Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
BODI ya wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL) imetangaza kujiuzulu kwa mwenyekiti wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) Nehemia Mchechu kuanzia Jumatano ya wiki hii.
Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa EABL wenye hisa Serengeti Breweries Ltd, Charles Munene ilisema kuwa Mchechu alijiuzulu wadhifa wake kuanzia tarehe 6 mwezi huu na anaendelea na majukumu mengine binafsi.
Ilisema kuwa wakati wa uongozi wake, Mchechu ambaye pia alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba nchini (NHC) alijitahidi kutumia uzoefu wake wa uongozi kuipeleka mbali kiwanda hicho.
Iliongeza kuwa mwenyekiti huyo ambaye aliyeteuliwa mwaka 2014 alifanikiwa kuimarisha uhusiano na utendeaji wa kiwanda baina na wadau
Awali iliripotiwa kuwa uteuzi wa Mchechu ulifuatia ukamilisho wa umiliki wa Jaji (mstaafu) Mark Bomani. Katika nafasi yake mpya, Bw Mchechu pia alikuwa mwanachama wa bodi ya kampuni ya bia ya East Africa.
Mbali na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Mchechu ambaye ana uzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .