Prof. Kabudi: Kwa sasa Wananchi hawatapewa dawa za kukabiliana na Corona kutoka Madagascar, inafanyiwa utafiti kwanza

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,744
2,000
1589086989903.png

Tumerudi kutoka Madagascar jana usiku ila hatujaja na dawa ya kuanza kugawa leo, tumekuja na dawa za kuanza utafiti na uchambuzi maabara, nimepokea simu nyingi, meseji WhatsApp Watu wanataka niwagaie, jamani sina dawa, sijaja na chupa za dawa”- Waziri Kabudi

“Chupa tumepewa mbili tu (control) ambazo zitasaidia pale Wataalamu watakapochanganya dawa na kufanya utafiti na uchambuzi ili waone kama wamepatia, tumepewa wastani wa box 3 za dawa itakayotumika kama tiba na Box 8 za dawa itakayotumika kama kinga pale utafiti ukikamilika”-Waziri Kabudi

“Madagascar wameijaribu wakajiridhisha kwamba ni salama ndio maana wanaitumia lakini sisi lazima tuifanyie utafiti na tujiridhishe kuwa inafaa,Ndege ya Rais haiwezi kuja na mzigo wa kutosha kugaiwa kwa Watanzania wote,Nchi yoyote ikituita kwamba ina dawa tutaenda kuchukua”-

Pia Prof Kabudi amesema "“Kile sio kikombe cha Babu, hatukwenda kuchukua kikombe cha Babu ile ni dawa ya kisayansi, ndio maana tumeenda na Wataalamu, mimi peke yangu kwakuwa ni Waziri nimepata bahati ya kugonga ile dawa, ila zile chupa tumekuja nazo 2 tu za kusaidia utafiti na nyingine (sio chupa) zipo kwenye Box, kwa sasa hatuna dawa za kugawa ni za utafiti”- Waziri Kabudi

“Watu waendelee kuchukua tahadhari hata kama tunaona hizi juhudi za uwepo wa matumaini ya dawa, lakini tuchukue tahadhari, hata sisi kwenye Ndege ya Rais tulikaa mbalimbali na tumevaa mask” Ameeleza waziri Kabudi!

========

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa dawa za kukabiliana na virusi vya corona ambazo Tanzania imepokea kutoka nchini Madagascar hazitogawiwa kwa wananchi kwa sasa.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa dawa hizo hapa nchini, Prof. Palamagamba kabudi amebainisha kuwa dawa hizo zitafanyiwa utafiti kwanza, na zitakapothibitika kuwa zina faa, ndipo wananchi wataanza kutumia.

“Dawa hii tumepewa na Madagascar ili tuje tuifanyie utafiti kabla ya kuitumia. Tungekuwa tumeenda kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania wote tungeenda na Bombardier au Airbus, lakini tulienda na ndege ya Rais. Na ieleweka hatukwenda kuchukua kikombe cha babu,” amesema Kabudi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa katika uchunguzi utakaofanyika, watalaangalia kama dawa hiyo ni salama kutumiwa, na pia ubora wake katika kupambana na corona.

Ameongeza kuwa nchini Madagascar tayari wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa dawa hiyo inafaa ndio maana wameanza kutumia.

Pia amesisitiza kwa mara nyingine kwamba ieleweke kwamba dawa hiyo haikuletwa kwa ajili ya kugawiwa kwa watu.

TBC
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,812
2,000
“Tumerudi kutoka Madagascar jana usiku ila hatujaja na dawa ya kuanza kugawa leo, tumekuja na dawa za kuanza utafiti na uchambuzi maabara, nimepokea simu nyingi, meseji WhatsApp Watu wanataka niwagaie, jamani sina dawa, sijaja na chupa za dawa”- Waziri Kabudi

“Chupa tumepewa mbili tu (control) ambazo zitasaidia pale Wataalamu watakapochanganya dawa na kufanya utafiti na uchambuzi ili waone kama wamepatia, tumepewa wastani wa box 3 za dawa itakayotumika kama tiba na Box 8 za dawa itakayotumika kama kinga pale utafiti ukikamilika”-Waziri Kabudi

“Madagascar wameijaribu wakajiridhisha kwamba ni salama ndio maana wanaitumia lakini sisi lazima tuifanyie utafiti na tujiridhishe kuwa inafaa,Ndege ya Rais haiwezi kuja na mzigo wa kutosha kugaiwa kwa Watanzania wote,Nchi yoyote ikituita kwamba ina dawa tutaenda kuchukua”-

Pia Prof Kabudi amesema "“Kile sio kikombe cha Babu, hatukwenda kuchukua kikombe cha Babu ile ni dawa ya kisayansi, ndio maana tumeenda na Wataalamu, mimi peke yangu kwakuwa ni Waziri nimepata bahati ya kugonga ile dawa, ila zile chupa tumekuja nazo 2 tu za kusaidia utafiti na nyingine (sio chupa) zipo kwenye Box, kwa sasa hatuna dawa za kugawa ni za utafiti”- Waziri Kabudi

“Watu waendelee kuchukua tahadhari hata kama tunaona hizi juhudi za uwepo wa matumaini ya dawa, lakini tuchukue tahadhari, hata sisi kwenye Ndege ya Rais tulikaa mbalimbali na tumevaa mask” Ameeleza waziri Kabudi!

Sent from my iPhone using JamiiForums

========

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa dawa za kukabiliana na virusi vya corona ambazo Tanzania imepokea kutoka nchini Madagascar hazitogawiwa kwa wananchi kwa sasa.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa dawa hizo hapa nchini, Prof. Palamagamba kabudi amebainisha kuwa dawa hizo zitafanyiwa utafiti kwanza, na zitakapothibitika kuwa zina faa, ndipo wananchi wataanza kutumia.

“Dawa hii tumepewa na Madagascar ili tuje tuifanyie utafiti kabla ya kuitumia. Tungekuwa tumeenda kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania wote tungeenda na Bombardier au Airbus, lakini tulienda na ndege ya Rais. Na ieleweka hatukwenda kuchukua kikombe cha babu,” amesema Kabudi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa katika uchunguzi utakaofanyika, watalaangalia kama dawa hiyo ni salama kutumiwa, na pia ubora wake katika kupambana na corona.

Ameongeza kuwa nchini Madagascar tayari wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa dawa hiyo inafaa ndio maana wameanza kutumia.

Pia amesisitiza kwa mara nyingine kwamba ieleweke kwamba dawa hiyo haikuletwa kwa ajili ya kugawiwa kwa watu.

TBC
 
Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,862
2,000
Yaani kuna muda unashindwa elewa watanzania tunataka nini, ni ujanja lawama, ujuaji, ukosiaji

Korona ipo chukua tahadhari

It is never too late to begin. Start now
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom