Ndugu zangu huu ni ugonjwa au madhara tu ya pilipili?

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,827
4,076
Vipi hali zenu wakuu, kuna tatizo limemtokea brother, so nimeona nije hapa nitafute ufumbuzi wa tatizo kwa wale wanaofahamu aina hii ya tatizo.

Ipo hivi, brother wangu ni mlaji wa pili pili, japo sio ile ya ukali wa sana maana huwa anaogopa usipate huko baadae.

Juzi aliporudi nyumban alikuta mkewe amepika chapati na samaki. Muda wa kula ulipowadia wakaanza kula yeye mkewe na mtoto wao mmoja. Wakati wanakula brother yeye alikuwa anakula kivyake kwani yeye anatumia pili pili, wengine hawatumii.

Brother kutokana na utamu wa chakula akaona pili pili aliyoweka haitoshi akaongeza nyingine hadi ikawa kali kabisa. Baada ya kumaliza kula wakanawa na muda ulipofika wa kulala wakaingia kulala. Mida ya saa 8 usiku akaanza kuhisi tumbo linaanza kumsumbua akataka kujikaza lakini akaona hali inazidi ikabidi awahi chooni kujisaidia.

Ile anajisaidia akahisi tumboni kama kuna fukuto la moto moto fulani na haja yake ilikuwa ni ya kuhara. Baadae akaanza kuhisi kitu kama msumari kinashuka na kukwama sehemu ya kutolea haja kubwa. Kila alipojaribu kujikamua kile kitu hakitoki lakini kuharisha kama kawaida. Alijitahidi kutaka kukitoa hashiki kitu lakini akikaa anakisikia kipo na kinamletea maumivu.

Sasa ameshinda jana akajua tatizo litaisha, lakini mpaka leo bado linaendelea. Sasa aliponambia mimi nimemshauri asubiri niulizie kwa watu mbali mbali ambao wanaweza kuwa wanalifaham tatizo hilo, na ikishindikana itabidi aende hospital.

Maana bado anahisi kile kitu kimekwama maeneo ya kutoea haja kubwa na tumbo bado linamsumbua sumbua, yani linauma kwa mbali. So wengine tunahisi isije kuwa amepata tatizo la vidonda vya tumbo kutokana na ukali wa pili pili aliyotumia.

Sijui kama kuna watu humu washawahi kukumbana na hili tatizo na tiba yake ni nini? Dawa za kizungu au mitishamba? Karibuni tujadili tafadhali.
 
Mh hapa pagumu. Ma hizi ultra sound wanagusisha gusisha tu unaambiwa hakuna tatizo ngoja wataalamu zaidi waje.

Ila ninachojua mpaka mfupa uchome na kukwama kwenye kuta za puru huo hautakuwa mfupa wa kawaida labda kipande cha chuma chemye ncha kali
 
Si aende hospital ?Au hana bima ?
 
Mh hapa pagumu. Ma hizi ultra sound wanagusisha gusisha tu unaambiwa hakuna tatizo ngoja wataalamu zaidi waje.

Ila ninachojua mpaka mfupa uchome na kukwama kwenye kuta za puru huo hautakuwa mfupa wa kawaida labda kipande cha chuma chemye ncha kali
Ndo hapo brother anahisi labda pili pili, lkn wengine wanahisi huenda amekula kipande cha wavu wa kusugulia vyombo labda ulibaki ndani ya sifuria bila shemej kuona.
 
Kwa haraka haraka nilitaka kusema ana vidonda vya tumbo, sasa uchawi ni hicho kikichokwama hapo, mwambie akimbie hoapitali tu hakuna ujanja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom