Nelson Mandela ni msaliti wa harakati za Uhuru wa Afrika Kusini na Afrika kiujumla?

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
1,000
Betrayal_of_African_Revolution-back-page-1-1.jpg

Kwa takribani miaka 27 Nelson Mandela (Tata/Madiba) amekuwa gerezani Hadi mwaka 1990 alipoachiwa.

Hadi kufikia mwaka 1990 nchi zote za kiafrika zilikuwa zimepata Uhuru kutoka kwa wakoloni. Ikumbukwe Afrika Kusini ilipata Uhuru wake mnamo 1931, mwaka 1994 haukuwa mwaka wa kupata Uhuru kwa Afrika Kusini bali ilikuwa end of Apartheid.

Mchango wa Nelson Mandela kwenye harakati za kusaidia bara la Afrika kujikomboa Ni mdogo Sana. Ni tofauti sana na ule Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius .K. Nyerere aliyeifanya Tanzania kambi kuu ya wapigania uhuru Kama Robert Mugabe (Zimbabwe), Sam Nujoma (Namibia), Mozambique (Samora Machel, Eduardo Mondlane),Afrika Kusini yenyewe n.k
Katika Historia ya ukombozi wa Afrika mchango wa Nelson Mandela ni mdogo Sana.

1: Kipi kilichompelekea mpaka kupata tuzo ya amani ya Nobel?
2: Kipi kilicho pelekea kuonekana kiongozi mashuhuri na Bora kwa Afrika nzima?
3: Umaarufu wake umepikwa na wabepari?
4: kwa Nini sio J.K Nyerere na Ni Nelson Mandela?
5: Nyuma ya heshima ya kimataifa aliyopewa Nelson Mandela ni Nini?
6: Ni kweli Nelson Mandela aliingia makubaliano ya Uhuru kwa wa-afrika?
7: Toka mwisho wa Apartheid ni kipi kimebadilika kwa wa-afrika Kusini? Ardhi umerudi kwa wa-afrika Kusini? Serikali ya Afrika Kusini inayo kauli asilimia Mia juu ya ardhi yake?

Ni maswali ya kujiuliza sana na Ni maswali ya kupatia ufumbuzi.
Na hi ni tokana na mchango mdogo Sana wa Nelson Mandela hususa kwenye harakati za Afrika.

Mnamo mwaka 2009 umoja wa mataifa ulisimika tarehe 18 ya mwezi wa 7 kuwa sikukuu ya kimaitaifa ikiitwa Mandela day na ndio siku ya kuzaliwa kwa Mandela, kwa lengo la kumhenzi Mandela.
How Nelson Mandela betrayed us, says ex-wife Winnie
 
Mshumaa_Tz

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
684
1,000
Kwa takribani miaka 27 Nelson Mandela (Tata/Madiba) amekuwa gerezani Hadi mwaka 1990 alipoachiwa.
Hadi kufikia mwaka 1990 nchi zote za kiafrika zilikuwa zimepata Uhuru kutoka kwa wakoloni. Ikumbukwe Afrika Kusini ilipata Uhuru wake mnamo 1931, mwaka 1994 haukuwa mwaka wa kupata Uhuru kwa Afrika Kusini bali ilikuwa end of Apartheid.

Mchango wa Nelson Mandela kwenye harakati za kusaidia bara la Afrika kujikomboa Ni mdogo Sana. Ni tofauti sana na ule Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius .K. Nyerere aliyeifanya Tanzania kambi kuu ya wapigania uhuru Kama Robert Mugabe (Zimbabwe), Sam Nujoma (Namibia), Mozambique (Samora Machel, Eduardo Mondlane),Afrika Kusini yenyewe n.k
Katika Historia ya ukombozi wa Afrika mchango wa Nelson Mandela ni mdogo Sana.

1: Kipi kilichompelekea mpaka kupata tuzo ya amani ya Nobel?
2: Kipi kilicho pelekea kuonekana kiongozi mashuhuri na Bora kwa Afrika nzima?
3: Umaarufu wake umepikwa na wabepari?
4: kwa Nini sio J.K Nyerere na Ni Nelson Mandela?
5: Nyuma ya heshima ya kimataifa aliyopewa Nelson Mandela ni Nini?
6: Ni kweli Nelson Mandela aliingia makubaliano ya Uhuru kwa wa-afrika?
7: Toka mwisho wa Apartheid ni kipi kimebadilika kwa wa-afrika Kusini? Ardhi umerudi kwa wa-afrika Kusini? Serikali ya Afrika Kusini inayo kauli asilimia Mia juu ya ardhi yake?

Ni maswali ya kujiuliza sana na Ni maswali ya kupatia ufumbuzi.
Na hi ni tokana na mchango mdogo Sana wa Nelson Mandela hususa kwenye harakati za Afrika.
Mnamo mwaka 2009 umoja wa mataifa ulisimika tarehe 18 ya mwezi wa 7 kuwa sikukuu ya kimaitaifa ikiitwa Mandela day na ndio siku ya kuzaliwa kwa Mandela, kwa lengo la kumhenzi Mandela.South Africa ilipata Uhuru wake 1910 (Minority rule na 1994 wakapata majority rule)

Mandela huwezi mfananisha na Nyerere dictator aliyekuwa anawatesa watu waliomkosoa, kuwafunga na kuwapoteza Mfano Jumbe ,Hance pope nk.
 
WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
1,000
South Africa ilipata Uhuru wake 1910 (Minority rule na 1994 wakapata majority rule)

Mandela huwezi mfananisha na Nyerere dictator aliyekuwa anawatesa watu waliomkosoa, kuwafunga na kuwapoteza Mfano Jumbe ,Hance pope nk.

Swala si tabia za uongozi wa Nyerere Bali mchango wake katika bara la Afrika, hata Mandela kwenye serikali yake ya 1995-2000 palikuwepo na Mambo mengi tu Kama ufisadi, Rushwa n.k
 
Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,238
2,000
Kwa sababu ndogo ndogo tu za kawaida...

Afrika kusini ni taifa lenye historia kubwa saana kwenye kila kitu ukilinganisha na Tanzania. Ukitaka kulijua hili...Kwa mwaka SA inatembelewa na watalii kutoka mataifa ya kimagharibi sio chini ya milioni 10.

Utaifa tu ulimbeba Mandela.

Ubaguzi wa rangi ilikuwa habari kubwa ya moto kwa kipindi hicho. Hata kina Nyerere ukifuatilia mahojiano yao kuhusu ubaguzi wa rangi centre ya mazungumzo yao ilikuwa kuirejelea South Africa.

Kwenye masanamu ya mashujaa ya Africa kusini waliyoyajenga hata Nyerere hayupo....kwa ufahamu wangu hawauchukulii mchango wake kiutofauti kiviile kwao Nyerere ni kama Kaunda, Samora na Khama tu.
 
Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,238
2,000
Mtoa hoja ameeleza Jinsi gani Nyerere alivyo zaidi ya Mandela.Tuambie wewe Mandela ana kitu gani kikubwa kumzidi Nyerere zaidi ya kufungwa jela na kuwasamehe Wazungu.
Mimi sipo kwenye huu uzi kuwalinganisha Nyerere na Mandela.

Nasema tu yaliyomfanya Mandela kwa urahisi akajibebea kombe.

Ni attention ya Dunia kwa South Africa.

Ubaguzi wa rangi ilikuwa habari kubwa saana. Kuumaliza mgogoro na kushawishi makaburu kufanya mazungumzo ya amani ilishindikana kwa miaka mingi. Hatimaye wakakubali wakakaa meza moja.

Nyerere alistahili Nobel ya amani kwa sababu ipi? Tanganyika ilikuwa na misukosuko gani?

Wengi tunasema kuisaidia Afrika...lakini kiuhalisia usiende hata Ulaya nenda hizo nchi za Afrika kama wanamhesabu kama mmoja wa viongozi walioipigania Afrika.

Hapo tu SA ukienda wamejenga masaanamu ya mashujaa yao. Kwa historia tuliyoisoma Tanzania nilidhani Sanamu la Nyerere lingekuwepo ila halipo...la Fidel lipo...Chegu lipo...Selasie lipo.

Hii inatuonyesha ni kwa jinsi gani mchango wa Nyerere ulikuwa wa kawaida tu kama wa kina Mugabe na kina Kaunda.
 
Antetokounmpo

JF-Expert Member
Feb 5, 2020
633

Samahan mkuu,Nimesikia AU wanataka kujenga sanamu la Nyerere....Hivi Mandela Ameshajengewa sanamu Hapo Makao makuu ya AU ????
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom