Ndugu wasio na shukrani!

Ndugu wasio na shukrani!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,105
Reaction score
136,784
Hivi na nyie wengine mnao ndugu wasio na shukrani?

Ndugu ambao hukukumbuka wakati wa shida zao tu?

Huwa mnakabiliana nao vipi watu wa aina hiyo?

Mimi wananikera sana kwa kweli.

Mtu anakuja na kukulilia shida zake lukuki, nawe kwa moyo mweupe kabisa unamsaidia.

Tena unamsaidia kwa kwenda mbali zaidi ya kile alichokiomba.

Cha ajabu [ingawa si ajabu kivile] ukishamsaidia tu, mwenzio anapotea.

Anapotea bila hata kutoa 'ahsante' ya msaada uliomsaidia.

Na akishapotea ndo imetoka hiyo. Kuja kusikia tena toka kwake labda ni awe na shida au kwenye msiba.

Hata salamu tu ya kujuliana hali toka kwake inakuwa tunu.

Naamini katika kutenda wema na kwenda zangu lakini pia sipendi mambo ya kufanyanya wapumb.avu.

Yaani kuniona nakufaa tu wakati wa shida zako. Ukiwa huna shida hata simu zangu hupokei.

Hovyo kabisa hao.....
 
kutoa msaada ni aina ya moyo uliopewa na Mungu.

Ni zaidi ya kipaji

ni karama

Ni zaidi ya uponyaji wa mwili maana ni uponyaji wa roho

UBARIKIWE SANA

NB: kwa maana nyingine kama umeumbwa na moyo huo, raha yako ni kuwasaidia na ikitokea mtu anahitaji msaada wako na wewe ukajikausha, basi roho itakuuma sana.

umejaliwa kupata ili utoe...toa maana pale unapotoa ndo panazidi kujaa

angalizo: mkono unajikuna pale unapofikia...hope you get me right American baby Nyani Ngabu
 
Ukitoa toa Tu pasipo kusubiri Shukrani!
 
True that, ndugu wengine wanapenda kugeuzana xhamba la bibi, huo sio uungwana, tubadilike watz
 
Hawa ndugu waliniacha hoi siku nilipo wajibu kwamba sina, eti wakanuna.
Hapo ni baada ya kua nimewasaidia kwa miaka mingi, pamoja na kuwajengea nyumba na kuwasomeshea watoto wao.
Niliwachoka pale nilipo wapa vimiradi, then wakaviua
 
Wengine ukiwaambia huna wanaanza kukusema eti uko mchoyo.

Wahshi kabisa.
 
pengine nyie mkiona simu tu za ndugu zenu ambao ni masikin mnajua huyu anashida na anataka pesa

haiko hivyo wengine wanataka kuwa salim tu

kwahiyo nyie pia kwa namna moja au nyingine mnachangia kuleta hali hii
 
Ndugu ni ndugu na ndiyo undugu wenyewe huo mmoja akitoka, basi inaaminika kwamba umefungua njia.

Mimi ndugu zangu hua wanastukia tu kuniona nipo around na ntakuwa na ratiba zangu.

Huwa nawaambia kwamba msaada mkubwa kutoka kwangu ni kukusaidia ada ya kozi (ku-top up) unayosoma yenye kuja kukusaidia maishani au kunisaidia shughuli zangu za shamba au kukusaidia mawazo ya ujasirimali.

Halafu wanafahamu siwezi kukusaidia tu bila kuja na business plan, kama kuwa na Barber shop, hair dressing saloon, grosery shop na aina yoyote ile ya biashara.

Lakini mimi sio benki kwani wengine wanaomba hata mitaji kabisa kama 10,000,000 hivi.

Sasa hii si anaweza kuipata akienda benki na business plan yake?

Ila siwasahau ndugu zangu kwa vitu vidogovodogo ambavyo ukiwapa anaweza kuwa nacho wakati wote kama kofia, top original ya Arsenal na handset ya kawaida.

Akiwa nacho anakuwa akikukumbuka kwamba ndugu upo.

Halafu mkuu NN, jaribu kuwaunganisha ndugu zako kwenye WhatsApp Group ndiyo utaona hizo feeds za maombi na utaweza kuchuja zipi za kuzingatia.

WhatsApp inaleta togetherness baina ya ndugu na mnakuwa mkiwasiliana kila mara.

Hizo feeds zingine unapotezea tu.
 
...hatuwatafuti mara kwa mara coz kila mkiona calls zetu mnadhani tunataka kusaidiwa, kumbe masikini ya Mungu tunataka kuwajulia hali tu.

Ukiwa na ndugu wenye uwezo ni bora mkutane kwenye "shughuli" tu, wengi nyodo zimezidi, kila akitoa senti kumi anatangaza kwa marafiki na ndugu wenye uwezo kuwa kakusaidia....

I'd rather be masikini jeuri.
 
Hivi na nyie wengine mnao ndugu wasio na shukrani?

Ndugu ambao hukukumbuka wakati wa shida zao tu?

Huwa mnakabiliana nao vipi watu wa aina hiyo?

Mimi wananikera sana kwa kweli.

Mtu anakuja na kukulilia shida zake lukuki, nawe kwa moyo mweupe kabisa unamsaidia.

Tena unamsaidia kwa kwenda mbali zaidi ya kile alichokiomba.

Cha ajabu [ingawa si ajabu kivile] ukishamsaidia tu, mwenzio anapotea.

Anapotea bila hata kutoa 'ahsante' ya msaada uliomsaidia.

Na akishapotea ndo imetoka hiyo. Kuja kusikia tena toka kwake labda ni awe na shida au kwenye msiba.

Hata salamu tu ya kujuliana hali toka kwake inakuwa tunu.

Naamini katika kutenda wema na kwenda zangu lakini pia sipendi mambo ya kufanyanya wapumb.avu.

Yaani kuniona nakufaa tu wakati wa shida zako. Ukiwa huna shida hata simu zangu hupokei.

Hovyo kabisa hao.....
Mweleze ukweli.
 
Back
Top Bottom