Ndugu zangu nimefiwa na baba yangu

Ndugu zangu nimefiwa na baba yangu

Ndugu yenu nimefiwa na baba yangu jana tar. 18/2/2011 muda wa saa 11 jioni kwa habari toka kwa ndugu zangu,
mimi ndugu yenu nipo nje ya TZ, ni vizuri kukaa mbali lkn yanapotokea mambo kama haya inaumiza sn, natamani ningekuwa nyumbani ningewahi mazishi kwani mazazi wangu amefia kijijini kwetu na nimbali na motuary, inaniuma sn kwani sitakuja uona uso wa baba yangu.
Hapa jamvini ni kwetu sote ni vema kupeana habari hizi.
Mungu awabariki sana.
Chamkey.

Pole sana kwa kufiwa na baba yako, inauma sana haswa ukiwa mbali. Nategemea ulikuwa na mawasiliano ya simu na mzazi wako kabla mauti hajamfika.

Tulia ujipange utafute njia ya kurudi moja kwa moja yaani upate kazi hapa nyumbani ili uwe karibu na mama aliyebaki mkiwa na ndugu wengine wa karibu uweze kuwapa mwanga wa maisha. yaani maisha hayatabiriki nikifikiri juzi nilivyopinda mbavu kwa kuhofia kufa kwa mabomu basi tu.
 
Pole sana Chamkey...MUNGU ndiye mpanga yote. pole pia kwa kuwa uko mbali. RIP Baba
 
Mkuu Pole sana. Hilo pigo silipaii picha!

Roho ya marehemu ipate rehema ya Mungu, apumzike kwa amani, AMEN!
 
pole sana mkuu,yote hayo ni mapenzi ya Mungu!Mungu akupe nguvu ya uvumilivu ktk kipindi hiki KIGUMU!
 
Pole sana , Mungu akutie Nguvu na kukufariji katika kipindi hiki kigumu.
 
Bwana ametoa na bwana ametwaa..jina lake lihimidiwe, naye Bwana akufariji na wote mlioguswa kwa namna moja ama nyingine na kifo hiki!
 
pole sana ndugu....!

roho yangu inahuzuni karibu ya kufa
 
HTML:
Ndugu zangu sijui nisemeje nilikuwa najililia mwenyewe toka jana usiku nikifikiri takuwaje ukijua kuwa huku umangani jpili siku yakazi ndipo niandike barua na sisi tuishio kwa kuajiliwa mpaka bosi aseme kwa kujibu barua lkn nashukuru kwani naona kila kitu kinaenda sw naamini kesho j2 nitatafuta ticket tayari kurudi nyumbani, najisikia huzuni lkn ndiyo maisha sina ujanja wa kupanda magari nakuunganisha,
ningependa kumwambia mmoja wa ndugu zangu, mie kwetu Dodoma, wilaya ya Kongwa Kijiji cha Golani lkn yeye amezikwa kijiji cha karibu Iduo.

Pole sana mkuu, siku zote kazi ya Mungu haina makosa bali ni kumuomba akupe nguvu na moyo wa uvumilivu.

Naamini wana JF walioko Dodoma mtatuwakilisha katika kumfariji mwenzetu mara atakapowasili.
 
Back
Top Bottom