activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
Habari ndugu wanajf,naomba mniwie radhi kama nitakuwa sina mpangilio mzuri wa andiko hili.
Nimekuja hapa jf nikiamini ni mahali pekee nitakapopata ushauri ambao utanisaidia kuiokoa ndoa yangu.
Yapata mwaka na nusu sasa tangu nifunge ndoa na mume wangu kipenzi,tumejaliwa kupata mtoto mmoja wa miez 6 sasa.Tangu nifunge ndoa ndugu wa mume hawachoki kuja nyumban kwangu kutoka kijijini kwao huko singida,mwanzo ndoa yetu ilikuwa na furaha mno ila tangu movements za hawa ndugu naona dosari zinaanza.
Wamekuwa ni watu wasiokuwa na fadhila hata kidogo,wamekuwa walalamishi mno.mbaya zaid wamekuwa wakipeleka maneno ya uongo kwa kaka yao hususan pale ndugu na rafik zangu wakija kunitembelea wanasikiliza maongez yetu(maongez ambayo ni ya kawaida sana ndo maana huwa tunaongea mbele yao) wanadai kuwa ndugu zangu wananipa kiburi sasa cjui kiburi cha nn maana naish nao vizuri na kuwajali vizuri tu.
Nashindwa kuelewa lengo haswa la hawa ndugu ni nini maana sasa hivi wanakuja kwa kupokezana utafikir wanalinda kitu.Mume wangu huwa analalamika kuja kwao ila yeye ndiye anawatumia nauli sasa cjui ananijaribu?? Ila siku zote huwa nakaa kimya pale anapolalamika.
Nimejua wao ndo wachonganishi maana kuna mmoja kati yao ananipenda sana hivyo huwasikiliza wenzie na kuja kuniambia,nikajaribu kuwa busy na mambo yangu wanalalamika tena hadi mume wangu akaniambia niwe napiga nao story maana wanalalamika...hilo pekee ndilo aliloniambia ila sijaweza kumwambia sababu ya mimi kuwa mbali nao sitaki kuwachonganisha.
Mambo mengne wanayopeleka kwa kaka yao sijui hata wanayapata wapi!! Naona tu mume wangu anakuwa na hasira zisizoisha,mbaya zaid na yeye ni mtu wa kukaa na vitu moyoni.
Naipenda ndoa yangu na nataka kuinusuru...maana nimeanza kuwachukia hawa ndugu kutokana na matendo yao.Nifanyaje wanaJF??
Naomben ushauri wenu ili niinusuru ndoa yangu.Mume wangu ananipenda sana na mimi nampenda sana.naomben msaada wenu.