Huu ugonjwa wa Gastritis sasa unanitesa mno

Tafakari_nami

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
779
1,517
Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.

Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.

Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.

Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
1704442824349.jpeg

Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.

Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.

Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.
 
View attachment 2862416

Habari!
Pole kwa kuumwa.

1: Picha uliyoitumia kuonyesha Gastritis ni ya Gastric ulcer/kidonda. Gastritis ni kututumka bila kidonda/ulcer.

2: Baada ya kuelekezwa tiba pale Regency:

A: Ulitumia tiba husika kwa mfululizo kwa siku kiasi gani?

B: Au umekuwa ukitumia tiba unapopata maumivu?

C: Upataji wako wa chakula kwa siku unazingatia muda halisi wa chakula?

D: Umezingatia vyakula vya jamii hii kutokuvitumia: kahawa, chai ya rangi, soda, juisi za nadukani, tangawizi nk.

E: Mtizamo wako juu ya kuumwa kwako ukoje/stress?

F: Ulishawahi kumwona daktari kwa mara nyingine baada ya kutumia tiba?

3: Majibu hapo juu yanaweza kutoa mwangaza wa nini kirekebishwe au kupata review/kumwona daktari tena na kulitizamaupya tatizo husika.
 
Mkuu pole sana,mimi huo ugonjwa kwa mwaka 2016-2020 umenitembeza sana hospital,ndanda hospital,(mtwara) baada ya kupewa referral kutoka Liwale-Lindi,ndanda walishindwa, ni kaandikiwa kwenda Mhimbili huko nilibainika kuwa na ugonjwa /tatizo kama lako,nilipewa dawa nyingi sana,zingine zilitaka kuniua.

Tatizo halikusha,ikabindi niende aghakani hospital,wapi,nikaenda hindu mandal-Mwanza wapi,nikaenda bugando hospital nikakutana na Doctor majimbe, niseme huyu ndo alikuwa chanzo cha mimi kupata nafuu,alinishauri kuhusu lishe,kula kwa wakati, sikupewa dawa nyingi sana ,pia alinikataza kunywa soda,kula maharage,maziwa,ndizi kwa namna zake,sukari nyingi kupita kiasi,pia kutoruhu hasira na huzuni ndani ya moyo wangu.

Baadae tatizo lilirudi tena,nikakutana na mtu akanishauri nitumie mlonge,ikumbukwe kwa wakati huo,nilizuiliwa kunywa soda, ndizi hapana,mboga iliyoungwa kwa viungo vingi hasa nyanya hapana,maharage, dagaa ,chakula kilicho lala nk.baada ya kutumia mlonge wa kununua kwa mwezi mzima nikianza kupata nafuu,nikaamua kuupanda huu mti nyumbani kwangu,nikaendeleza doazi kwa miezi miwili mfululizo ,hiyo ilikuwa kwaka 2021.

Baada ya hapo nikaanza kula maharage,maziwa nakunywa soda,dagaa nakula bila shida nk.

Ushauri wangu ni kuwa utashauriwa kuuziwa madawa mengi sana ya kienyeji lakini ni bure maana yanaweza kukuletea shida nyingine,hivyo mmea ambao madhara yake hayajathibitishwa kisayansi,kwani hata hao wanasansi wana usifu hadi sasa ni mlonge ,utumie huu mmea uone ,naimani utapona kabisa.

Mimi sasa nakula kila kitu ambapo hapo awali nilizuiliwa
 
Reply yako imenipa faraja sana mpaka nimehisi kupona, nime furahi sana kama kwa sasa hauna hii shida kabisa, nita tafuta huo unga muu, matumizi yake yapoje yaani kiasi gani ca kijiko, mara ngapi kwa siku ,a kwenye kikombe kiasi gani, maana kwa sasa nina tumia unga wa kokwa la parachichi asubuhi mchana na jioni kwenye kikombe kimoja cha chai ile dawa ya hospital nime acha kwa siku 5 mfululizo mpaka sasa ila sasa maumivu ndiyo balaaa kuchoka, ganzi, kichefuchefu ila nikirudi kwenye ile dawa ya hospital antacid inaitwa pantonex kidonge kimoja kwa siku ile asubuhi baada ya siku 3 au 4 napata nafuu, ila sasa ndiyo nakuwa mlemavu wa hizo dawa na siponi after miezi 2 au mwezi 1 nikianza kula vyakula vingine shida ina rudi so nakuwa najua mh hapa bado sijapona ila ni nafuu tuu nilikuwa nime pata. Sasa nauliza naweza kunywa huo mlonge huku natumia hizi dawa za antiacid maana nataka kuanzia kesho asubuhi nianze tena kumeza hizi antiacid huku nakunywa huu unga wa tangawizi maana nasikia wengi wanasema ume wasaidia pia, ila nataka kuanza kutumia huo mlonge kama wewe ume kusaidia na mimi nina imani nitapona nitoke kwenye hii shida jamani maana unateseka kuliko kawaida.
 
Habari!
Pole kwa kuumwa.

1: Picha uliyoitumia kuonyesha Gastritis ni ya Gastric ulcer/kidonda. Gastritis ni kututumka bila kidonda/ulcer.

2: Baada ya kuelekezwa tiba pale Regency:

A: Ulitumia tiba husika kwa mfululizo kwa siku kiasi gani?

B: Au umekuwa ukitumia tiba unapopata maumivu?

C: Upataji wako wa chakula kwa siku unazingatia muda halisi wa chakula?

D: Umezingatia vyakula vya jamii hii kutokuvitumia: kahawa, chai ya rangi, soda, juisi za nadukani, tangawizi nk.

E: Mtizamo wako juu ya kuumwa kwako ukoje/stress?

F: Ulishawahi kumwona daktari kwa mara nyingine baada ya kutumia tiba?

3: Majibu hapo juu yanaweza kutoa mwangaza wa nini kirekebishwe au kupata review/kumwona daktari tena na kulitizamaupya tatizo husika.
Asante kwa reply yako mkuu, after pale regency dawa nilitumia kwa miezi 3 mfululizo nikapata nafuu kubwa tuu, sasa nika anza kula vyakula vya kawaida hivi na juisi na soda mara 1 1 ila sasa baada ya muda ugonjwa ukarudi upya sasa nimekuwa mlevi wa ivyo vidonge bila hivyo siwezi kaa sawa, kurudi hospital hapana maana sikurudi, mimi nikiona nimezidiwa naenda nunua antacid after one week napata nafuu ila lazima niendelee kumeza hizo dawa kila siku sasa ina fika muda nina jiuliza hiyo itakuwa mpaka lini, na pia hizo dawa zina side effects mfano nikitumua dawa hizo kama wiki 3 mfululizo kichwa kinakuwa kizito sanaaa nika angalia shida nini nika kuta hizo dawa zina fanya mwili unakosa vitamin B12 , n kuna mtu mwingine namjua ana umwa huu ugonjwa kabla yangu akaniambia shida ni hizo dawa ndiyo maana kichwa kinakuwa kizito au kuuma na nikia cha kumeza hizo dawa kichwa kina funguka japo maumivu ya tumbo yana rudi upya na kufanya na mateso kuendelea, stress za hapa na pale zipo siyo uongo.
 
Reply yako imenipa faraja sana mpaka nimehisi kupona, nime furahi sana kama kwa sasa hauna hii shida kabisa, nita tafuta huo unga muu, matumizi yake yapoje yaani kiasi gani ca kijiko, mara ngapi kwa siku ,a kwenye kikombe kiasi gani, maana kwa sasa nina tumia unga wa kokwa la parachichi asubuhi mchana na jioni kwenye kikombe kimoja cha chai ile dawa ya hospital nime acha kwa siku 5 mfululizo mpaka sasa ila sasa maumivu ndiyo balaaa kuchoka, ganzi, kichefuchefu ila nikirudi kwenye ile dawa ya hospital antacid inaitwa pantonex kidonge kimoja kwa siku ile asubuhi baada ya siku 3 au 4 napata nafuu, ila sasa ndiyo nakuwa mlemavu wa hizo dawa na siponi after miezi 2 au mwezi 1 nikianza kula vyakula vingine shida ina rudi so nakuwa najua mh hapa bado sijapona ila ni nafuu tuu nilikuwa nime pata. Sasa nauliza naweza kunywa huo mlonge huku natumia hizi dawa za antiacid maana nataka kuanzia kesho asubuhi nianze tena kumeza hizi antiacid huku nakunywa huu unga wa tangawizi maana nasikia wengi wanasema ume wasaidia pia, ila nataka kuanza kutumia huo mlonge kama wewe ume kusaidia na mimi nina imani nitapona nitoke kwenye hii shida jamani maana unateseka kuliko kawaida.
Hizo kokwa achana nazo ni uhuni tu,mlonge umenisaidia,parambannda lingeshapigwa kwangu,tia kijiko kimoja cha chakula kwenye maji ya moto kikombe cha chai,acha yapoe kisha kunywa,kutwa mara tatu,ni majani ya mlonge ,endelea na dozi hadi pale utakapoona nafuu,

Ukizembea hata shemeji atakukimbia maana jogoo huwa anaishiwa nguvu,nguvu za kiume kwa mwanamme ziko tumboni,huwezi fanya kazi ikiwa tumbo lako si salama
 
Kabla ya kula kwa maana tumbo likiwa empty au baada ya kula ndiyo ninywe iyo dawa, maana dawa nyingine si unajua zina masharti uta ambiwa kula kwanza au nyingine usile kwanza. na kama kuna tahadhari nyingine juu ya hiyo dawa naomba niambie ili nianze hiyo dozi. Pia swali langu naweza tumia huo mlonge uku nikiendelea kumeza hii dawa ya hospital ya antiacid au wewe ulikuwa hautumii kabisa antiacid. Asante sana
 
Kutwa mara 3, before or after taking food
 
Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.

Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.

Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.

Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
View attachment 2862416
Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.

Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.

Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.
Kunywa maji ya birika lako mwenyewe kama wewe ninmwanamme na kama ni mwanamke kunywa ya kisima chako mwenyewe kama aandikivyo mfalme Suleiman mithali 5:15,

Hiyo ni tiba ya urine therapy inayotumiwa na wachina na wahindi Kwa miaka mingi sana!!

Unakunywa ule was asubuhi na mapema saa kumi na mbili,au na Moja au saa kumi hata lita Moja au nusu lita! Kutikana na uwezo wako!!

Hakuna hospital inayotibu vidonda vya tumbo zaidi ya kutuliza TU vina rudi!

Kunywa Kwa siku saba!

Case study;-

Nilikua naamka usiku wa mane tumbo linauma na kukata sana yaani silali Hadi asubuhi,siku moja staff member akaniambia hebu kunywa Omeprazole likitulia ujue ni vidonda vya tumbo!

Bas siku nikanywa likatulia nikajua ni huo mzigo!

Nilichaeki Makala YouTube ya tiba ya mkojo wako mwenyewe nikaona kinyaa,then nikagoogle urine therapy nikakuta andiko na mzungu mmoja alianzisha huo utaratibu na wachina na wazee was zamani walitumia sana,nilitumia hiyo kitu Hadi leo sijahisi maumivu tena!!
 
Dawa mbadaIa ya kwanza, ni kunywa maji ya moto kuanzia unapoamka na kila unapohitaji maji ya kunywa na zaidi.

Wacha kutumia maji na vinywaji baridi.

Maji ya moto kama vile ya kupikia chai.

Anza na tiba hiyo mbadala utuletee mrejesho baada ya mwezi.
 
Au kama una tengeneza niambie mkuu au una jua sehemu wanauza nitashukuru pia.
Suruhisho ni kupanda Mti wako,huwezi himili bei yake kwa dozi ya mwezi mmoja hadi miwili maana kijiko kimoja ni sh 1000,sasa ili kuepuka hili panda mti wako,ukiutunza vizuri ndani ya miezi mitatu unakuwa uko tayari kuvunwa
 
Hapa mtaani Suruhisho ni kupanda Mti wako,huwezi himili bei yake kwa dozi ya mwezi mmoja hadi miwili maana kijiko kimoja ni sh 1000,sasa ili kuepuka hili panda mti wako,ukiutunza vizuri ndani ya miezi mitatu unakuwa uko tayari kuvunwa
Hapa mtaani upo huo mti, sija jua tuu namna ya kuandaa huo unga, itabidi nijifunze namna ya kuuandaa. Asante sana nimefarijika mno
 
Dawa mbadaIa ya kwanza, ni kunywa maji ya moto kuanzia unaposlamka na kila unapohitaji maji ya kunywa na zaidi.

Wacha kutumia maji na vinywaji baridi.

Maji ya moto kama vile ya kupikia chai.

Anza na tiba hiyo mbadala utuletee mrejesho baada ya mwezi.
Nita anza tiba mbadala maana sikuwahi tumia tiba mbadala kabisaa zaidi ya dawa za ospital tuu. Nitakuja rudisha mrejesho hapa.
 
Kunywa maji ya birika lako mwenyewe kama wewe ninmwanamme na kama ni mwanamke kunywa ya kisima chako mwenyewe kama aandikivyo mfalme Suleiman mithali 5:15,

Hiyo ni tiba ya urine therapy inayotumiwa na wachina na wahindi Kwa miaka mingi sana!!

Unakunywa ule was asubuhi na mapema saa kumi na mbili,au na Moja au saa kumi hata lita Moja au nusu lita! Kutikana na uwezo wako!!

Hakuna hospital inayotibu vidonda vya tumbo zaidi ya kutuliza TU vina rudi!

Kunywa Kwa siku saba!

Case study;-

Nilikua naamka usiku wa mane tumbo linauma na kukata sana yaani silali Hadi asubuhi,siku moja staff member akaniambia hebu kunywa Omeprazole likitulia ujue ni vidonda vya tumbo!

Bas siku nikanywa likatulia nikajua ni huo mzigo!

Nilichaeki Makala YouTube ya tiba ya mkojo wako mwenyewe nikaona kinyaa,then nikagoogle urine therapy nikakuta andiko na mzungu mmoja alianzisha huo utaratibu na wachina na wazee was zamani walitumia sana,nilitumia hiyo kitu Hadi leo sijahisi maumivu tena!!
Sawa mkuu nita fanya na hii nione maendeleo yakoje mkuuu. Asante sana
 
Hapa mtaani upo huo mti, sija jua tuu namna ya kuandaa huo unga, itabidi nijifunze namna ya kuuandaa. Asante sana nimefarijika mno
Kama upo DAR, ukienda kwenye supermarket yoyote kubwa utapata unga wa majani ya mlonge wamepaki vizuri kwenye packet au chupa. Bei yaweza kuwa kama 10k.
Kwa jinsi ulivyosema unaumwa, nahisi unahitaji kuanza hiyo tiba mapema
 
Back
Top Bottom