NEC yasema haitatumia Wakurugenzi kusimamia uchaguzi Tanzania

Mh, hapo umekosea. Kaijage amefanya madudu mengi kuiangamiza CUF ya Maalim,as if siyo jaji, leo unasema majaji wa zamani ni wazuri, hapana! HAPANA SIYO KAIJAGE NSHOMILE!
Tofautisha mwenyekiti wa NEC na msajili wa vyama vya siasa, Kaijage na Mtungi different spicie mkuu.
 
Sasa Attorney General wetu alikuwa anaongea nini siku ile? Si alisema wakionyesha nia tu, uamuzi wa mahakama unasimama? Sasa huyu anawashwa nini?
 
Sasa badala watu waishukuru mahakama, wanaanza kutanguliza uoga

Hapa tunawapa point ma fifi_m kushinda

Tunapaswa kuamini maamuzi ni ya mahakama na Nec wametekeeleza, sasa badala ya kujikita kwenye ushindi na tuchukue hatua, sisi ndio tunashangaa kama vile tuliomba kisichowezekana
 
Ni upinzani kukaa China na kuangalia ni wapi tena panawakwamisha ktk uchaguzi .

Upinzani kuanzia sasa unatakiwa kujua kama wakurugenzi hawatatumiwa je Tume imejipanga kuwatumia akina nani ktk hizi chaguzi zilizopo mbele yetu.

Na hao watakaotumika wanapatikana vipi kwani wapinzani wanatakiwa haya wayajue mapema ndani ya hii miezi sio kukaa ofisini then baada ya uchaguzi wanakuja kulilia tena.

Waibane tume mapema kabla uchaguzi ili wanaingia ktk uchaguzi wakitegemea nini baada ya uchaguzi
 
NEC YASEMA HAITATUMIA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI TANZANIA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeweka wazi kuwa vifungu vya sheria ya uchaguzi vilivyopingwa, kutenguliwa na kuharamishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania havitatumika kwenye utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo katika uchaguzi.

Vifungu hivyo ni kifungu cha 7(1) na 7(3) vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi. Vifungu hivyo vinawataja wakurugenzi wa jiji, wakurugenzi wa manispaa, wakurugenzi wa miji na wakurugenzi wa wilaya (DED) kwamba wanaweza kuteuliwa na tume kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Akizungumza wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage alisema wanazingatia maelekezo ya Mahakama hivyo NEC haitotumia vifungu hivyo vilivyotenguliwa.

Jaji Kaijage aliyasema hayo wakati akijibu swali la mhariri wa gazeti la The Citizen Damas Kanyabwoya aliyetaka kufahamu kama Nec itaendelea kuwatumia wakurugenzi baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

“Mahakama ilitimiza wajibu wake ikavitengua baadhi ya vifungu vya sheria vilivyolalamikiwa. Niwahakikishie kuwa vile vifungu vilivyolalamikiwa hatutavitumia katika utekelezaji wa majukumu yetu. Kifungu cha 7 (1) na 7(3) cha sheria ya taifa ya uchaguzi ndivyo vilivyotenguliwa, vingine havijalalamikiwa.”

Hatua ya Mahakama Kuu kutengua Wakurugenzi wa majiji, manispaa, halmashauri, miji na Wilaya (DED) ilifikiwa baada ya mwanaharakati Bob Chacha Wangwe kufungua shauri Mahakama Kuu kupinga Wakurugenzi hao kusimamia uchaguzi, shauri ambalo lilisimamiwa na Wakili Msomi Fatma Karume.

Je unaikumbuka kauli ipi ya Rais Magufuli dhidi ya Wakurugenzi na Uchaguzi?

Kesho ni nzuri kuliko jana. Jiandikishe, Piga Kura, linda Kura.

Nini maoni yako?

#MwagaPombe2020
#HabarizaChadema

1132240
 
Nimekuajiri mimi, mshahara ninakupa pamoja na gari na mafuta, alafu unamtangaza mpinazani ni mshindi, jua huna kazi.
 
Badala ya hao ni nani watakaosimamia au hakuliweka wazi isijekuwa wameshapata watu wengine ambao nao watakuwa kwa manufaa ya watawala

Ila so far ni hatua nzuri hiyo kuwaondoa hao jamaa maana walikuwa wanavuruga sana matokeo sasa watulie wapige kazi maana wengi waliteuliwa kwa ajili ya uchaguzi

Hongera sana Bob Wangwe kwa kuitumia vyema taaluma yako
 
Na hawapaswi kuwatumia. Si hiari, ni lazima. OLE WAO.

Tatizo ni hakuna muongozo wa wazi... Je, wakitolewa wakurugenzi akina nani watasimamia..?
Mi natamani itamkwe kuwa wanasiasa, watumishi wa umma ama wateule wa rais hawatakiwi kusimamia uchaguzi wowote ndani ya mipaka ya nchi ya Tanzania.
 
Badala ya hao ni nani watakaosimamia au hakuliweka wazi isijekuwa wameshapata watu wengine ambao nao watakuwa kwa manufaa ya watawala

Ila so far ni hatua nzuri hiyo kuwaondoa hao jamaa maana walikuwa wanavuruga sana matokeo sasa watulie wapige kazi maana wengi waliteuliwa kwa ajili ya uchaguzi

Hongera sana Bob Wangwe kwa kuitumia vyema taaluma yako
Alijibu alicho ulizwa nadhama. Kama angeulizwa nani sasa watasimamia badala ya wakurugenzi, bila shaka angejibu pia.
 
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeweka wazi kuwa vifungu vya sheria ya uchaguzi vilivyolalamikiwa na kutenguliwa na mahakama havitatumika kwenye utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.

Vifungu hivyo ni kifungu cha 7(1) na 7(3) vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi. Vifungu hivyo vinawataja wakurugenzi wa jiji, wakurugenzi wa manispaa, wakurugenzi wa miji na wakurugenzi wa wilaya (DED) kwamba wanaweza kuteuliwa na tume kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma;

Tatizo ni hakuna muongozo wa wazi...
Je, wakitolewa wakurugenzi akina nani watasimamia..?
Mi natamani itamkwe kuwa wanasiasa, watumishi wa umma ama wateule wa rais hawatakiwi kusimamia uchaguzi wowote ndani ya mipaka ya nchi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom