wakiambiwa ukweli kwamba walikuwapo pia wanaharakati weupe waliounga harakati za weusi kwa SIRI. Mathalan, makampuni ya Anglo Gold na hasa kampuni tanzu yake ya Debeers yalikuwa yakiiwezesha ANC kifedha kwa siri ili kukwepa adhabu toka serikalini.

Sasa nirudi katika hoja ya uzi uliotolewa unaouliza kama Nelson Mandela alikuwa msaliti.
Kutokana na mtiririko wa matukio Nelson Mandela hakuwahi kuwa msaliti wa harakati za kudai usawa kabla hajaenda jela, akiwa jela na baada ya kutoka jela. Alipokamatwa na kushtakiwa na baadaye kuhukumiwa, Mandela alikuwa na msimamo uleule. Ikumbukwe kwamba kosa ambalo yeye na wanaharakati wenzie walishtakiwa nalo ni TREASON,..shtaka la kufanya njama za kuipundua serikali, kosa ambalo adhabu yake ni kifo. Lakini alipopewa nafasi ya kujitetea, yeye ndiyo kwanza akatoa ile hotuba fupi maarufu sana hapo mahakamani akielezea malengo na mtazamo wa harakati zao,..akahitimisha kwa kusema kuwa kama kudai haki na usawa ndilo hilo analoshtakiwa na kuhukimiwa nalo yuko tayari kufa,."..IF NEEDS BE I'M READY TO DIE ".

Mandela alikataa hongo ya kutolewa jela kwa sharti la kwenda kuishi nje ya Afrika ya kusini na kupewa huduma zote za kianasa na makaburu. Kwa hlo hakuwasaliti wananchi kwa vile kwa kubaki kwake jela kukamfanya yeye kuwa nembo ya watu kudai haki, na watu ndani na nje ya Afrika ya kusini kuzidisha mapambano na msukumo wa kudai haki kwa serikali ya kibaguzi.

Msukumo dhidi ya makaburu ulipozidi,kulikuwa hakuna namna kwa makaburu,ikabidi wakubali kubadili sera za ubaguzi na kwa mantiki hiyo kuwaachia pia wafungwa wote wa kisiasa waliofungwa wakidai haki na usawa.
Kwa kufanya mabadiliko ya sera katika Afrika ya kusini kungemaanisha kuwa hata vyama vya siasa vingekuwa huru kushiriki katika uchaguzi. Katika hali hiyo ilishajulikana kuwa endapo Mandela angeachiwa, na ANC kushiriki uchaguzi huku Mandela akiwa mgombea wake, ANC ingeshinda uchaguzi kwa kishindo.
Katika hiyo hali kuna masuala kadhaa ilibidi yajulikane mapema,na hasa kuhusu aina ya sera ya kiuchumi ambayo serikali itakayoongozwa na ANC ingeendesha. Kwamba ingeendesha SERA YA KIUCHUMI WA KIBEPARI au SERA YA UCHUMI WA KIJAMAA? Serikali ya makaburu pamoja ba sekta binafsi, sekta binafsi iliyohusisha wafanyabiashara wakubwa kama vile wamiliki wa migodi walitaka kujua hatma yao itakavyokuwa baada ya kuingia serikali ya ANC. Kama ANC ingependa kufanya sera za kijamaa ingemaanisha kwamba njia kuu za kiuchumi pamoja na migodi,mashamba na viwanda vingetaifishwa toka sekta binafsi na kuwa katika umiliki wa serikali. Kwa hiyo ilikuwa muhimu kwa wafanyabiara wale ambao kihistoria walikuwa weupe kujua hatma yao; ANC iongoze nchi kijamaa, ili wao waondoke mapema au ANC iongoze kibepari au uchumi huria ili wao wabaki.

Ili kujua hilo ilibidi lazima vikao vya makubaliano kati ya wadau wote vifanyike mara kadhaa. Washiriki wa vikao walikuwa watendaji wa serikali ya makaburu na wafanyabiashara kwa upande mmoja na wawakilishi wa ANC kwa upande wa pili. Muwakilishi mkuu wa ANC alikuwa Mandela, upande wa sekta binafsi wawakilishi walikuwa akina William na Harry Oppenheimer wa kampuni ya Anglo Gold. Serkali iliwakilishwa na watendaji wa juu wakiongozwa na PW Botha ambaye alikuwa kiongozi wa nchi na vikao vilifanyika nyumbani kwake.

Ikumbukwe tena jambo la msingi, sera ya ujamaa haikuwa muundo wa ANC toka awali kwa hiyo kufikia makubaliano ya aina gani ya mfumo wa kiuchumi watatumia haikuwa suala la mjadala. ANC waliamini katika uchumi huria, ambao ni ubepari.
Akina Oppenheimer ambao walikuwa wakiisaidia ANC kifedha kwa siri walimkumbusha Mandela juu ya jitihada zao hizo katika vikao. Na Mandela aliwakumbusha ANC ilichokipigania toka mwanzo, kwamba hawawachukii weupe lakini wanapinga sera zinazowabagua weusi na kuwapendelea weupe. Kwa hiyo serikali ya ANC ikiingia madarakani itasimamia uchumi wa kibepari kama ilivyoamini lakini ingesimamia haki na usawa kama ilivyopigania toka mwanzo.

Chama ambacho kilikuwa nacho ni cha ukombozi katika Afrika ya kusini lakini chenye mlengo wa kikomunisti ni SACP ambacho kiongozi wake miaka ya tisini alkikuwa ni Chris Hani. Hiyo ina maana kuwa kama chama cha SACP kingeshika madaraka baada ya uchaguzi mwaka 1994 ,serikali yake ingeendesha sera za utaifishaji wa njia zote kuu za kiuchumi.

Baada ya Nelson Mandela na ANC kuingia madarakani waliendesha nchi kwa mfumo wa uchumi huria/ubepari, mfumo ambao upo hadi leo na ni mfumo ambao upo katika kila nchi duniani kwa sasa isipokuwa Cuba pekee.
Katika hali ya kuleta usawa kwa fursa hasa kwa weusi ili kufidia lile pengo la umaskini uliotengenezwa na miaka mingi ya unyanyaswaji, serikali ikaanzisha sera maalum (BLACK EMPOWERMENT)ya kuwawezesha weusi ili nao kuweza kufanya biashara kubwa ambazo awali hawakuruhisiwa kuzifanya.

Katika sera hiyo, weusi waliwezeshwa na kupewa upendeleo maalum na serikali ili waweze kufanya zile biashara na tenda kubwa ambazo awali hawakuruhusiwa kufanya na serikali ya makaburu. Sera hiyo maalum ya upendeleo ndiyo ikawatengeneza wafanyabiashara mabilionea wa mwanzo wa Afrika ya kusini kama akina Tokyo Sexhwale na Cyril Ramaphosa, rais wa sasa.

Kwa hiyo kabla ya kusema kwamba Nelson Mandela aliwasaliti weusi inabidi huo ukweli niliouleza hapo juu ujulikane na kuingia kwenye akili za watu kwanza.

Kuna baadhi ya watu ndani na nje ya Afrika ya kusini wanaamini kwamba Mandela baada ya kuingia madarakani alitakiwa ataifishe mashamba,migodi na biashara zote za weupe ili aonekane kwamba ameleta usawa.
Hoja hiyo ni dhaifu kwani sera kiuchumi ya ya ANC haikuwa katika utaifishaji toka mwanzo na hata sasa; Na kama Mandela angesimamia utaifishaji ,basi angekuwa anakiuka mtazamo na sera za chama chake.
Kuna hoja nyingine dhaifu inayosema kwamba Mandela aliwasaliti weusi kwa vile hadi anaondoka madarakani watu weusi bado wengi walikuwa maskini.
Ijulikane wazi kwamba pamoja na ukweli kwamba serikali ya Mandela ilianzisha sera maalum ya kuwezesha weusi, lakini mabadiliko ya kimaendeleo kwa weusi yasingeweza kuja kwa haraka ndani ya miaka mitano, huku ikizingatiwa kuwa hata hao weupe pamoja na kupewa upendeleo iliwachukua zaidi ya miaka 70 kuwa katika hali ya kiuchumi waliyokuwa nayo.

Upotofu huo wa kufikia waliokuwa nao weusi Afrika kusini, ulikuwapo pia kwa waafrika wakati nchi zao zikipata uhuru toka. Wao walidhani kwamba wakishapata uhuru tu, basi kila kitu kitakuwa kinatolewa bure na serikali. Julius Nyerere ilibidi awaamshe watu kwa kuwaambia UHURU NA KAZI..,ili wafanye kazi.
 
Bandiko bora kabisa.

Sawa, kwa Nini haheshimike Sana zaidi ya J.K Nyerere?
 
Kama Tanzania ingewekeza nguvu zake tangu mwanzo kujenga uchumi wake tungekuwa mbali sana. Hata Mwl. Nyerere wakati wa mwisho wa uhai wake aliangalia jinsi tulivyojifukarisha na nchi za kusini mwa Afrika na kufedheheka na kukata tamaa na yale aliyowafanyia nchi za kusini.

That is one the reasons why most of the people with the knowledge in Tanzania are happy to see JPM make changes in order to make sure that Tanzania is at per or above (economically) with most of our friends/enemies within the region and beyond.
 
Lenyewe swali hili gumu mbona!
Mwl Nyerere is African Hero aliruhusu WaTz waishi kwa shida kwa kusudi la kuikomboa Africa lakini sifa na utukufu huwa wanapewa wale waliofungwa magereza
Nampenda President Kaunda aliwaambia ukweli ' sifa zimwendee Mwl Nyerere katika ukombozi wa South Africa na Africa kwa ujumla'

Nelson Mandela bado ni African Hero maisha yake yote yalimalizikia gerezani kwa ajili ya mtu mweusi South Africa the rest ni history. Haikuwa rahisi!
 
Heshima na sifa alizonazo Ulimwenguni Nelson Mandela leo hii ni kwa sababu tu wazungu wameamua iwe hivyo kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe zaidi ,na si kwa sababu ya matendo yake ndani na nje ya Africa.

Kiukweli kabisa (sina nia ya kumkosea heshima kwa namba yoyote ile)Mandela hana lolote kubwa alilolifanya kwa ajili ya Africa ,au ndani ya SA kwenye zaidi ya kuwa mfungwa wa kisiasa kwa muda mrefu,nadhani watu kama S Biko,O Tambo,nk wamefanya harakati kubwa za ukombozi ndani ya SA kuliko hata Tata Madiba ila ndio hivyo tena Dunia ina wenyewe kwenye kufanya maamuzi.

Hivyo basi hakuna namna yoyote na kivyovyote unaweza kufananisha aliyoyafanya N Mandela na aliyofanya Mwalimu Nyerere katika nchi zao na Africa kwa ujumla.

Mandela hamfikii Mwalimu hata kidogo,basi tu Dunia ina inafiki sana hii.
 
Saa nyingine ukiona IQ ni ndogo ni bora usome tu sio lazima uchangie.Sasa unategemea system ya apartheid iliyoanza rasmi 1948 na imeota mizizi unategemea mandela angeing'oa kwa muda huo mfupi wa miaka 5 aliyokaa madarakani mpaka unamuita msaliti.Mambo si rahisi namna hiyo kama unavyodhani.Believe me or not japo systematized racial policies hazipo lakini ubaguzi bado unaexist kwenye jamii.Africans bado wanaangaliwa kwa jicho la tofauti na Afrikaners
 
huu Uzi utasababisha baba wa taifa aonekane wa kawaida Sana hata kwetu sisi wabongo wakati historia tuliyosoma mashuleni imemfanya Kama Mungu wa afrika.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Mimi mchonge nilishamtoa kwenye mashujaa kwa kitendo chake cha kukiri hadharani kwamba katiba yetu ikipata dikteta ataitumia vibaya lakin hapo hapo hakuona umhimu wa kuibadili ili iwe ya kidemokrasia!

kuanzia hapo, na alivoanza kulia lia miaka ya 90 ndio nikajua huyu mtu alikua mbinafsi pia, alipenda kuabudiwa!
 
Sawa, kwa Nini haheshimike Sana zaidi ya J.K Nyerere?
Suala la kwa nini Mandela kufahamika zaidi ya Julius Nyerere kimataifa ilitokana na sababu kama 2 hivi.

Kwanza ijulikane kwamba wanaharakati wa kudai haki na wanachama wa ANC na PAC waliofungwa na serikali ya makaburu walikuwa wengi, akina Walter Sisulu, Govan Mbeki, Ahmed Kathrada,Elias Mtsoaledi,Dennis Goldberg kwa kutaja wachache tu.
Wakati wa kelele za walifungwa kisiasa na makaburu zikifanywa ndani na nje ya Afrika ya kusini, waandamaji walikuwa wakibeba mabango yenye ujumbe na picha za wafungwa wote walio gerezani. Lakini ilikiwa Mandela ambaye hata katika kesi hiyo maarufu iliyoitwa RIVONIA, ndiye aliyekuwa na namna fulani kueleza hoja zake kiasi cha kuwavutia waandishi wa habari wakati wote. Na pale alipohitimisha kwa kugeuza ile fursa ya kujitetea na kuwa hotuba kwa kusema ikibidi kufa na afe lakini hatoacha kutetea haki , na maneno yake hayo kuwa katika vyombo vya habari vya nje ya Afrika ya kusini tayari watu wakamuona kama kiongozi japo hakuwa kiongozi.

Kisha kukawa na matukio ya Winnie Mandela. Mkewe Mandela, Winnie alikuwa mara nyingi akiingia katika mzozo na askari wa makaburu kwa kuvunja sheria za kihuni za kuingia mjini bila kibali au kulazimisha haki ya kwenda kumuona mumewe jela mara kwa mara huku akidai aambatane na mabinti zake wadogo . Kwa matukio yake hayo, akawa mara nyingi katika kurasa za magazeti ya ndani na nje ya Afrika ya kusini.
Waandishi hawakuacha kumfuatilia Winnie, aliyeonekana mrembo, mwenye watoto wawili ambaye mumewe amefungwa maisha huku akiachwa kama mjane vile akiwa bado kijana sana lakini mwenye nguvu ya kupambana kijasiri.

Mchanganyiko wa hayo mambo ukafanya watu wamtambue zaidi mumewe Nelson kuliko mfungwa yeyote mwingine hasa kwa nje ya Afrika.
Kwa hiyo mbiu ya kudai wafungwa wale waachiwe ikabebwa na jina la NELSON MANDELA NA WENZAKE WAACHIWE HURU . Bahati mbaya kutokana na sababu nilizosema, wenzake hao wakawa hawatajwi sana midomoni mwa watu japo waandishi wa habari walikuwa wakiandika habari zao. Kwa hiyo Brand ya kudai haki ikageuka na kuwa Nelson Mandela katika namna ileile Julius Nyerere aligeuka kuwa brand ya kudai uhuru japo yeye naye alikuwa na umri wa miaka 2 tu wakati chama kilichokuja kuizaa TANU, yaani African Association kilipoanzishwa na akina KLEIST SYKES na CECIL MATOLA. Hivi leo hii ukiwatajia vijana wa Kitanzania majina ya hawa watu na umuhimu wao wataelewa zaidi kuliko wanavyomuelewa Nyerere?
Kulikuwa na watu wengi nyuma ya pazia ambao walimfanya Julius Nyerere kama brand ya kudai uhuru wa Tanganyika kutokana na uwezo wake wa kujieleza na kuwasilisha mada husika.

Nyuma ya pazia la harakati za kudai haki kwa weusi wa Zimbabwe,Namibia na Afrika ya kusini, ambazo nje ya Afrika ya kusini ziliongozwa na jukwaa la NCHI ZLIZO MSTARI WA MBELE KATIKA UKOMBOZI WA NCHI ZILIZO KUSINI MWA AFRIKA, jukwaa ambalo lilikuwa chini ya uenyekiti wa Julius Nyerere nalo lilimfanya Mandela kuwa brand ya harakati zao. Na ndiyo maana katika hata katika nchi zetu hizi ambako harakati zilifabyika tulimjua Mandela zaidi kuliko wafungwa wenzie.

Kwa hiyo kwa serikali za magharibi walimjua Nyerere vizuri sana, na walijua kuwa ni mwerevu sana, na walijua pia nyuma ya pazia ndiye aliyekuwa akiongoza mapambano ya kudai haki kwa nchi za kusini.
Lakini Nyerere na wenzake akina Kenneth Kaunda hawakuwa maarufu kwa public ya magharibi kwa namna ile ile ambayo Kleist Sykes na Cecil Matola hawakuwa maarufu kwa Watanzania wengi lakini walijulikana kwa wakoloni

Sawa, kwa Nini haheshimike Sana zaidi ya J.K Nyerere?
 
Ukitaka kujua nchi inaendeshwa na nani nenda south ukajionee. kiukweli mtu mweusi hana chake .mpaka leo mtu mweusi bado anaitwa bobjan kwenye nchi yake .alafu kaburu alipoona anaachia madaraka kwa mtu mweusi .walichota ela nyingi wakawapa wazungu wenzao ili waendelee kua na power walichota Rand billion 500 .
 
It is not true that Mandela is overrated.

Issue ni kwamba hiyo ndiyo level yake. Hiyo league aliyopo inamfaa....... historia ya SA inambeba.
Kitu usichokijua ni kuwa uwepo wa wazungu SA ni alama ya white supremacy Afrika. Ndiyo maana walipata support kubwa ya nchi za magharibi, kiuchumi na hata kiulinzi.

Alichokipata Mugabe ni adhabu ya kuondoa alama hiyo ya white supremacy, Zimbabwe. Mandela hakuondoa alama hiyo SA, ndiyo maana wakamkweza. Kwa hiyo unaposema hiyo ni level yake ni sawa na kusema anapata heshima ya kuwa snitch.

Ukiangalia mlolongo wa viongozi, utaona wale wanaowarubuni waafrika wenzao huwa wanapata sifa na heshima za kijinga. Viongozi kama Mobutu walipata heshima za kinafiki kipindi chao wakati wale kama Nyerere na Sankara huwezi kusikia wakienziwa na nchi za magharibi. Sababu ikiwa, hawa walifanya jitihata za kuondoa white supremacy Afrika.
 
Katika sera hiyo, weusi waliwezeshwa na kupewa upendeleo maalum na serikali ili waweze kufanya zile biashara na tenda kubwa ambazo awali hawakuruhusiwa kufanya na serikali ya makaburu. Sera hiyo maalum ya upendeleo ndiyo ikawatengeneza wafanyabiashara mabilionea wa mwanzo wa Afrika ya kusini kama akina Tokyo Sexhwale na Cyril Ramaphosa, rais wa sasa.
Huoni hao wachache waliowezeshwa wamewekwa kama buffer zone ili kuendeza mfumo wa ukandamizaji wa walio wengi?
 
Kitu usichokijua ni kuwa uwepo wa wazungu SA ni alama ya white supremacy Afrika. Ndiyo maana walipata support kubwa na nchi za magharibi, kiuchumi na hata kiulinzi.

Alichokipata Mugabe ni adhabu ya kuondoa alama hiyo ya white supremacy, Zimbabwe. Mandela hakuondoa alama hiyo SA, ndiyo maana wakamkweza. Kwa hiyo unaposema hiyo ni level yake ni sawa na kusema anapata heshima ya kuwa snitch.

Viongozi wanaowarubuni waafrika wenzo huwa wanapata sifa na heshima za kijinga. Viongozi kama Mobutu walipata heshima za kinafiki kipindi chao wakati wale kama Nyerere na Sankara huwezi kusikia wakienziwa na nchi za magharibi. Sababu ikiwa, hawa walifanya jitihata za kuondoa white supremacy Afrika.
Mara kadhaa umezungumzia neno KUONDOA ALAMA YA WEUPE. Sijui una maanisha nini? Kama ukiwa mfuatiliaji wa siasa za kimataifa vizuri ungegundua kwamba hata Wakulima na Wenye migodi Afrika ya kusini walitaka kutoka kwa kutoa hela yao katika mabenki katika miaka ya karibuni baada ya kuona wakulima wa Zimbabwe wanaporwa mashamba. Serikali ya Afrika ya kusini iliwaambia wawekezaji weupe haitapora mashamba wala migodi yao. Lakini hawakuamini, bado wakataka kutoka Afrika ya kusini na kuhama na mtaji wao. Lakini walishindwa kuhamisha mtaji wao kutokana na sheria kali ya REPATRIATION OF CASH ya Afrika ya kusini na hiyo ndiyo sababu iliyofanya wabaki kwa lazima.
Katika sheria hiyo ambayo inamtaka mwekezaji au yeyote mwenye biashara atoe nje ya nchi asilimia 15 tu ya kiasi anachoingiza kwa mwaka na hivyo kufanya asilimia 85 ya mapato ya mtu huyo kubaki ndani. Hiyo inamaanisha kwamba hata kama unataka kuhamia nchi nyingine lakini huwezi kuhama na mapato yako ambayo umeyachumia Afrika ya kusini.

Hicho unachokisikia kuwa Johannesburg ilijengwa kwa dhahabu ya migodi ya Kimberley ni kweli. Lakini unachotakiwa kujua pia ni ukweli kwamba kasoro ya utawala wa serikali ya Afrika ya kusini ilikuwa ni ubaguzi wa rangi,..lakini katika maeneo mengine kama kusimamia sheria na uchumi wao walikuwa vizuri sana.
Watu waliowekeza katika migodi, baada ya kuuzwa kwa dhahabu na madini mengine, ukiacha masuala ya serikali kuwa na mrahaba na kuchukua kodi yake, lakini mmiliki wa mgodi alitakiwa kurudisha nyumbani Afrika ya kusini asilimia 85 ya mapato yake kwa mujibu wa sheria.
Wataalam wa kiuchumi wanasema ni bora hata serikali isichukue kodi toka kwa investors lakini ihakikishe kuwa asilimia 85 ya mapato yao yanabaki au kurudi nyumbani ndipo utaona faida ya uwekezaji.
Ukiacha Afrika ya kusini, nchi nyingine kusini mwa jangwa la Sahara ambayo iko makini katika kuhakikisha sheria ya kurudisha mapato ya uwekezaji nyumbani inasimamiwa vizuri ni Botswana.

Mugabe alikosea sana lazima ujue hilo. Alikuwa sahihi katika nia yake kugawa ardhi kwa wakulima wazawa weusi kwa sababu ilikuwa ni ardhi ndiyo hasa waliyoipigania wakati wa kudai uhuru.
Lakini alikuwa na nafasi ya kugawa ardhi kwa wakulima weusi bila kusababisha kuporomoka kwa uchumi.
Kwanza nusu tu ya ardhi ambayo wakulima weupe walikuwa wakiilima na ambayo tayari walikubali kuitoa, wakulima weusi wasingeweza kuilima yote. Hata kiasi cha robo ya ardhi hiyo wasingweza kuilima, jambo hilo lilijulikana,.kwa hiyo Mugabe alishauriwa na watendaji wake kwa vile uchumi wa Zimbabwe ulitegemea pia wakulima wakubwa ambao wengi wao ni weupe,basi waendelee kuilima nusu ya ardhi na nusu ya ardhi wapewe wakulima weusi. Lakini Mugabe akakataa kwa kusikiliza makada wa chama chake ambao kumbe walikuwa na agenda ya kutaka mashamba yale.
Jambo la pili Mugabe akashindwa tena kuwazuia wakulima waliotaka kutoka na kutoa mapato yao yote. Alisema kama wanataka wanataka watoe cash yao waondoke, jambo liliporomosha uchumi wa Zimbabwe ghafla.
Kuna uzuri mmoja Mugabe kabla hajafa alikiri kukosea katika namna walivyogawa mashamba kwa kuwapa watu ambao waliyaua.
Tatizo letu sisi Waafrika kwa kila tunapokwama tunasingizia watu wengine.
Utasikia nchi zetu zimekuwa maskini kwa sababu ya ukoloni. Wasichokijua kuwa hata nchi nyingi zilitawaliwa lakini sasa hivi zimeshapiga hatua kubwa.
China imepata uhuru wake mwaka 1949 tu toka kwa Japan, na huku kupigwa vita na nchi za magharibi lakini leo ndiyo nchi namba 2 kiuchumi duniani.
Ni muda kwa nchi za Afrika kuwajibika kwa uongozi mbovu wanaoundekeza, na siyo kusingizia watu wengine
 
Kitu usichokijua ni kuwa uwepo wa wazungu SA ni alama ya white supremacy Afrika. Ndiyo maana walipata support kubwa ya nchi za magharibi, kiuchumi na hata kiulinzi.

Alichokipata Mugabe ni adhabu ya kuondoa alama hiyo ya white supremacy, Zimbabwe. Mandela hakuondoa alama hiyo SA, ndiyo maana wakamkweza. Kwa hiyo unaposema hiyo ni level yake ni sawa na kusema anapata heshima ya kuwa snitch.

Ukiangalia mlolongo wa viongozi, utaona wale wanaowarubuni waafrika wenzo huwa wanapata sifa na heshima za kijinga. Viongozi kama Mobutu walipata heshima za kinafiki kipindi chao wakati wale kama Nyerere na Sankara huwezi kusikia wakienziwa na nchi za magharibi. Sababu ikiwa, hawa walifanya jitihata za kuondoa white supremacy Afrika.
Upo sahihi mkuu.... ila kusema kwangu hiyo ilikuwa league ya Mandela na historia kubwa ya taifa ka SA.

Huwezi ukaifananisha na Taifa lolote Africa hasa kwenye suala la ukoloni.

Ni kweli Mandela alipambwa na wazungu kwa alichokifanya. Inasemekana baada ya kutoka gerezani walimmonitor 24/7. Na akaenda kuishi nao kwa miezi kadhaa.

Wapinzani wa SA wanamchukulia kama kiongozi aliyeuza weusi kwa sababu ya uongozi ambao haukuwa na faida kwa wengi.

Ukiachilia yote hayo...Je ni kiongozi gani mwingine wa Afrika akiwepo Nyerere alipitia aliyoyapitia Mandela? Nyerere njia ilikuwa nyeupe pee. 27 jela sio suala la kubeza.

Ubaguzi uliokwepo kupungua kwa kiasi kilichopo sasa sio wa kubezwa. Nitabaki kusema Mandela sio overrated.
 
Mandela alikuwa mpole mno ndio maana wazungu walimfunga miaka 27 ili kumpooza machungu wakampa hako katuzo ka Nobel
 
Huoni hao wachache waliowezeshwa wamewekwa kama buffer zone ili kuendeza mfumo wa ukandamizaji wa walio wengi?
Kwani unafikiri pia kwamba hata wakati wa utawala wa weupe, basi weupe wote walikuwa matajiri? Usichokielewa ni nini? Nimesema kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi watu weusi na wahindi hawakuruhusiwa kukopa kiasi kikubwa katika mabenki na hivyo kukosa fursa ya kunya biashara kubwa, sasa baada ya ANC kuingia madarakani walipata fursa hiyo na hivyo akina Ramaphosa na Sexwhale kuwa watu wa mwanzo kunufaika na uhuru huo,..hilo nalo gumu kuelewa? Au ulitaka watu weusi wote wapate fursa hiyo kwa maana kwamba wote wawe mabilionea,..hiyo inaingia akilini?
IQ zenu zikoje kiasi cha kushindwa kutafakari mambo madogo kiasi hicho?
 
Usichokielewa ni kitu kinachoitwa systematic racism, huu ni mfumo unaozuia kundi fulani la watu kutoka hali ya chini ya maisha kwenda nyingine. Wewe unasifia uhuru wa mtu mmoja mmoja kama Ramaphosa, ambaye ni rahisi kurubuni, mimi naongelea kuwezesha angalau 40% ya raia weusi. Na hapa siongelei kukopa mamilioni ya pesa bali kuwapatia vitu vya msingi kama elimu, makazi bora na mifumo ya kusaidia jamii hizo kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Makaburu waliwezeshana kama kundi (group economics) wakati wa ubaguzi, siyo wote walikuwa matajiri lakini wengi walipata elimu na kuweza kupata ajira nzuri na wengine kukopa fedha za kuanzisha biashara. Na hii kama fungu moja la watu waliweza kurithisha utajiri kizazi kimoja mpaka kingine. Pesa za kina Ramaphosa sana sana zitasaidia familia na watu wachache waliokaribu lakini haita wasaidia waafrika wengi wa nchi hiyo.
 
Back
Top Bottom