Ndugu zangu nimefiwa na baba yangu

Pole sana kaka..! Kikubwa ni kumuombea kwa Mungu ili alale mahali pema peponi. Pia tunakuombea na wewe Mungu akutie nguvu kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na baba yetu mpendwa. AMEN
 

Pole sana ndugu yetu mungu akupe nguvu uweze kustahimili.
 
Ndugu Mungu akupe Moyo wa uvumilivu katika wakati huu mgumu na neema ya amani moyoni.
Mungu akutulize na akupe amani.
 
Inna Lillahi wa Inna ilaihi Raji'un
We belong to Allah and to Him we shall return


Pole sana mkuu.
 
Pole mkuu yote ni mapenzi ya mungu,sote tutapitia njia hiyo na tumuombee marehemu ili apokelewe vizuri kwenye makao ya milele juu mbinguni kwa MUNGU. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
I hope, from my heart, that your pain for the loss of your father will decrease, that your spirit will gain strength again, and I pray that your faith will create inner peace, and that God will send blessings!

Amen
 

Pole sana mkuu Mungu akutie nguvu kukabiliana ukweli huo. Bw ametoa bw ametwaa jina la bwan lihimidiwe. Ni wazi sasa kuwa majukumu yako yameongeza zaidi ukiwa kama mtoto wa marehemu.

Leadership yako inahitajika zaidi kwa sasa kuliko kabla. Omba Mungu atakusaidia kukabiliana na changamoto zilizo mbele yako.
 
pole mkuu! NAJUA UCHUNGU WAKUFIWA NA BABA MKUU!
MUNGU AKUJALIE UVUMILIVU MKUU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU!
 
Pole sana Cham. Katika kipindi hiki cha majonzi Mungu akupe faraja wewe na familia yako.
 

Pole sana kaka, Sote duniani tunapita,mtumaini Mungu atakupa faraja,matumaini na nguvu kwenye kipindi hiki kigumu kwako. Tunakuombea na sisi, tuko pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…