Ndugu zangu, naombeni msaada kwa hili...

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Aug 10, 2021
2,035
2,682
Habari za humu ndani wana Jamiii Forums?

Niende moja kwa moja kwenye mada husika, nina jamaa yangu anaomba apewe ushauri kwa hili, ame ishi na mwanamke toka 2018 kipindi chote hicho amebahatika kupata watoto wawili, ameishi naye mda wote huo hata hakuwahi kujitambulisha kwa ndugu zake maana huyo mkewe wazazi wake wote wawili washatangulia mbele za haki. Amebaki na kaka zake wawili na dada zake wawili ila wote hao ni upande wa baba mdogo.

Hataki kujitambulisha kwao kwa kuwa hajaridhia kuishi naye, yaani kwa kifupi hajampenda. Mwanamke wake anaye ishi nae ni mtata sana(mkorofi), hamuheshimu, ana mdharau sana jamaa yangu, jamaa anaendelea kusema hata akitoka kazini anamkuta amelala, akimuhamsha amuwekee maji ya kuoga mwanamke anadai amechoka, hamsikilizi mmewe kwa kitu.

Ikitokea ameumwa jamaa yangu anahangaika kumuhudumia, akimpa pesa ya dawa mwanamke wake ana mpa shemeji yake akamlete dawa, mwisho wa siku dawa inabuma kumtibu jamaa anaingia mfukoni anatoa tena, maana asipo toa hapo ndani hapakaliki ni kelele mtindo mmoja.

Jamaa anasema hata akiacha hela ya matumizi mwanamke anasema haitoshi, kumbe kuna kanisa anapeleka huko wananunua mkaa na mawe. Nabii wa hilo kanisa anamuambia mkewe kuwa huo mkaa na hayo mawe yatamsaidia.

Akiacha pochi yake akienda kuoga anakuta mwanamke kamsachi kachukua hela, akimuuliza anasema hajachukua, mwanamke wake anapenda kukopa sana kila kona jamaa akipita anadaiwa yeye badala ya mkewe. Aliniambia mengi sana mengine hayana maana kuyaeleza huku nimeamua kufupisha.

Naombeni ushauri nzuri ndugu zangu jamaa afanyaje je, akimbie familia, au ampangishie chumba mwanamke kila mtu haishi kivyake maana anamkondesha jamaa kwa mawazo, anajuta kuishi naye.
 
Naomba ni assume kuwa ni wewe alafu ndio nikupe ushauri.

Sawa tuendelee Sasa. Mi naona matatizo Yako kwako wewe jamaa. Unataka afanye Nini kingine zaidi Ili ujue hukupangiwa kuishi na huyo mwanamke. Kilichopo hapo ni kuwa tu chemistry imechenga kati yenu. Bila kujali stori ni ya upande mmoja au vipi hapo hakuna mahusiano. Ni vyema Kila mtu akashika hamsini zake. Cha muhimu Vaa uanaume muite muweke chini mpange namna ya kulea hao watoto na Kila mtu ashike time zake.

Unajua haya maisha tumepewa Kila aina ya Furaha Ili Kila mtu apate Furaha aipendayo na amini nakwambia idadi ya Furaha zilizopo duniani zinatosha kabisa Kwa Kila mtu. Kwann kung'ang'ania kuishi sehemu paliposhindikana boss?
 
Naomba ni assume kuwa ni wewe alafu ndio nikupe ushauri.

Sawa tuendelee Sasa. Mi naona matatizo Yako kwako wewe jamaa. Unataka afanye Nini kingine zaidi Ili ujue hukupangiwa kuishi na huyo mwanamke. Kilichopo hapo ni kuwa tu chemistry imechenga kati yenu. Bila kujali stori ni ya upande mmoja au vipi hapo hakuna mahusiano. Ni vyema Kila mtu akashika hamsini zake. Cha muhimu Vaa uanaume muite muweke chini mpange namna ya kulea hao watoto na Kila mtu ashike time zake.

Unajua haya maisha tumepewa Kila aina ya Furaha Ili Kila mtu apate Furaha aipendayo na amini nakwambia idadi ya Furaha zilizopo duniani zinatosha kabisa Kwa Kila mtu. Kwann kung'ang'ania kuishi sehemu paliposhindikana
Mwanamke ana fanya makusudi ili jamaa akajitambulishe,na jamaa ataki kumuoa maana ajampenda,jamaa kaamua akaishi mbali anakuwa anamtumia ela ya matumizi tuu
 
Shauri kila mtu ila sio wana ndoa,tena ndoa ya hivi iliyobakisha Uzi ukatike.

Ukitia neno 1 tu kuna mawili umalizie kale ka uzi au uimarishe,experience inasema mara nyingi uzi humaliziwagwa na haya maushauri,staki yanikute.

Mkuu mimi nakuombea tu,inshaalah yataisha! Bwana Asifiwe...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom