Habari zenu? Natumaini wote wa forum hii hamjambo.
Kwa jina naitwa Ashery Jamal Masoud, nina miaka 57. Nilizaliwa hapa Dar es Salaam, na nimeishi hapa miaka yote kasoro kwa kipindi fulani nilipopata kazi Dodoma.
Hapo nimeamua kujieleza kwa sababu nawatafuta ndugu zangu na natumaini mtu mmoja anaweza kujitokeza kunisaidia.
Mama yangu Sara Mponela aliolewa na Mturuki baharia ambaye alinilea mpaka nilipokuwa na miaka 14 alafu akarudi kwao.
Mama mwenyewe aliwahi kutoroka nyumbani (Kisarawe?)kuja hapa mjini alipokuwa bado msichana, hii kwa sababu hakutaka kuolewa na Mzee kwa ndoa ya kupangiwa.
Hapa Dar es Salaam akakutana na Baba yangu na mwaka 1965 alipata mimba. Kwa hiyo alijaribu kurudi kwa ndugu zake lakini alikuta wengine walishahamia mjini, wengine walimchukia kwa mimba huo.
Na ndo maana hajataka mimi niwafahamu ndugu zangu, alisema walikuwa hawampendi na mimi pia hawatanipenda.
Mama yangu kwa bahati mbaya alifariki kwenye ajali ya meli Bukoba huko Mwanza mwaka 1996, na maiti haikupatikana.Angekuwepo, mwaka huu angekuwa na miaka 75 maana alizaliwa mwaka 1948.
Na mimi nimebaki peke yangu mpaka sasa hivi naangahika na kazi zangu za fundi umeme mitaani.Maisha yameenda si vibaya na nina kazi yangu najitegemea, na hela inanitosha kwa kuishi vizuri.
Mwaka jana nilipata ajali ya bodaboda na nikaumia mguu: nilipata operesheni lakini mguu haujakaa sawa. Kwa bahati nzuri nilikutana na mtu mkubwa ambaye nilifanyakazi kwake na alinionea huruma akaniahidi kwamba nikipata paspoti atanilipia matibabu nje ambayo yatanirudisha kwenye hali ya kawaida na uwezo wangu wa kutembea bila fimbo ambaye mpaka sasa naitumia.
Hapo nilipo naishi na akiba yangu na kazi ndogo ndogo na maisha yanaenda siyo vibaya lakini nawatafuta ndugu zangu.
Hawa ndugu tulipoteana nao si kwa ajili ya ugomvi bali kwa ajili ya matakwa ya Mama yangu marehemu.
Nikimpata ndugu yangu hata mmoja ntafurahi sana alafu itanisaidia kumtambulisha Mama yangu kwenye ofisi ya kuomba paspoti maana pale wameniambia kwamba wanahitaji mtu ambaye ni ndugu ya Mama yangu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Mama anaweza kutambulika.
Hapo nitaweza kupata paspoti, kwenda kutibiwa nje na kurudi mzima hapa nchini ili niweze kuendelea na maisha ya kawaida.
Naomba sana kama kuna mtu aliweza kumjua Mama yangu Sara Mponela na ni ndugu yake, ajitokeze basi:nitafurahi kumjua ndugu yangu mmoja na kujua kwamba sipo peke yangu dunia hii.
Samahani kama nimeeleza mengi lakini naamini kwamba kwa kutumia grupu hii yenye watu wengi nitaweza kubahatika kumpata ndugu yangu yeyote ambaye anaweza kukumbuka mambo niliyoadithia hapo.
Natanguliza shukrani kwa wote na Mungu awabariki katika maisha yenu.
Namba yangu ya simu ni: 0655-404494
Asante,
Ashery Jamal Masoud