Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

Ndugu wa 'mume' wa Ufoo waja na mapya

Picha plz...
Au laa piga kimya...

Mkuu unataka picha ya jehanamu? Joto Approx. 35,000,000℉ mzee. Hakuna Camera itaweza vumilia kabla haija undergo sublumation change (Solid to Vapour, bila kupitia gas state)
 
Katika Bastola zinazomilikiwa kihalali,
% kubwa zinatumika kwenye issue za malovee zaidi kuliko kuulia majambazi, shame on you owners!!!

Ushauri: Zitolewe kwa walio single Tu.
 
Sasa kama ilitokea purukushani na jamaa akadhania ufo amefariki sasa ilikuwaje mpaka akakimbia kwa uyo fundi samani na kuomba msaada? Hapa ---- mengi ya kuelezwa na si kuchukua majibu rahisi tuu..
Na yule mdada alisema alikuwa juu ya dari? Na je kuna matundu yeyote ya risasi kwenye ukuta?
 
Ndugu wa mume waja na mapya

09:49

NA JESSICA KILEO
FAMILIA ya aliyekuwa mzazi mwenzake, Mwandishi wa ITV na Radio One, Ufoo Saro, Anthery Mushi (40), imevunja ukimya na kudai inapata wakati mgumu kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe.

Imesema suala hilo inaliachia Jeshi la Polisi lishughulikie ili kubaini undani wake.

Kaka wa marehemu, Isaya Mushi alidai hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wawakati mwili wa Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi na kumuua mama mkwe wake, Anastazia Saro pamoja na kumjeruhi mchumba wake Ufoo, ukiagwa.

Mushi alidai wapo katika wakati mgumu wa kuamini kwamba ndugu yao alijiua mwenyewe, k
wani haiwezekani mtu akajipiga risasi sehemu mbili ambazo ni kidevuni na upande wa bega la kushoto.

Alidai sio kazi yao kutoa hukumu, kwani wanasubiri upelelezi wa polisi kutoa jibu lililo sahihi kuhusiana na tukio hilo.

Baada ya kifo cha ndugu yetu, wanafamilia tulifanya uchunguzi wa awali na bado linatuwia vigumu kutambua upi ni ukweli kuhusu jambo hilo kuhusiana na kifo hiki,î alidai.

Kaka huyo alidai katika uchunguzi wa madaktari, walibaini kuwa marehemu alijipiga risasi mbili sehemu tofauti.

Akisoma risala kwa waombelezaji, Mushi alidai marehemu alizaliwa Januari 3, 1973 katika kijiji Uru Ongoma Timbirini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mushi alisema alisoma Shule ya Msingi Ongoma Timbirini kutoka mwaka 1981 hadi 1987 na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Zanzibar na baadaye alisoma kozi mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari.

Alisema mwaka 1994 alijunga na Kituo cha Televisheni cha ITV na mwaka 2002 alikwenda STR na hadi mauti inamkuta alikuwa akifanya kazi Umoja wa Mataifa, Sudan, akiwa mtaalamu wa habari.

Kwa upande wake, dada wa marehemu, Eviolatha Mushi alisema alipokea kwa masikitiko msiba wa mdogo wake kwa sababu alikuwa mtu mwelewa na msikivu katika jamii ambayo wamekulia.

Eviolatha alitoa wito kwa wanandoa kumshirikisha Mungu katika maisha yao na sio mwanadamu, hali itakayosaidia kutatua matatizo wanayopitia kwa kuwa neno la Mungu linasema kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke lazima atalamba mauti, hivyo hawana budi kukubaliana na neno hilo.

Naye, mdogo wa marehemu, Happy Mushi, alisema hadi sasa hawezi kuamini chochote hadi polisi itakapotoa majibu ya upelelezi .

Alisema Oktoba 9, mwaka huu, marehemu alimpigia simu na kumwambia anamshukuru Mungu, kwani ametoka kufanya kazi katika mazingira magumu, hivyo muda si mrefu anaweza kuhamia Tanzania, na kwamba yupo nchini kwa ajili ya kumalizia nyumba yake ambaye ipo Mbezi, Dar es Salaam.

Lakini cha kushangaza kabla ya wiki alisikia katika vyombo vya habari vikitangaza kaka yake amejiua mwenyewe pamoja na familia ya mke wake,î alisema.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda kijijini kwao Ongoma Timbirini na unatarajiwa kuzikwa leo.

Wakati huo huo, Ufoo aliyelazwa Muhimbili hali yake imetengemaa na ameanza kutembea pamoja na kwamba daktari anayemhudumia anakataza watu kuingia kumtazama.

Ofisa wa Habari wa MNH, Aminiel Eliegaisha, alisema jana kuwa, Ufoo anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya kutembea, ingawa bado hawajaanza kuwaruhusu watu kwenda kumtaza kwa sababu ameshonwa sehemu nyingi na kwamba wanahofia kidonda kutokupona haraka.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Oktoba 13, mwaka huu, eneo la Kimbamba nyumbani kwa wazazi wa Ufoo, ambapo alikwenda akiwa na mzazi mwenzake Anthery Mushi.

Mushi alimuua mama wa Ufoo kwa kumpiga risasi zinazosadikika tano na kumjeruhi kabla ya kujiua mwenyewe.

source: Uhuru Online

Hata kama uchunguzi ukibaini kua Ndugu yao alijiua mwenywe bado ni tatizo maana tayari ndugu ni kama wameshatoa hukumu kua inawapa wakati mgumu kuamini kua Ndg yao kajipiga risasi mwenyewe!
 
Nimekuwa naperuzi huku na kule kuhusu hizi habari, napata zenye face tofauti tofauti, sasa hapa nitaomba Mods wasini-BAN maana nimepick info fulan kwenye chanzo kisicho rasmi (personal communications) ili kwa wenye taarifa sahihi waniprove wrong ama right, if zitakuwa siyo sahihi basi i/we must take them as illussions and falsifiable allegations, nanukuu aya ndogo ya hyo taarifa......
"Sasa kukawa na plot ingine hapa ya kujengwa ambayo ni hy anayokaa mama...mushi wakat house inajengwa anatumiwa photos za progress
Kurud kumbe hola akauliza mama kamjibu 'nyumba ni ya alvin, ww huna kitu labda vihela vidogo tuuu visenti, fanya ufanyalo'
Ndio akafungua bag akatoa pastola ndio akaanza kuwashoot..." Mwisho wa kunukuu.
Siwezi kuweka habari nzima ilivyo maana kama nilivyotangulia kusema chanzo cha habari sio rasmi (not the one you can bring here as reference)
Na sehem nyingine ya habari hii inamtaja huyo mwanaume Part II anayehusika, sasa kwa 7bu hizi habari sio rasmi naomba nihifadhi hilo jina maana nikiliweka hapa umma wa JF mioyo itafanya paaaaaaaaah!

Note; take this as hearsay and not the proof wadau.
 
Hii taarifa hata mimi nimetumiwa kwenye viber ikimtaja mwanasiasa mmoja maarufu kama ndiye aliyekuwa rafiki wa Ufoo. If there is any truth in this, I don't know. Time will tell.
 
kweli kuna utata katika kifo hicho mtu hawezi kujipika risasi mara 2
tusubiri uchunguzi uendelee ndiopo tutagundua ukweli wake
 
Nimekuwa naperuzi huku na kule kuhusu hizi habari, napata zenye face tofauti tofauti, sasa hapa nitaomba Mods wasini-BAN maana nimepick info fulan kwenye chanzo kisicho rasmi (personal communications) ili kwa wenye taarifa sahihi waniprove wrong ama right, if zitakuwa siyo sahihi basi i/we must take them as illussions and falsifiable allegations, nanukuu aya ndogo ya hyo taarifa......
"Sasa kukawa na plot ingine hapa ya kujengwa ambayo ni hy anayokaa mama...mushi wakat house inajengwa anatumiwa photos za progress
Kurud kumbe hola akauliza mama kamjibu 'nyumba ni ya alvin, ww huna kitu labda vihela vidogo tuuu visenti, fanya ufanyalo'
Ndio akafungua bag akatoa pastola ndio akaanza kuwashoot..." Mwisho wa kunukuu.
Siwezi kuweka habari nzima ilivyo maana kama nilivyotangulia kusema chanzo cha habari sio rasmi (not the one you can bring here as reference)
Na sehem nyingine ya habari hii inamtaja huyo mwanaume Part II anayehusika, sasa kwa 7bu hizi habari sio rasmi naomba nihifadhi hilo jina maana nikiliweka hapa umma wa JF mioyo itafanya paaaaaaaaah!

Note; take this as hearsay and not the proof wadau.

Mkuu mtaje tuu uyo mheshimiwa ila ukwel uzidi fuatiliwa, la tuwaite jicho pevu watusaidie? Kwa sababu huku ni kutumia madaraka yao hovyoo na huyu ufoo kama ana mimba kweli tuu, ajue ana laana hata kama jamaa aliwapiga risasi kweli. Anataka kuleta ujanja wa kula viwili kwa wakat 1...?
 
Hii taarifa hata mimi nimetumiwa kwenye viber ikimtaja mwanasiasa mmoja maarufu kama ndiye aliyekuwa rafiki wa Ufoo. If there is any truth in this, I don't know. Time will tell.

Hapa sasa ndio utamu unaanza. Ebu mkuu create fake account kwa muda then mtaje hafu hiyo account achana nayo.
 
Hapo wenye ushahidi ni marehemu wawili hakuna kesi hapo! Get well soon Ufoo uje kuripoti mikutano ya Chadema!
 
Strange! Risasi mbili utajipigaje? Behind the sene!

inawezekana akajipiga hata 3. kuna tukio lilitokea hapo sinza darajani dereva wa daradara alipigwa risasi na mtu wa boda boda lakini alikuwa anacheka na akaendesha gari kama hatua kumi na tano kabla ya kupoteza fahamu na hatimaye kufa: pia angalia picha ya kifa cha muhamari gadafi wa libra jamaa alimpiga risasi ya kwanza upande wa sikio na gadafi akawa anashaanga damu inayomtoka akaongezwa ya pili akawa analalamika mpk amekufa; niliwahi kumuuliza Dr mmoja pale OSHA akaniambia mtu akipata maumivu makubwa huwa hawezi kuyasikia hapo hapo mfano kuvunjika mguu nk no unaweza kuanza kushaaanga kipande cha mkono kumbe ni cha kwako.
 
Niliwahi kuona movie ya Nigeria maiti inakabidhiwa shoka kabla ya kuzikwa then inazikwa na hiyo shoka. Huwezi amini hilo shoka lilikuja kuwaua wote walioshiriki kumuua huyo jamaa. kama vipi Mushi naye akabidhiwe shoka tu inawezekana ikarudi kuwabeba hao wengine (kama wapo).
Nimetoa huu mfano maana kwa polisi hawa hawa wakina Kova na wenzie, haitegemewi tupate uchunguzi wa kweli kizingatiwa kuwa maiti huwa haiongei. kila kitu inasukumiwa maiti.
 
Back
Top Bottom