KERO Wakusanya tozo za pikipiki Daraja la Kigamboni (Dar) hawatoi risiti, fedha wanachukua wao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2024-02-09_13-30-06.jpg

photo_2024-02-09_13-30-08.jpg
Kuna mambo ya hovyo yanafanyika kwa wakusanyaji wa ‘gate collection’ upande wa pikipiki katika Daraja la Kigamboni (Dar es Salaam), wanachokifanya hawatoi risiti halafu fedha za malipo zinazotozwa wanazichukua wao.

Nimeshuhudia hilo jambo likifanyika mara nyingi tu kwa kuwa hiyo ni njia yangu.

Kinachotokea majira ya asubuhi ambapo kuna msongamano wa magari mengi hawafanyi huo mchezo, nilichobaini ni kuwa wanakuwa na hofu ya kwamba wakifanya hayo watabainika kwa sababu wanaopita mida hiyo ni watu wengi na wanaweza kuwemo wenye mamlaka, hivyo ikawa kwao.

Mara nyingi, majira ya mchana walinzi wa kwenye kizuizi hicho wanafanya majukumu yao kama kawaida kisha wakiona pametulia yaani hakuna purukushani nyingi za mpishano wa vyombo vya moto, wale wanaopokea hela na kutoa risiti wanajifanya kuingia ndani kwenye ofisi zao, wanabaki walinzi kadhaa kwa nje ambao wanasimamia upande wa Bodaboda.

Kila Bodaboda anayepita anatoa Shilingi 300 au 200 kwa kuwakabidhi wahusika (walinzi) ambao hawatoi risiti ya Kielektroniki na wanapeana zamu kukaa eneo la hilo.

Wakiona 'jau' wanarejea na kuanza kutoa risiti, ni kama vile wanapeana zamu kula 'matunda'.
 
Naunga mkono hoja hii ni kweli Kabisa hata mwezi uliopita niliwaona kwa macho yangu
 
Sasa hv usipojenga au kununua kuwanja, na upo serikalini,huna bahati, serikali ya wezi hii,
 
Soma hii tajiri mmoja pale iringa amenunua 400 scania, na anazipeleka joberg zikajengewe tanks!,middle class humu ana lalama ni 200tsh za kigamboni bridge!,kuna fisadi kaua tembo 500 kapigwa faini na yupo huru,mlala hoi eti kakamatwa na vikilo 3 vya nyama (wanadai ya swala, wakati hawana majibu ya kisayansi kuthibitisha hii nyama kama ni ya swala)kahukumia 20yrs jela!!,tatizo la nchi hii niiwapumbavu wa middle class ambao wanajiona wamepatia maisha kisa ana ki ist na watoto wake wanaenda Choo kila siku, wanasahau kuwa huku lingusenguse watu wanalimia meno kwenye maisha haya
 
Unakuta wanakaba hizo mia mbili mbili walau jioni atoke na ya kununulia fungu la mchicha,hafanyi hivyo kwa kupenda
 
Unakuta wanakaba hizo mia mbili mbili walau jioni atoke na ya kununulia fungu la mchicha,hafanyi hivyo kwa kupenda
Exactly mkuu, sio kwamba naunga mkono hili ILA nimelifikiria upande wa pili wa coin, hawa ni walala hoi na sio kwamba watanunua v8 ni hivi 200tsh, wanajikimu tu kimaisha
 
Back
Top Bottom