Nehemiah Kyando Mchechu, ajiuzulu ujumbe wa Bodi EABL

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
image.jpg

BODI ya wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL) imetangaza kujiuzulu kwa mwenyekiti wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) Nehemia Mchechu kuanzia Jumatano ya wiki hii.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa EABL wenye hisa Serengeti Breweries Ltd, Charles Munene ilisema kuwa Mchechu alijiuzulu wadhifa wake kuanzia tarehe 6 mwezi huu na anaendelea na majukumu mengine binafsi.

Ilisema kuwa wakati wa uongozi wake, Mchechu ambaye pia alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba nchini (NHC) alijitahidi kutumia uzoefu wake wa uongozi kuipeleka mbali kiwanda hicho.

Iliongeza kuwa mwenyekiti huyo ambaye aliyeteuliwa mwaka 2014 alifanikiwa kuimarisha uhusiano na utendeaji wa kiwanda baina na wadau

Awali iliripotiwa kuwa uteuzi wa Mchechu ulifuatia ukamilisho wa umiliki wa Jaji (mstaafu) Mark Bomani. Katika nafasi yake mpya, Bw Mchechu pia alikuwa mwanachama wa bodi ya kampuni ya bia ya East Africa.

Mbali na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Mchechu ambaye ana uzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .
 

Attachments

  • eabl-ltd--resignation-of-a-director.pdf
    3.4 MB · Views: 46
Lete full story mkuu. Jamaa hasa tatizo ni nini??
Conflict of Interest, Ina maana ndefu kwa ufupi pale unapotumia Personal company na kupata tenda kwenye shirika unaloongoza mwenyewe, madhara yake

1.Miradi mingi bei walioverstate ili kampuni binafsi zipate pesa nyingi

2.personel company inanunua maeneo kwanza halafu unaliuzia shirika unaloendesha mwenyewe kwa bei kubwa
 
bado haikupi haki ya kumuona kuwa ni mkosaji kuliko wewe, soma tena nilichoandika. Mbona aliyewapiga 1.5T hamumsemi na kila siku yuko makanisani akitaka kuombewa
Soma uzi wa zitto ameupandisha jana, Tatizo husomi unasubiri tukusimulie ameiba au amefanya nini? Soma
 
ndugu usishangae ni kawaida ya maskini kushangilia pale anapoona tajiri kayumba kidogo, hajui kuwa hata kama mchechu kaacha ujumbe wa bodi bado maisha yake yatakuwa ya hali ya juu tu kwani kashajiwekeza

Maisha yatakuwa ya hali juu wakati ana wasiwasi wa kufikishwa mbele ya sheria muda wowote?Hakuna maisha ya taabu duniani kama kuishi kwa WASIWASI wa kutojua nini kinafuatia kutokana na UOVU,UBADHIRIFU, DHULUMA, WIZI uliofanya !! huyo uliye mtaja na yule mwingine MNDOLWA hawana amani !!!
 
Mungu awe naye daima, wote wakosaji katenda mema mengi
Alijengea mawe shirika, kodi za wananchi yeye alipewa fursa asimamie Kama tulivyompa fursa Mbalawa waziri kusimamia Stigler's gorge na flyover, Kama anatumia kampuni zake za mfukoni kujenga flyover tutamjadili tu si ni kodi zetu au?
 
waafrica kazi tunafanya sana tu... shida ni wizi..

mtu kama mchechu hakuwa na sababu ya kuipa tenda kampuni yake.. ukitaka kula na kipofu.. usimshike mkono

unaongea na muhindi au mchina au mkenya..au raia yoyote wa nchi nyingine.. unampa matenda yeye... mgao wako anakuwekea huko huko majuu... sasa wewe unaipa tenda kampuni yakk.. au mkeo au mwanao.. why usishtukiwe

Chuki mbaya.. Napita tu mwanawani
Ila ungejua Mchechu.. Alikoitoa NHC... Ungemtukuza Mungu Kwa hilo..kwamba tunao watanzania wanaweza kuzisimamia Mali zetu Kwa ufanisi.. Hili la kuondolewa Mchechu NHC. ..lina mengi ndani ila time will tell
 
Wabongo kwa ku pretend hatujambo. Hivi ni nani ambaye angepewa nafasi kama aliyokuwa kapewa mchechu na a sipige ulaji? Kwa miaka ya leo hii yupo?

Chuki tu na ubinafsi na roho mbaya. Kujiona malaika kumbe mbwembwe tu, useless kabisa
 
Chuki zinakusaidia nini? Umasikini ni mzigo mzito, hasa umasikini wa fikra
Yani kuna watu akili zenu zinashangaza sana!

Mtu ameweka ukweli kuhusu ubadhirifu ambao Mchechu amefanya NHC halafu anajitokeza mtu bila kujua kinachozungumzwa anaropoka tu "eti umaskini!".

Kwahiyo ulitaka wote hapa tuchekelee tu kupigwa? Kama kwako unaona sawa basi endelea kumshabikia huyo mwizi ila wengine hatukubali kupigwa kiboya boya tu.
 
Wabongo kwa ku pretend hatujambo. Hivi ni nani ambaye angepewa nafasi kama aliyokuwa kapewa mchechu na a sipige ulaji? Kwa miaka ya leo hii yupo?

Chuki tu na ubinafsi na roho mbaya. Kujiona malaika kumbe mbwembwe tu, useless kabisa

Sasa usilalamike pale nchi isipoendelea...Kula unakula lakini wee Wala mpaka watu wanastuka.
Mie alichoniboa huyu jamaa ni kusema eti low cost housing haiwezekani....
 
Back
Top Bottom